Sunday, March 15, 2009

Msiba CUF

The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi) kinasikitika kuwaarifuni kwamba, leo asubuhi mwasisi wa chama hiki, Mhe. Shaaban Khamis Mloo, amefariki dunia, nyumbani kwake, mjini Zanzibar.
Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika leo leo saa 10.00 alasiri huko huko Zanzibar.Marehemu Mzee Mloo alikuwa katibu mkuu wa kwanza wa CUF kwa miaka nane, kutoka 1992 hadi 2000 alipochukua nafasi ya umakamo mwenyekiti hadi alistaafu mwaka 2004. Yeye ndiye miongoni mwa waasisi wa Chama hiki, kwa kuanzia na vuguvugu la KAMAHURU.
Ni yeye ndiye aliyeongoza mazungumzo ya kwanza na aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CCW), Mhe. James Mapalala, na hatimaye kuungana na kuzaliwa kwa CUF tuliyonayo sasa.

No comments:

Post a Comment