Mwananchi Queen
Hiki ndio Kikosi Kamili cha makwini wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, inayochapisha magazeti ya Mwananchi, mwanaspoti, Mwananchi Jumapili, The Citizen na Sunday Citizen. Kikosi hiki kikiongozwa na mama lao, Maimuna Kubegeya (Mbele Kushoto) kimefanikiwa kwa mbinde kuingia fainali ya Mashindano ya NSSF
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 6:52:00 PM

|
Permalink |
Makaburi mengine balaa
Kaburi kwa sura ya gari. Hii ni zawadi ya Marehemu Joely Kivelege aliyezikwa Kinondoni Dar es Sa Salaam, aliyopewa na Mzungu mmoja aliyekuwa mlezi wa kituo cha watoto yatima. Kivelege alikuwa miongoni mwa watoto hao. Mzungu huyo alimpenda sana kutokana na tabia yake njema. Alipotaka kwenda Ulaya likizo, alimuahidi kijana huyo zawadi ya gari, lakini aliporudi, alikuta mambo yameharibika. Kivelege alikuwa amefariki kwa malaria iliyopanda kichwani. Ahadi ni deni, mzungu huyo aliamua kumjengea kaburi mfano wa gari na hiyo ikawa ndiyo zawadi yake.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 2:03:00 PM

|
Permalink |
Kila mtu na 'Ushujaa' Wake
Waziri Mkuu, Mizengi Kayanza Peter Pinda akikabidhiwa upinde na mishale ili akapambane.
Waziri Mkuu aliyestaafishwa, Edward Ngoyai Lowassa akionyesha ngao yake ya kujikinga dhidi ya mishale
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 1:38:00 PM

|
Permalink |
Mafisadi Wazidi Kubanwa
Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya Mbeya, Tanzania wakionyesha bango lenye katuni inayomuonyesha kiongozi mmoja, wakimuuliza; fedha zote hizi unazipeleka wapi? Bila nao wamekerwa na wizi wa mapesa ya umma.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 12:13:00 PM

|
Permalink |
Cheka Awacheka Kina Matumla
Taarifa kutoka katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Bondia Froncis Cheka wa Morogoro amemchakazi vibaya Hassan Matumla kwa KO na kutwaa ubungwa wa mabara uzito wa kati. Alimuangusha katika round ya 10 kati ya 12 zilizotakiwa. Kwa hiyo Cheka ameendelea kucheka katika familia ya wanamasumbwi ya kina matumla, baada ya kuwachapa hata kakaze Hassan.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 12:03:00 PM

|
Permalink |
Ndondi Ndondi

Hassan Matumla (kulia) na Hassan Cheka wakitunishiana misuli wakati wa kutangaza mtanange wao wa kesho ili kuwania mkanda huu.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 7:25:00 PM

|
Permalink |
Waliyokubaliana, Kibaki na Raila
Key points: Kenya power-sharing deal
- The post of prime minister will be created, with the holder having the authority to co-ordinate and supervise the execution of government functions.
- The prime minister will be an elected member of parliament and the parliamentary leader of the largest party in the National Assembly, or of a coalition if the largest party does not command a majority in parliament.
- Two deputy prime ministers to be appointed, one to be nominated by each member of the coalition.
- The prime minister and deputy prime ministers can only be removed if the National Assembly passes a motion of no-confidence with a majority vote.
- A cabinet to consist of a president, vice-president, prime minister, two deputy prime ministers and other ministers.
The removal of a minister of the coalition will be subject to consultation and agreement in writing by the leaders.
- The composition of the coalition government will at all times take into account the principle of portfolio balance, and reflect the parties' relative parliamentary strengths.
- The coalition will be dissolved if the current parliament is dissolved; or if the parties agree in writing; or if one coalition partner withdraws from the coalition.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 2:08:00 PM

|
Permalink |
Chemical Ali naye Kunyongwa
Bila shaka, kwa waliofuatilia vita ya Iraq, mnamkumbuka mjombawe Saddam Hussein, Chemical Ali...Naye amehukumiwa kunyongwa hadi kufa. Taarifa yenyewe iko hivi.
BAGHDAD - Iraq's presidency endorsed the execution of Saddam Hussein's cousin known as "Chemical Ali," who was sentenced to death for his role in the 1980s scorched-earth campaign against Kurds, a government adviser said Friday.
The backing by Iraq's President Jalal Talabani and two vice presidents is the final step for the approval of Ali Hassan al-Majid's death sentence, which must be carried out within 30 days of the decision.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 12:29:00 PM

|
Permalink |
Kenya Waafikiana. Amani Kurejea?

Wazee wa kazi wakubaliana kugawana madaraka
Hapa Watiliana saini, tuone nani atakuwa wa kwanza kukiuka makubaliano
Hata 'wazee' wetu walioshindwa miafaka kibao ya Zanzibar, walikuwepo, labda wamepata somo
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 11:33:00 AM

|
Permalink |
Juhudi za Mbowe Hola!

Pamoja na Ushawisho wooote wa Mwenyekiti wa Chadema kumnadi mgombe wake, Victor Kimesera bado kapoteza.

Unamuona mfanyabiashara Kimesera anavyofurahia, akidhania ataibuka mbunge baada ya kushindwa mara tatu jimboni humo. Kumbe sasakapoteza mara ya nne.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 10:15:00 AM

|
Permalink |
Wapinzani Wavyopoteza Kiteto
WanaCCM wakishangilai ushindio wa Benedict ole Nangaro kuwa Mbunge wa Kiteto
Mwanzoni Chadema walishani mgombea wao, Victor Kimesera ndio ameshinda baada ya kuona matokeo ya mjini Kibaya, lakini kumbe, mambo yakawa kama Kenya...Kibaki (Nangaro) kaitangazwa mshindi Odinga (Kimesera) Mhh!.
FFU walikuwa kibao. Taarifa zilisema walikuwa zaidi ya 500. wote wilaya moja, kufanya kazi gani? au walikuwa wanapiga kura?
Kapteni John Komba wa TOT na Mbunge wa Mbinga Magharibi akishuka kkwenye chopa ambayo ilitumika kama silaha ya msaada baada ya Bendi yake kushindwa kufua dafu kuwashawishi watu wa Kiteto
Wapiga kura wakiangalia majina yao kwenye daftari (karatasi) za kudumu za wapiga kura. Inasemekana zaidi ya nusu ya wapiga kura hawakuona majina yao. Wengine yalikuwa kwenye vituo vya mbali na walipotarajia...Baadhi sijui wa chama gani walihamishwa kwa magari kwenda kupiga kura mbali majina yao yalipopelekwa.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 10:02:00 AM

|
Permalink |
Vita ya Chopa
CCM YATANGAZWA MSHINDI KITETO
CCM kwa muda mrefu ilikuwa inasema matumizi ya helkopta ni matumizi mabaya ya fedha kwa Chadema. Ilipoona inakabwa koo, nayo ikakodi chopa hii, sababu ya matumizi ikaisha, wakasingizia hali ya hewa. Siku chopa yao ilipoanza kazi, ya Chadema 'ikafia' Dodoma. Hapo huenda ndipo mambo yakaharibika.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 9:56:00 AM

|
Permalink |
Muungwana husikiliza
Baadhi waliniandikia hapa, wengine wakaandika kwa email baada ya kushindwa kutoa maoni katika kisanduku cha maoni. Wengine walinipigia simu na wachache wakanieleza kwa mdomo. Nimeona sina sababu ya kuwa mkaidi...Nimerudi.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 9:43:00 AM

|
Permalink |
KWAHERINI
Ndugu wasomaji wa Blog hii
Kwaherini. Ninawaaga nimeamua kuachana na blog. Asanteni kwa kuniunga mkono tangu Novemba 2006.
Ndimi Miruko
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 5:41:00 PM

|
Permalink |
Joji Bush kwenye Benchi la Wagonjwa
Mzee wa Vituko: Bush kwenye benchi la wagonjwa Arusha
Mzee unamshika kila mtu, angalia usirudi US na 'Nairobi Red Eyes'
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 4:44:00 PM

|
Permalink |
JK akinga bakuri; Bush amwaga vyandarua
Jana mjini Arusha Rais Kikwete alielelzea tatizo la malaria nchini kwa Bush, naye hakuwa na ajizi...Endelea.
PRESIDENT KIKWETE: Mr. President, today there are thousands of women and children who would have died from malaria that are alive in Tanzania and all over the country, thanks to your malaria support program. I can give the example of Zanzibar. In 2004, in the outpatient clinic, 500,000 malaria patients were treated; in 2007, only 10,000. (Applause) In 2004 in Zanzibar, 40 percent of the patients tested positive for malaria; in 2007, only 5 percent. (Applause.) When the blood slide is taken, 35 percent tested positive for malaria in 2004; in 2007, only 1 percent. (Applause.).
PRESIDENT BUSH: Today, I'm pleased to announce new steps in the bed net campaign. Within the next six months, the United States and Tanzania, in partnership with the World Bank and the Global Fund, will begin distributing 5.2 million free bed nets. This ambitious nationwide program will provide enough nets to protect every child between the ages of one and five in Tanzania
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 3:50:00 PM

|
Permalink |
Bush Alipotembelea A-Town
Joji Kichaka akutana na akinamama wa Kimasai, KIA, huku mkewe, Laura akiwatazama kwa mshangao
Baada aya Kilio cha Malaria kutoka kwa JK, Bush aalitoa vyandarua milioni 5 kuwasaidia wabongo wasife kwa mbu. Baba ana huruma huyu!
Mama akazawadiwa chandarua na mzee Bush kufaidi joto lake. Walau si haba.
Labels: Bush in Arusha
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 3:35:00 PM

|
Permalink |
Bush

George Bush akicheki Ngoma Ikulu ya JK

Bush akiwapa mkono wachezaji wa ngoma
Shein akiwa ameketi na Mke wa Bush, Laura wakati wa chakula cha usiku
Kikwete na Makamu wake, Dk Shein, wakigonganisha glasi na wageni wao Ikulu
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 1:27:00 PM

|
Permalink |
Bush in Africa
Kiatu cha Bush
Kicheko cha Bush
Kumbe anapenda mademu
Makachero wa Bush wanoko kama wako kwao!
Hawana imani na Ikulu ya JK, Yaani hadi kwenye paa
Labels: Bush in Africa
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 4:38:00 PM

|
Permalink |
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 10:31:00 PM

|
Permalink |
Mtoto adondoka kutoka kwenye 'ndege', apona
Mtoto huyu (katikati) akiwa katika Ofisi za Mwananchi, akisimulia kisa chake. Kushoto ni mwandishi wa Mwananchi na Kulia na Padri wa Parokia ya Kristo Mfalme, Tabata aliyemsindikiza. KISA KAMILI:
Na Peter Edson
MTOTO mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa kijiji cha Kilima Hewa mkoani Mtwara amekutwa akiwa uchi kwenye eneo la Kanisa la Kristo Mfalme, Tabata jijini Dar es salaam baada ya kuanguka kutoka kwenye ungo waliokuwa wakisafiria kishirikina.
Akiongea na Mwananchi Jumapili, mtoto huyo alisema yeye na bibi yake, Binti Abdala Mkumba walikuwa wakisafiri kutoka Mtwara kwa usafiri wa ungo wakielekea mjini Morogoro kwenye mkutano wa wachawi wapatao 50 wenye lengo la kumpokea mwenzao aliyejiunga katika kundi lao hivi karibuni ili kumjengea nguvu na uwezo wa kupambana na nguvu nyingine zaidi soma www.mwananchi.co.tz
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 7:07:00 PM

|
Permalink |

Ukitaka kwenda Makete hivi sasa inahitaji moyo

Angepelekwa Bush ili aone, au?

Basi hili linaweza kumaliza hata wiki mbili bila kuvuka hapa...Tanzania yetu na mafisadi mh!
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 6:00:00 PM

|
Permalink |
Kichaka Aingia Afrika

Bush akiwa na Rais wa Benin, Thomas Boni Yayi

Hapa Joji Kichaka akimbusu mkewe, Laura, baada aya kutunikiwa medali ya heshima ya Benin

Akiwa na Rais kwenye zuria jekundu. Hivi nani alipanga mazuria hayo kuwa mekundu duniani pote? Nyuna inaonekana Air Force One

Akikagua jeshi la Benin
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 4:27:00 PM

|
Permalink |
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 3:05:00 PM

|
Permalink |
Diallo Akisoma Gazeti Bungeni
Aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Antony Diallo (kulia), akijipatia habari katika gazeti la Mwanahalisi, lililokuwa na headline: Richmond ya Rostam -Ikulu. Anayesikiliza mjadala wa bunge ni Mbunge wa Pangani, Mohamed Rished
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 12:44:00 PM

|
Permalink |
Wazushi Wameshaanza Mambo Yao

Labels: Wazushi
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 5:42:00 PM

|
Permalink |
Kazi kwao Celtel
Kazi kubwa iko kwa wateja wa Celtel kuongea kwa wingi kushindani haya ma-RAV4 na LandCruiser moja.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 5:03:00 PM

|
Permalink |
Mawaziri Waapishwa Dodoma
Kilichovutia wakati wa hafla ya akuapishwa kwa mawaziri ni watu wengi katika viwanja vya Ikulu ndogo , Chamwino Dodoma, kuimba Tyson, Tyson, Tyson, mara baada ya kuapishwa Stephen Wasira, Waziri pekee muda mrefu ambaye alikuwa serikalini tangu Awamu ya Kwanza. Sasa amekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Aliwahi kuhamia upinzani, NCCR-Mageuzi na kuwa mbunge.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 2:08:00 PM

|
Permalink |
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 9:24:00 AM

|
Permalink |
Mawaziri 17 Wapoteza
* Wamo mawaziri kamili 9, manaibu 7
* Baadhi yao waliomba kupumzika
Mawaziri waliokumbwa na 'panga' hilo
1. Zakhia Meghji (Fedha)
2. Anthony Diallo (Maendeleo ya Mifugo)
3. Basili Mramba (Viwanda, Biashara na Masoko).
4. Joseph Mungai (Mambo ya Ndani)
5. Dk Juma Ngasongwa (Mipango, Uchumi na Uwezeshaji)
6. Kingunge Ngombale-Mwiru (Ofisi ya Rais-Siasa na Uhusiano na Jamii)
7. Dk Ibrahim Msabaha (Ushirikiano wa Afrika Mashariki)
8. Nazir Karamagi (Nishati na Madini).
9. Juma Mwapachu (Usalama wa Raia)
Manaibu mawaziri waliochwa ni
1. Abdissalaam Issa Khatib (Fedha)
2. Ludovick Mwananzila (Elimu na Mafunzo ya Ufundi).
3. Daniel Nsanzugwanko (Habari, Utamaduni na Michezo)
4. Dk Charles Mlingwa (Maendeleo ya Mifugo) na Gaudence Kayombo (Mipango, Uchumi na Uwezeshaji).
5. Ritha Mlaki (Aridhi na Maendeleo ya makazi)
6. Gaudence Kayombo (Mipango, Uchumi na Uwezeshaji)
7. Dk Luka Siyame (Ofisi ya Waziri Mkuu-Maafa)
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 7:27:00 PM

|
Permalink |
Mawaziri 'wapya' Kuapishwa kesho Mchana
Taarifa ya Ikulu:
Baraza Jipya la Mawaziri litaapishwa na Rais Jakaya Kikwete (pichani) kesho Jumatano saa 7.30 mchana Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma.
Idara ya Mawasiliano Ikulu
Februari 12
Labels: Kuapishwa Mawaziri
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 6:37:00 PM

|
Permalink |
Baraza Dogo, Sura Chache Mpya
1. WAZIRI OFISI YA RAIS (UTAWALA BORA) SOFIA SIMBA
2. WAZIRI OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UMMA) HAWA GHASIA
3. WIZARA OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO) MOHAMED SEIF KHATIB
4. WIZARA YA UTALII NA MAZINGIRA DK. BATILDA BURIANI
5. WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS (SERA NA URATIBU WA BUNGE), PHILIP MARMO
6. WIZARA YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, STEVEN WASIRA
7. WIZARA YA FEDHA MUSTAFA MKURO NA MANAIBU NI JEREMIAH SUMARI NA OMARI YUSUF MZEE
8. WIZARA YA AFYA PROFESA DAVID MWAKYUSA NAIBU NI AISHA KIGODA
9. WIZARA YA ARDHI JOHN CHILIGATI
10. ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI PROFESA JUMANNE MAGHEMBE MANAIBU GAUDENSIA KABAKA NA MWANTUMU MAHIZA
11. WIZARA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA DK SHUKURU KAWAMBA NAIBU NI DK. MAUA DAFTARI
12. WIZARA YA MIUNDO MBINU ANDREW CHENGE NAIBU DK. MAKONGORO MAHANGA
14. WIZARA YA UTAMADUNI NA MICHEZO GEORGE MKUCHIKA, NAIBU JOEL BENDERA
15. WIZARA YA KAZI NA AJIRA POFESA JUMA KAPUYA NAIBU HEZEKIA CHIBULUNJE
16. WIZARA YA MAJI PROFESA MARK MWANDOSYA NAIBU CHIZA
17. WIZARA YA KILIMO NA CHAKULA MATHAYO DAVID MATHAYO
18. WIZARA YA MENDELO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MARGARETH SITTA NAIBU NI DK LUCY NKYA
19. WIZARA YA UVUVI NA MIFUGO JOHN POMBE MAGHUFULI NA MANAIBU NI SHAMSA MWANGUGA NA EZEKIEL MAIGE
20. WIZARA YA MAMBO YA NDANI LAWRENCE MASHA NAIBU NI HAMISI KAGASHEKI
21. WIZARA YA MAMBO YA NJE NI BERNARD MEMBE, NAIBU SEIF ALI IDDI
22. WIZARA YA NISHATI NA MADINI WILLIAM NGELEJA, NAIBU ADAM MALIMA
23. WIZARA YA SHERIA MATHIAS CHIKAWE
24. WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA DK. HUSSEIN MWINYI NAIBU DK EMMANUEL NCHIMBI
25. WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI DK. EMMANUEL KAMALA
26. WIZARA YA VIWANDA NA BISHARA DK. MARY NAGU NAIBU CYRIL CHAMI
Labels: Baraza la Mawaziri
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 5:58:00 PM

|
Permalink |
Huyu Dingi Vipi, Abaki au Aondoke?
Mzee Kingunge Ngombare-Mwiru anaonekana akiondoka. Ndio moja kwa moja au atarudi? Toa maoni yako
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 11:18:00 AM

|
Permalink |
Zigo la Richmond
Hii ndiyo mitambo ya Richmond ikishushwa kutoka kwenye dege kubwa la mizigo kutoka Marekani mwaka jana. Balaa lote lilianzia hapa, kwani mzigo huu ndio pekee uliowezekana. Mwingine uliletwa na Kampuni ya Dowans baada ya Richmond kushindwa kabisa.Labels: Mitambi ya Richmond
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 11:10:00 AM

|
Permalink |
Richmond Ilivyozua Mambo

Hawa waliokuwa mawaziri kabla ya kutemeshwa, Profesa Peter Msolla na Margaret Sitta wakiondoka kwa staili za kila aina. Je watarudi leo?
Labels: Balaa la Richmond
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 11:00:00 AM

|
Permalink |
Bara la JK Utata
Baraza la JK lapipigwa tena danadana. Taarifa kamili:
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kutangaza Baraza la Mawaziri leo(12/02/2008) saa 9.00 alasiri katika ukumbi wa TAMISEMI, Dodoma, badala ya saa 4.00 asubuhi kama ilivyotangazwa awali. Wahariri/Waandishi/Wapiga picha wawe wamewasili ukumbini saa 8.00 Mchana na walewenye waandishi wao Dodoma wawaeleze vema ili wazingatie muda.
Ahsante na karibuni.
Kurugenzi ya Mawasiliano,
Ikulu, Chamwino DODOMA.
12/02/2008 .
Zipo tetesi za kuingiza wapinzani kutoka Chadema na CUF. Yawezekana kweli ni mpango wake, lakini inawezekana amevujisha makusudi ili kusikia wananchi wanasemaje.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 10:51:00 AM

|
Permalink |
Pinda Aapishwa
Waziri Mkuu Mizengo Peter Kayanza Pinda tayari ameapishwa. Ameapa kuwa mtiifu kwa Rais, Katiba, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutokutoa siri za baraza la mawaziri.Labels: Pinda Aaapishwa
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 12:56:00 PM

|
Permalink |
Mawaziri Wakuu Tanzania

JULIUS Kambarage Nyerere alipewa nafasi hiyo na wakoloni Septemba 2,1960 hadi Mei Mosi, 1961 alirejea wadhifa huo Mei Mosi, 1961 hadi Januari 22,1962.
Rashidi Kawawa alishika wadhifa huo Januari 22, 1962 hadi Desemba 9,1962. Pia, aliteuliwa kuendelea na nafasi hiyo Februari 17, 1972 na Februari 13,1977.
Edward Sokoine aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu Februari 13,1977 hadi Novemba 7, 1980 baada ya kwenda masomoni aliporejea aliteuliwa tena Februari 24, 1983 hadi Aprili 12, 1984 alipopata ajali akitokea Dodoma bungeni na kufariki dunia.
Cleopa Msuya alishika nafasi hiyo baada ya Sokoine kwenda masomoni Novemba 7, 1980 hadi Februari 24,1983. Aliteuliwa tena kushika wadhifa huo kuanzia Desemba 7, 1994 hadi Novemba 28, 1995 badala ya John Malecela.
Salim Ahmed Salim, aliteuliwa Aprili 24,1984 hadi Novemba 5, 1985.
Joseph Warioba alishika wadhifa huo kati ya Novemba 5, 1985 hadi Novemba 9, 1990. John Malecela alishika nafasi hiyo Novemba 9, 1990 na Desemba 7, 1994 baada ya kulazimishwa kujiuzulu.
Frederick Sumaye, ndiye Waziri Mkuu pekee aliyeshika na nafasi hiyo kwa miaka 10 mfululizo tangu Novemba 28, 1995 hadi Desemba 30, 2005.
Edward Lowassa aliteuliwa Desemba 30, 2005 hadi Februari 7,2008 baada ya kujiuzulu kutokana na Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza mchakato wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura ulioipa ushindi Kampuni Richmond Development ya Houston, Texas, Marekani kumhusisha na kuingia taratibu za kuisaidia.
Labels: Mawaziri Wakuu Tanzania
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 7:10:00 PM

|
Permalink |
Wawili Wamkataa Pinda
Wabunge wawili wamemktaa Waziri Mkuu. Amepata kura za ndiyo 279. Mbili zilikuwa za Hapana. Moja imeharibika. Jumla ya kura zilikuwa 282. Hivyo, amethibitishwa kwa asilimia 98.9
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 6:29:00 PM

|
Permalink |
Kambi Zote Namkubali Pinda
Wabunge wote waliochangia hoja ya uteuzi, Kiongozi wa Upinzani, Hamad Rashid Mohamed, Waziri Mkuu alitepita, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Spika wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela, Mwenyekiti wa UWT, Anna Abdallah, Mbunge Kijana kuliko wote, Zitto Kabwe na Mbunge mzee kuliko wote, John Malecela wameunga mkono uteuzi wa Kikwete. wamesema Mizengo Pinga ni mzoefu na mwadilifu kiasi cha kutosha. Sasa Kura zinapigwa.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 5:40:00 PM

|
Permalink |
Taarifa za Uhakika
JK amekubali ombi la kujiuzulu la Dk Edward Hosea (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru kuanzia saa 6.00 mchana leo. Anayekaimu ofisi hiyo nyeti, ni aliyekuwa naibu wake, Lilian Mashaka. Takukuru imetajwa kwa kuwalinda watuhumiwa wa ufisadi katika kashfa ya Richmond. Katika Kashfa hiyo kiongozi aliyetajwa na hajajiuzulu hadi sasa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, ambaye bila shaka alibakia ili kukamilisha kazi ya Rais ya uteuzi wa Waziri Mkuu na taratibu za kutangazwa kwake; na pengine kuapishwa kwake.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 5:31:00 PM

|
Permalink |
MIZENGO PINDA WAZIRI MKUU
Rais Jakaya Kikwete amemteua Mizengo Peter Kayanza Pinda kuwa Waziri Mkuu. Pinda ambaye ni Mbunge wa Mpanda Mashariki na alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 1:17:00 PM

|
Permalink |
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 9:22:00 AM

|
Permalink |
SERIKALI IMEBAKI NA WATU WAWILI TU
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali imesalia na viongozi wawili tu. Jakaya Kikwete, Rais na Makamu wake, Dk Ali Mohamed Shein. Basi. Hawa wawili sio wabunge. Bunge limeshindwa kuendelea asubuhi leo bila upande wa serikali. Limesitishwa hadi saa 11.00 jioni. Tunatarajia muda huo Waziri Mkuu Mpya atangazwe. Endelea kusoma hapa.
Imeandikwa na:Reginald S. Miruko Saa 9:05:00 AM

|
Permalink |