Monday, March 30, 2009

Chenge Akiri Kumjua Marehemu Vicky

...Afikishwa Mahakamani Kinondoni

MBUNGE wa Bariadi Magharibi na mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge amekiri kuwa anamfahamu Vicky George Makanya, ambaye ni mmoja wa wanawake wawili waliofariki katika ajali iliyohusisha gari lake mwishoni mwa wiki iliyopita.Habari Kamili. Wakati huo huo, Chenge leo amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka, taarifa zaidi ziko hapa kwa Mzee wa Mshitu

Sunday, March 29, 2009

Eti Chenge Anawajua Aliowaua

Hawa ndio wanawake waliogongwa na Andrew Chenge na kufa hapo Ijumaa iliyopita. Vicky (kushoto) na (Beatrice kulia)


Frederick Katulanda, Mwanza

SAKATA la ajali ya gari la Andrew Chenge ambalo limesababisha vifo vya wanawake wawili, limeingia katika sura mpya baada ya ndugu wa wasichana hao kudai kuwa Chenge alikuwa akimfahamu mmoja wa marehemu.
Chenge ambaye alikuwa Waziri na Mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, aliingia matatani baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga "bajaji" usiku wa kuamkia juzi na kuua wanawake wawili ambao ni Beatrice Costantine (kulia) ambaye ni mfanyabiashara wa Mwanza na mmiliki wa saluni ya kike na Vicky George Makanya (kushoto).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Mwanza baadhi ya ndugu waliohojiwa na Mwananchi Jumapili akiwamo mama mzazi wa Vicky, walisema wanafahamu Chenge kuwa alikuwa akimjua ndugu yao Vicky. Mwananchi Jumapili limeandika kwa kirefu.

Friday, March 27, 2009

Kikwete abadili ma-DC

27 Machi, 2009

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya chini kwa kuwateua wapya 15, kuwastaafisha wengine saba na kuwabadilisha vituo vya kazi 54.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) imeonyesha pia kuwa Wakuu wa Wilaya wawili watapangiwa kazi nyingine na wengine wawili wameteuliwa hivi karibuni kuongoza Jumuiya za Chama Tawala.

Mabadiliko haya yanatarajiwa kuongeza chachu katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa ni Bi. Mercy Silla (Arumeru, Arusha), Bw. Norman Sigalla (Hai, Kilimanjaro), Col. Issa E. Njiku (Misenyi, Kagera), Bi. Angelina Mabula (Karagwe, Kagera), Dkt. Rehema Nchimbi (Newala - Mtwara), Francis Isaac (Mbulu, Manyara), Lt. Col. Benedict K. Kitenga (Rorya, Mara) na Lt. Col. Cosmas Kayombo (Mbarali, Mbeya).

Wengine ni Bw. Christopher Ryoba Kangoye (Kwimba, Mwanza); Bi. Queen Mwanshinga Mlozi (Ukerewe, Mwanza); Bi. Fatuma Mwassa (Mvomero, Morogoro); Bi. Fatma Ally (Nanyumbu, Mtwara); Bw. Juma Solomon Madaha (Tunduru, Ruvuma); Bw. Anatory Choya (Kishapu, Shinyanga) na Bw. Erasto Sima (Korogwe, Tanga).

Wakuu wa Wilaya waliostaafishwa na vituo vyao kwenye mabano ni Bw. Elias Maarugu (Misenyi, Kagera); Bw. Deusdedit Mtambalike (Muleba, Kagera); Bw. David Holela (Babati, Manyara); Bi. Hawa Ngulume (Mbarali, Mbeya); Bw. Mashimba H. Mashimba (Kyela, Mbeya); Col. Peter Madaha (Nyamagana, Mwanza) na Bw. Gilbert Dololo (Kibaha , Pwani).

Wakuu wa Wilaya ambao wamepangiwa kupewa kazi nyingine ni Bw. Patrick Tsere aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (Dar es Salaam) na Bi. Doreen Kisamo aliyekuwa Uyui (Tabora).

Bw. Martin Shigela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi (Lindi) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM wakati Bi. Husna Mwilima aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai (Kilimanjaro) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UWT.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
IJUMAA, MACHI 27, 2009.

Chenge asababisha vifo viwili

Bima ya gari lake ilimalizika Juni 06, 2007


Waziri wa zamani wa Miundombinu, Andrew Chenge yuko matatani tena; safari hii gari alilokuwa akiendesha limegonga "bajaji" na kuua wanawake wawili.
Lakini Jeshi la Polisi limeamua kupumzisha taratibu zake za kawaida za kulipeleka suala hilo mahakamani kushughulikiwa kama kosa la usalama barabarani na kuunda tume ya kuchunguza ajali hiyo.

Anna Kilango Ule uleee

The United States Chargé d’Affairés Larry André (right) presents a certificate to Member of Parliament for Same East constituency in Kilimanjaro Region, the Honorable Anne Kilango Malecela (left), who was selected as the 2009 Tanzanian Woman of Courage by the U.S. Embassy in Dar es Salaam. The annual award was established to recognize women who have shown exceptional courage and leadership. Also in the photo is Anne Kilango Malecela’s husband former Premier John Samuel Malecela. (Photo courtesy of the American Embassy) Kusoma zaidi hapa

Thursday, March 26, 2009

Chadema Yatimua 15

Chadema ambacho jana kiliripotiwa Mwananchi jana kuandamwa na bundi, kimewavua uanachama watu 15 kwa makosa mbalimbali yakiwamo usaliti na kutoa siri za chama. Waliovuliwa ni Abdul Mateleta, Nasir Chimko, Hamisi Msasa, Abdallah Kaoneka, Mkwanji Maulid, Bimkubwa Uwesu na Peter Katunka, anayedaiwa kuwa mtumishi wa Mbunge wa Ubungo, Charles Keenja.

Wengine ni Zuberi Haji, Kimaro T, Bakari Shingo, Shaaban Salum, Adam Yasin, Said Mareja, Mwanahamisi Sadiki na Martin Mng’ongo, aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Kinondoni, ambaye inadaiwa alikuwa mpangaji na mshauri mkuu wa mpango wa uasi ndani ya chama na anayepeleka nyaraka zote.
Kamati Kuu pia ilitengua nafasi ya mjumbe wa Kamati Kuu ya Mecky Mzirai na kumpa onyo kutokana na kudaiwa kuvujisha siri za chama na kupanga mikakati ya kuleta vurugu ndani ya chama hicho. Hata hivyo rufaa yake ipo wazi kwa siku 14. Zaidi Soma Hapa

Dakika za majeruhu

Muda wa kipimajoto cha wiki hii unazidi kuyoyoma. Swali lenyewe linajionyesha hapo kulia kama kawa. Piga kura yako sasa, matokeo kesho.

Ni Bao la Dunia

Wapo waliowahi kuliona. Lakini ni wachache. Tumezoea kusikia mpira umepigwa kutoka mita 20, 25 au 30 n a kujaa wavuni. lakini hili la Juma Kaseja kutoka ndani ya eneo lake la mita 18 kupiga shuti reeefuuuuu hadi likajaa wavuni upande wa pili, inaelezwa hii iliwahi kutokea tu kwa Essam El-Hadary wa Al Ahly ya Misri, lakini yeye aliupiga kutoka umbali wa mita 70. Bao hilo liliipeleka Yanga kwenye ubingwa ikiwa na mechi kadhaa mkononi. Hapa gazeti hili limeandika kwa kirefu.

Ni mgao wa umeme kweli?

ETI Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kutakuwa na mgawo wa dharura wa umeme kwa jiji la Dar es Salaam kwa saa nane (8) zenye mahitqaji makubwa ya umeme kila siku, kutokana na kile walichosema ni kukosa huduma ya mitambo miwili ya kuzalisha umeme ya kampuni ya Songas. hali hii inajitokeza katikati ya mjadala wa ununuzi wa mitambo ya Dowans na huku ikiwapo kauli ya Tanesco "tukiingia gizani tusilaumiwe" Pata Habari Kamili. Na Tayari ratiba ya mgao huo ukiitaka Isome Hapa.

Wednesday, March 25, 2009

Aliyeturoga Kashakufa


Nchi maskini za Afrika ikiwamo Tanzania zinaibiwa mabilioni ya fedha kwenye madini kutokana na kutokutoza kodi za kufaa na kutolipwa mrabaha muafaka...Inauma sana. Iko Hapa kwenye Herald Tribune na The Citizen wameinyumbua vilivyo.

The Citizen 'Hard Copy' online


Now, READ your favorite newspaper, The Citizen, online exactly as it appers in print.

Songas Yaikana Dowans




KAMPUNI ya kuzalisha umeme wa gesi ya Songas Limited imesema haina mpango wa kununua mitambo iliyotumika ya kampuni ya Dowans Tanzania Limited (DTL), kwa haina uwezo wa kutumiwa kibiashara Cheki hapa. Habari hii ilianzia kwenye gazeti la The Guardian (Tanzania). Kilichokuwa kinashangaza zaidi ni kuwa miongoni mwa wanahisa watano wa Songas, yamo mashirika ya Umma matatu yafuatano:

1. Petroleum Development Corporation - TPDC (shirika la umma 100%)

2. Tanzania Electricity Supply Company Limited - TANESCO (shirika la umma 100%)
3. Tanzania Development Finance Company Limited - TDFL (shirika la umma 100%). Wanahisa wengine ni;

4. Nederlandse Financierings - Maatschappij Voor Ontwikkelingslanden NV - FMO; na

5. Globeleq (mwenye hisa nyingi)

Monday, March 23, 2009

Moto Moto Moto Bagayomo

Baadhi ya vijana hawa wa Bagamoyo waliamua kuokoa maji ya kunywa ambayo labda waliyamisi kwa kuwa hotelini hapo huuzwa bei mbaya.

Mkazi wa Bagamoyo akishangaa 'moto wa mabua' ulivyoteketeza hoteli za Paradise Holiday Resort na Oceanic Hotel leo. Ukitaka kuona picha zaidi peruzi ukurasa huu. Hii ndiyo ilikuwa habari kubwa kwa vyombo vya habari ndani na nje ya Tanzania. Mwananchi wameripoti hivi lakini Tanzania Daima likasema ni hoteli tatu, ikiwamo Livingstone

Wabaguzi wa vyama vya siasa

Swali la Wiki:

Hili linaweza kuwa la kibaguzi: Hivi kwanini Watanzania wenye asili ya Kiasia wanavibagua vyama vingine vya siasa, yaani huwezi kuwaona kwenye chama zaidi ya hiki kinachotawala--CCM?

Gari Nafuu Kuliko Yote

Tata Nano Monday, March 23, 2009 5:52 AM

Shirika la kutengeneza magari la Tata Motors la India linatarajia kuzindua gari lake jipya litakalouzwa kwa bei rahisi kuliko magari yote duniani likiwa na uwezo wa kubeba watu watano. Soma zaidi Nifahamishe

Sunday, March 22, 2009

Thabeet Hashim

Thabeet Hashim akiwa na Balozi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Dk Augustine Mahiga. Zamani nilidhani huyu balozi ni mrefu.
Hasheem amechaguliwa kuwa finalist wa Mens College Player of the Year awards.
Kwa wale walioko Marekani wanaweza kupiga kura kwa kutuma sms 51234 ukiwa na ujumbe VOTE.
Asilimia 25% za kura zitatokana na kura za washabiki.

Ili kumpigia kura bofya hapa
http://www.thehrr.com/HRR_blog/2009/
03/four-finalists-named-for-naismith-award.html

Umeliona Jumba Hili?

Welcome to NIFAHAMISHE.COM (inform me.com). This is one of many internet-based news publications for Tanzanians and friends living abroad.
The Publication was established in the United Kingdom, in late 2008, NIFAHAMISHE.COM is currently one of Tanzanian’s and friends abroad major news publishers and we are reputed internationally for our quality content. Funguo Zake Hizi Hapa

Changa la macho Dowans

Sasa eti mitambo yake kununuliwa na Songas

As the heated debate on whether the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) should or should not buy the Dowans Power Plant comes to a close, it has been hinted that Songas Power Company is now the potential buyer of the machines, The Guardian has learnt allayed fears over power rationing should the weather forecasts behave accordingly

Wanahisa wa Songas:

Globeleq

Tanzania Petroleum Development Corporation - TPDC (shirika la umma 100%)

Tanzania Electricity Supply Company Limited - TANESCO (shirika la umma 100%)
TDFL
Tanzania Development Finance Company Limited - TDFL (shirika la umma 100%)

Nederlandse Financierings - Maatschappij Voor Ontwikkelingslanden NV - FMO

Kwa hiyo: Dowans kununuliwa na umma

Saturday, March 21, 2009

Editorial Mwananchi

Mvutano huu ni ujanja wa
kutuondoa kwenye ajenda
MALUMBANO yanayoendelea baina ya wabunge wawili wa CCM, Rostam Aziz wa Igunda na Dk Harrison Mwakyembe wa Kyela yanawafanya Watanzania wahoji mantiki yake kwa sababu hayana masilahi kwa taifa na jamii kwa ujumla...Zama Mwenyewe Ndani

Moto posho za wabunge wasambaa

"Tunakula mapesa mengi yapunguzwe"
SIKU chache baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kutaka posho za wabunge nchini zipunguzwe, imebainika kumbe hoja hiyo imesambaa karibu nchi zote za Afrika Mashariki. Soma zaidi

Baraka ya Papa Benedict XVI

Jumapili njema wanawani

Friday, March 20, 2009

Rostam: Mwakyembe Mbaguzi

Malumbano kati yao yazua mjadala mpya

Kauli ya Rostam Aziz kuwa Dk Harrison Mwakyembe ameanza ubaguzi kwenye aliyoitoa Mwananchi imepokelwa kwa hisia tofauti, wengi waliojadili suala hilo kwenye Jamii Forum wanashangaa nani mbaguzi kati ya hao wawili...endelea na mjadala hapa. Hayo yote tisa, kumi ni kwamba malumbano yao yamemkera Spika wa Bunge, Samuel Sitta ambaye amesema HAPA kuwa atawaifa kwenye Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge. Sekeseke halikuishia hapo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Anne Kilango amesema kupitia Nipashe malumbano yao ni makovu ya kashfa ya Richmond.

Matokeo ya Kipimajoto

Kifungo cha mwaka mmoja
kwa aliyempiga Mwinyi

Kinastahili 5 (25%)
Ni kifupi 3 (15%)
Ni kirefu 2 (10%)
Hakustahili adhabu 10 (50%)

Total votes 20

Swali jipya: Nani aungwe mkono kati ya
Rostam Mwakyembe. Piga kura hapo kulia

Tanzania Haitambui Mapinduzi Madagascar

Rais Andry Rajoelina (pichani)azidi kupeta
PRESS RELEASE

STATEMENT OF THE GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA ON THE UNCONSTITUTIONAL CHANGE OF POWER IN THE REPUBLIC OF MADAGASCAR


The Government of the United Republic of Tanzania has received with profound consternation, news of the forced resignation of the democratically elected President Marc Ravalomanana of the Republic of Madagascar.
Forcing a democratically elected head of state to resign by a mutinous faction of the military, at the instigation of a section of the population, is a serious set-back for the cause of entrenching the spirit of democracy and good governance on the African continent, and for the Republic of Madagascar; it is tantamount to a military coup which is unacceptable. For Madagascar, this event negates the will of the people and denies them of their basic right, to elect the leaders of their choice democratically. It is also a reminder of Madagascar’s dark past of military coups that took place in 1975 and 1991.
Furthermore, the Government of the United Republic of Tanzania considers the forced resignation as being an unconstitutional change of power in the Republic of Madagascar, and is strongly opposed to it as it goes against the letter and spirit of the Constitutive Act of the African Union, the Protocol Establishing the Peace and Security Council of the African Union and the Lome Declaration of July 2000, all of which prohibit unconstitutional changes of Governments on the African continent.
For these reasons the Government of the United Republic of Tanzania does not recognize the illegal regime of Mr. Andry Rajoelina.
The Government of the United Republic of Tanzania joins the African Union and SADC, in urging an expeditious return to Constitutional rule and in demanding the de facto authorities comply scrupulously with the provisions of the Constitution of Madagascar relating to interim arrangements in the event of resignation.
To this end the Government of the United Republic of Tanzania calls on the parties concerned to uphold the spirit of dialogue and compromise, with a view to finding a peaceful constitutional solution to the crisis and restoring democracy in Madagascar.
The Government of the United Republic of Tanzania calls on the Madagascar military to take all necessary measures to ensure the safety of the President and his family, his associates, respect for individual and collective freedoms and prevent any act of violence or intimidation and protect property.


ISSUED BY: MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM
20 MARCH, 2009

Scholarships

I'm MAKULILO Jr, FULBRIGHT Visiting Scholar and Professor at Marshall University in West Virginia, USA. I teach GLOBAL CONNECTIONS: DISCOVER
AFRICA. T0 write/contact me, Click
CONTACT ME or call +1 304 633 0978

Thursday, March 19, 2009

Maisha Plus Mhh!







Maisha plus mambo yanazidi kuinoga keshokutwa wengine wawili wanatoka kijijini. Wawili hao kwenye picha tayari wako nje wanapunga upepo Picha za Washiriki

Watoto wa Pinda


Niliweza kupata picha hii ya watoto wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakiwa na watoto wezao wa makabwela enzi hizo .Kuanzia kwa mtoto mwenye suti kulia waliosimama nyuma, watatu aliyesimama ni Namsi Pinda (mwenye gauni jeupe na anayecheka aliyebana nywele) na mwingine aliyesimama nyuma ya mtoto mwenye nguo nyekundu anayecheka mbele, ana nguo nyeupe anaitwa Mkalo Pinda (amebana nywele).

(Picha hii imepigwa na Rev-John Mlemeta Nov-1987 Mbagala Saba-saba , Dar es salaam)

Yaliyojiri kwa Mwakyembe

Dk. Mwakyembe alionyesha kukerwa na baadhi ya wanahabari wanaotumiwa kuwachafua watu kwa maslahi ya wachache na si ya taifa na taaluma nzima ya habari.

Waandishi wa habari lazima mzingatie maadili ya taaluma yenu na msikubali kutumiwa na baadhi ya watu kuwachafua wengine kwa sababu kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya taaluma, ambayo kwa sasa imeingiliwa na ni jukumu lenu kuilinda,” alisema.

Alisema kuna wanasiasa waliochafuka kutokana na matendo yao machafu kwa jamii na kwamba, wanatumia wanahabari wasio waadilifu kuwasafisha na kuwafichia maovu, lakini kuna wengine hawawezi kusafishika.

Kutokana na kauli hiyo ya Dk. Mwakyembe, aliyeonyesha magazeti yaliomchafua, baadhi ya wanahabari waliingia kwenye mgawanyiko, jambo lililomfanya mwanasiasa huyo, ambaye kitaaluma ni mwanasheria kukatisha kujibu maswali na kuwasuluhisha.

Mmoja wa waandishi, alihamaki na kubishana huku akitetea habari iliyoandikwa katika gazeti lake, iliyoshutumiwa na Dk. Mwakyembe.

Kutokana na kutetea huko, mwandishi wa habari mwingine, ambaye gazeti lake halikushutumiwa, alimtaka kunyamaza kwa sababu yeye naye ni mwandishi kama walivyo wengine.

Mwandishi huyo aliyekuwa akilitetea gazeti lake, alijibu kwamba, hata kama yeye ni mwandishi wa habari kama walivyo wengine, lakini huyo asijifananishe na yeye.

Hivi karibuni kumezuka mjadala mkubwa kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuonyesha nia ya kutaka kununua mitambo ya Dowans, jambo lililopingwa na baadhi ya wabunge wakisema ni kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma. TANESCO baadaye ilitangaza kuachana na mpango huo. Chanzo:
Gazeti la Uhuru. Note: Gazeti halikutaja majina, bado yanatafutwa.

Safari ya Mallya


Hii ndiyo safari ya Mally kwenda Gereza la Isanga mkoani Dodoma, linaloaminika kuwa na ulinzi mkali zaidi nchini.

Wednesday, March 18, 2009

Deus Malya alamba mvua 3

Wakili wake amwaga machozi

Deus Malya, aliyedaiwa kuendesha lililomuua Chacha Wangwe aliyekuwa mbunge wa Tarime, amepatikana na makosa mawili, kuendesha gari kwa kasi na kusababisha ajali; na kuendesha gari bila leseni.
Kwa kosa la kwanza amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na mwaka mmoja kwa kosa la pili. Kwa kuwa vifungo hivyo vinakwenda pamoja, Malya atakaa jela kwa miaka mitatu. Hukumu imetolewa leo katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma. (pichani akiwa kizimbani na kulia ni mawakili )

Breaking News


Mwakyembe kaanza kwa kusema "Siwezi kuumbuliwa na kampuni ya mtu asiye na maadili kama Rostam".
Anasema: "Sina mkataba na Bunge. Nina profession yangu na natamani mambo mengi kama mtanzania."
Anasema kuna projects nyingi ambazo ameziona zimeandaliwa ili ziwe read story za kumchafua Mwakyembe.Anasema kuna magazeti yanayoandika "Sasa Umoja wa Mataifa unamuunga mkono dhidi ya Mwakyembe". Anasema Profession ya uandishi wa habari imeingiliwa! Anasema kuna watanzania wangapi ambao wanaweza ku-declare interest kwenye mambo kadhaa ati kwakuwa wamesajili kampuni tu?
Akatoa mfano: Kuna waandishi wangapi wamesajili magazeti na hawajaacha kazi kwakuwa wameanzisha magazeti?
Akauliza tena: Ingewezekana vipi afanye ku-declare interest kwa kusajili kampuni tu ati akiwa na memorandum of articles? Anasema labda itawezekana lakini si rahisi kwa sababu unakuwa huna kazi in hand .
Anasema:Dhamira ya kampuni yake ni kuzalisha umeme wa Megawati 1800 na hakuna kampuni hata moja kwa Tanzania itaweza.Na anasisitiza ziangaliwe annual returns za kampuni hiyo za mwaka 2007/08 tutagundua kuwa shares zilishakuwa transfered siku nyingi.

Ameulizwa kuwa ametoa tuhuma kadhaa kwa RA na wote wawili ni wajumbe wa NEC... Haoni kama baadae itakuwa tatizo?
Kajibu: Hilo swali angeulizwa Rostam, kwakuwa yeye ndo anayefanya kuchafua wenzake na anajua siku si nyingi mambo yake (RA) yatalipuka tu.
Chanzo

Dk Mwakyembe Kumwaga Mboga


VYANZO vya karibu vya Dk Harrison Mwakyembe vimesema leo atatoa maelezo yake na vinasema kuwa leo"mstari uliokuwa hauvukwi, utavukwa". Mmoja wa watu wa karibu na Mwakyembe alisema jana, "Dokta atawatolea uvivu kesho". Alipobanwa kuelezea ni kwa jinsi gani uvivu huo utatolewa jamaa huyo alikataa na kusema "subirini kesho". Hadi tunakwenda mitamboni jioni hii haijawekwa sawa mkutano huo utafanyika wapi lakini muda uliopangwa hadi hivi sasa ni saa nne za asubuhi. Chanzo

Mwosha Uoshwa


Aliingia Ikulu kwa njia hii hii. Wananchi wanaandamana bila kikomo hadi Rais anatekuwa madarakani anasalimu amri...Nguvu ya Umma. Nini kimetokea sasa... endelea...Rais wa Madagascar Mark Ravalomanana (kulia) amelazimika kujiuzulu na kukabidhi nchi kwa jeshi la nchi hiyo baada ya sekeseke lililodumu ndani ya taifa hilo kwa muda sasa na baada ya kiongozi...na aliyekuwa kiongozi wa upinzani, Andry Rajoelina (34) (kushoto) kaingia Ikulu. Kusoma zaidi

Tuesday, March 17, 2009

Papa Ampinga Mwinyi!

Pope Benedict XVI said on his way to Africa Tuesday that condoms were not the answer in the continent's fight against HIV, his first explicit statement on an issue that has divided even clergy working with AIDS patients.
Benedict had never directly addressed condom use. He has said that the Roman Catholic Church is in the forefront of the battle against AIDS. The Vatican encourages sexual abstinence to fight the spread of the disease. (Mwinyi yeye alisema kondom ndio njia ya kuwasaidia wale 'wasiokubali mafundisho ya dini yanayozuia uzinzi) Soma zaidi alichosema Papa hapa

Kisa cha Anna Tibaijuka

Monday, March 16, 2009

Kesi juu ya Kesi










Machi 16, 2009

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa niaba ya kamati inayoundwa na waandishi, wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari ambao jumla yao ni 13 , ninapenda kuwafahamisha kuwa kesho Machi 17, mwaka huu saa 4.00 asubuhi tunatarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari katika Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.


Dhumuni la kufanya mkutano huo ni kuelezea kusudio lao la kumfungulia mashtaka mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi pamoja na magazeti yake yakiwemo Kulikoni na Nipashe kwa kuwakashifu.

Kashfa hizo ni pamoja na kuwaita waandishi, wamiliki na wahariri hao kuwa ni mafisadi na magazeti yao aliyoyaita kuwa ni vipeperushi, yameanzishwa, kumilikiwa na kufadhiliwa na mafisadi nchini.

Aidha, katika kikao hicho na wanahabari, wajumbe wa kamati wananakusudia kueleza umma ili uelewe kuwa hawana ugomvi binafsi na mwenyekiti huyo bali wanatimiza wajibu kama vyombo vya habari katika kuelimisha, kupasha habari na kuburudisha na si vinginevyo, hii ni pamoja na kuzingatia maadili.

Tunatarajia ushirikiano katika hilo.

……………………
Prince Bagenda
Mwenyekiti wa kamati

Mechi ya Yanga kwa Video

Yanga 0 Al Ahly 3

Sunday, March 15, 2009

Msiba CUF

The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi) kinasikitika kuwaarifuni kwamba, leo asubuhi mwasisi wa chama hiki, Mhe. Shaaban Khamis Mloo, amefariki dunia, nyumbani kwake, mjini Zanzibar.
Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika leo leo saa 10.00 alasiri huko huko Zanzibar.Marehemu Mzee Mloo alikuwa katibu mkuu wa kwanza wa CUF kwa miaka nane, kutoka 1992 hadi 2000 alipochukua nafasi ya umakamo mwenyekiti hadi alistaafu mwaka 2004. Yeye ndiye miongoni mwa waasisi wa Chama hiki, kwa kuanzia na vuguvugu la KAMAHURU.
Ni yeye ndiye aliyeongoza mazungumzo ya kwanza na aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CCW), Mhe. James Mapalala, na hatimaye kuungana na kuzaliwa kwa CUF tuliyonayo sasa.

Kibao cha Mwinyi: Serikali Yazinduka

Sofia Simba (pichani), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) anayesimamia mashushushu anasema, "Tukio hili limetufedhehesha sana, pia ni aibu kwa taifa, ni lazima tujipange upya.
"Kutokana na tukio hilo tumeamua kuongeza ulinzi katika ziara zote za viongozi wakuu wa kitaifa na kimataifa hapa nchini hasa katika nyumba za ibada." Kujisomea zaidi hapa

Friday, March 13, 2009

Alompiga Mwinyi Jela

Breaking News

Kijana aliyempiga kibao Mzee Mwinyi, Ibrahim said Sultan amehukumiwa kifungo mwaka mmoja jela.

Ushauri kwa Zitto Kabwe

Dear Hon. Zito, I clearly see the point in the arguments you have put forward to support the idea of buying Dowans turbines. I am fully convinced that you are absolutely right. But I just want to remind you one thing.

To make an economic decision we need to carryout analysis. Based on the level of subjectivity we have two main types of analyses; positive and normative analysis. The difference between the two is that positive analysis is based on empirical reasoning while normative analysis introduces subjectivity in the reasoning. In other words, positive economics deals with “what is” whereas normative economics addresses the issue of “what ought to be”. Both are important.

I will give you an example to make myself clear. Suppose you secure a consultancy work from the Revolutionary Government of Zanzibar to investigate and recommend the way to curb the problem of protein deficiency in Zanzibar. As an economist, you carry out cost-benefit analysis for different type of protein sources, and realise that the protein that can be made available at affordable cost for the majority of Zanzibaris is pork. Up to this point what you have carried out is positive economic analysis. Now the issue is whether you could go ahead and recommend this to the government for implementation! Having taken into consideration of values and norms of the Zanzibar society you may be forced to opt for the second best alternative source of protein. When you do that you have carried out normative analysis.

The same applies to the Dowans saga. Mh. Zito, you have done your homework well on the positive analysis side. It is now time to take on board normative aspects in the analysis, i.e. the dubious environment surrounding the Richmond/Dowans drama and the negative feelings people have on it.

On this background Mh. I advise you to forfeit the idea of buying these turbines and opt for the next best alternative.

Regards,


Dr. Damian M. Gabagambi
LecturerSokoine University of Agriculture Department of Agricultural Economics and agribusiness P.O.Box 3007 Morogoro - Tanzania

Tel: (+255 232) 603415 (Office)
Mob: (+255 744) 501541
Fax: (+255 232) 600968 (Office)

Thursday, March 12, 2009

Misamaki ya Magufuli


Hizi ni sehemu ya samaki (zaidi ya tani 70) zilizokamatwa kwenye meli jini la samaki...wadau wanasema badala ya kupelekwa mahakamani kama kilelezo zingemwagwa feri wananchi wakajipatia vitamini

Aliyemchapa Mwinyi Akiri Kosa


Yule kijana aliyemzaba kofi Mzee Mwinyi, Ibrahim Said Sultan amekiri kosa mahakamani leo, kesi yake imeahirishwa hadi kesho atakaposomewa tena maelezo ya mashtaka, kabla ya kusomewa hukumu yake.



Wednesday, March 11, 2009

Du! Massage ya nyoka!




Hii kali. Nimeikuta kwa Chemi che-Mponda, imesisimua mwili wangu sana, eti massage kwa kutumia majoka! Thubutu!

Wazo Bonzo

Tujiulize,

Kwa kuwa, Mwinyi alimwakilisha JK kwenye Baraza la Maulid, na

Kwa kwa, aliyosema pale ni yale aliyotumwa na mgeni rasmi, JK na

Kwa kuwa, watu waliohudhuria walidhani wangemkuta JK, kwa hiyo basi,

Itakuwa ni kosa kusema kuwa ALIYEZABWA KIBAO NI JK?

Kichapo Alomzaba Kibao Mwinyi



Ibrahim Hassan, kijana aliyemzaba Mzee Myinyi kibao akipokea 'haki yake' kutoka kwa wanausalama waliomkamata baada ya tukio hilo. Habari za ndani kutoka katika vyombo vya usalama zinasema kuwa anaendelea kuhojwa huku kukiwa na tetesi kuwa, alisema 'ametumwa' kufanya kitendo hicho. HABARI NDIYO HII...Hii ndiyo habari ya siku, mijadala kwenye tovuti na blog mbalimbali inazungumzia suala hili, Cheki hapa BONGO CELEBRITY wadau wanavyosema. (Picha na Sumo)

Tuesday, March 10, 2009

Maskini Mzee Mwinyi

Ilikuwaje?






Tukio hilo ambalo halikutarajiwa lilitokea jana majira ya saa 12:20 hivi wakati rais huyo mstaafu alipokuwa akihutubia Baraza la Maulid kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) lililohudhuriwa na Waislam wengi katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Alhaji Mwinyi alikuwa akizungumzia masuala ya afya na namna ya kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi ndipo alipojitokeza mmoja wa waumini aliyekuwa amevalia shati na suruali na kupanda jukwaani kisha kujifanya kama vile anamsalimia Mufti Sheikh Mkuu Issa bin Simba.
Kwa kuwa imezoeleka shughuli za kidini kama ile huwa ni za amani basi waliokuwa karibu na mtu huyo wala hawakuwa na shaka naye ndipo mtu huyo akarudisha kibao kwa nguvu na kumzaba Mzee Mwinyi.
Mtu huyo alijifanya kama anataka kumsalimia Kaimu Mufti, Sheikh Suleyman Gorogosi.Kwa kuwa imezoeleka katika shughuli za kidini kutawaliwa na amani, watu waliokuwa karibu na mtu huyo hawakuwa na shaka naye ndipo mtu huyo akarudisha mkono ghafla na kumzaba kibao Mzee Mwinyi.
"Sisi tulishangaa kuona yule jamaa akipanda jukwaani na kujifanya kama anasalimiana na Mufti. Lakini cha kushangaza tukaona akageuka na kumzaba kibao Mzee Mwinyi... sisi tulishikwa butwaa," alisema Hussein Kauli mmoja ya watu waliohudhuria sherehe hizo

Mwinyi Achapwa Kibao

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi leo pale Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam amelambwa kofi na muumini kwa kile kinachoelezwa kama kutetea matumizi ya KONDOMU kwa waumini. Alikuwa akizungumza katika baraza la Maulid lililofanyika jioni hii. Aliyemlamba kibao ameshughulikiwa ipasavyo na wanausalama.

Limeli jizi la samaki


Juhudi za Waziri vitoweo (uvuvi na mifugo) John Pombe Magufuli zimefanikisha kukamatwa kwa meli kubwa ya uvuvi iliyokuwa na tani 70 za samaki katika eneo la Tanzania, kwenye Bahari ya Hindi. Inaelezwa kuwa faini ya kosa hilo ni ama kulipa Tsh 20 bilioni, au meli kutaifishwa au yote mawili kwa pamoja. HABARI KAMILI