Tuesday, March 10, 2009

Maskini Mzee Mwinyi

Ilikuwaje?


Tukio hilo ambalo halikutarajiwa lilitokea jana majira ya saa 12:20 hivi wakati rais huyo mstaafu alipokuwa akihutubia Baraza la Maulid kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) lililohudhuriwa na Waislam wengi katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Alhaji Mwinyi alikuwa akizungumzia masuala ya afya na namna ya kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi ndipo alipojitokeza mmoja wa waumini aliyekuwa amevalia shati na suruali na kupanda jukwaani kisha kujifanya kama vile anamsalimia Mufti Sheikh Mkuu Issa bin Simba.
Kwa kuwa imezoeleka shughuli za kidini kama ile huwa ni za amani basi waliokuwa karibu na mtu huyo wala hawakuwa na shaka naye ndipo mtu huyo akarudisha kibao kwa nguvu na kumzaba Mzee Mwinyi.
Mtu huyo alijifanya kama anataka kumsalimia Kaimu Mufti, Sheikh Suleyman Gorogosi.Kwa kuwa imezoeleka katika shughuli za kidini kutawaliwa na amani, watu waliokuwa karibu na mtu huyo hawakuwa na shaka naye ndipo mtu huyo akarudisha mkono ghafla na kumzaba kibao Mzee Mwinyi.
"Sisi tulishangaa kuona yule jamaa akipanda jukwaani na kujifanya kama anasalimiana na Mufti. Lakini cha kushangaza tukaona akageuka na kumzaba kibao Mzee Mwinyi... sisi tulishikwa butwaa," alisema Hussein Kauli mmoja ya watu waliohudhuria sherehe hizo

1 comment:

Anonymous said...

...Kwa mujibu wa uislam uzinzi umekatazwa (ni haram) iwe umevaa kondom au hujavaa! Mzee Mwinyi anatumia jukwaa la dini ya kislaam kufundisha watu wazini kwa kutumia kondom, hii ni haramu na amekosea, achilia mbali wanaozini wafe kwa ukimwi, uislam haufuati upepo kwamba sababu mnataka kuzini na mnakufa kwa ukimwi basi uislam uruhusu kuzini kwa kondom. Baya zaidi unaambrisha uovu huo siku ya kuzaliwa yule aliekuja kuukataza uovu huo (Mtume S.A.W). Kwa hiyo Mzee mwinyi alifanya uovu, na kwa mujibu wa Mtume, anasema "ukiona uovu uwondoe kwa mikono yako, au ukemee kwa mdomo au chukia moyoni mwako, ingawa huko kuchukia tu ni imani dhaifu..." Kwa hiyo huyu kijana alomchapa Mzee Mwinyi kibao, machoni mwa wanaadamu ataonekana mtovu wa adabu, muhuni na kila aina ya sifa mbaya, Ila mbele za Allah na waumini wenye kujuwa dini yao, yeye ni shujaa, ni mtu bora na kweli anatafuta radhi za Allah na sio sifa na utukufu wa dunia, kama wengine wanaoacha uislam wao kwa maslahi ya kidunia...!

Post a Comment