Sunday, March 29, 2009

Eti Chenge Anawajua Aliowaua

Hawa ndio wanawake waliogongwa na Andrew Chenge na kufa hapo Ijumaa iliyopita. Vicky (kushoto) na (Beatrice kulia)


Frederick Katulanda, Mwanza

SAKATA la ajali ya gari la Andrew Chenge ambalo limesababisha vifo vya wanawake wawili, limeingia katika sura mpya baada ya ndugu wa wasichana hao kudai kuwa Chenge alikuwa akimfahamu mmoja wa marehemu.
Chenge ambaye alikuwa Waziri na Mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, aliingia matatani baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga "bajaji" usiku wa kuamkia juzi na kuua wanawake wawili ambao ni Beatrice Costantine (kulia) ambaye ni mfanyabiashara wa Mwanza na mmiliki wa saluni ya kike na Vicky George Makanya (kushoto).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Mwanza baadhi ya ndugu waliohojiwa na Mwananchi Jumapili akiwamo mama mzazi wa Vicky, walisema wanafahamu Chenge kuwa alikuwa akimjua ndugu yao Vicky. Mwananchi Jumapili limeandika kwa kirefu.

1 comment:

davidmusika said...

ajali ngapi zilizowahi kutokea bila kuundiwa tume ya uchunguzi kwani hii ina nini? tena watu walikufa ni wawili tu! kule arusha,Tanga watu wangapi walikufa katika ajali na hatukusikia tume? kuna nini kinataka kufichwa hapa? kwanza kabisa inabidi chenge awe jela kwa kuendesha gari bila bima ya gari kwa miaka 2! ebu fikiria ungekuwa wewe unaedesha bila bima ya gari wacha kupata ajali? nahisi bado tanzania hatuna usawa!mbona yule kijana aliyemuua chacha wangwe hakupewa dhamana? au tuseme hao marehemu ndiyo walioua chenge katika ajili hiyo wangepewa dhamana? jamani lazima tutenda haki kwa kila mtanzania kwa vile ni haki ya mtanzania kuwa na haki katika nchi yake.kumwachia mzee chenge huru ni kuendeleza matabaka ya walionacho na wasio nacho.

Post a Comment