Friday, February 10, 2006

Kweli Nyerere Anastahili Utakatifu?

UTASIKIA MENGI. TUMIA BUSARA. mengi hayo ni yapi, ni kuhusu mchakato ulioanzishwa na Jimbo Katoliki la Musoma Kumtangaza Julius Nyerere kuwa Mwenye Heri-hatua ya kwanza kuelekea utakatifu. Kila mtu ana maoni yake, Christopher Mtikila wa Chama cha DP amepinga Nyerere kupata heshima hiyo. Wachungaji kadhaa wa makanisa ya Kiprotestant Dar, wamepinga vile vile. Soma huyu Deogratius Mushi-The Guardian, "I ask myself, why is there lack of enthusiasm among Catholics concerning Nyerere’s process to sainthood? You can hardly hear ordinary people, expressing their satisfaction concerning Nyerere’s process to sainthood. This is not because they hated him or he was not a good person, but simply because they fail to associate his spiritual life and the process to sanctity," . Na wengine wana maoni tofauti juu ya suala hilo, mtazame Mwandishi Maarufu Stanly Meisher anavyosema, "Nyerere was like a saint. Incorruptible, frank, good-humored, intellectual, he could charm the most suspicious and doubtful questioners into following the flow of his logic as he expounded the need in Africa for socialism, one-party democracy, self-reliance, non-alignment...He always made sense, at least in theory, and, since we knew he did not line his pockets with gold or pander to tribalism and racism, we always wished him and his poor country well". Katika mjadala huu hata viongozi wa dini wana mengi ya kumsemea Nyerere na 'utakatifu wake, Fr. Fr Andrzej G Madry C R wa Jimbo la Musoma anasema: "The decision of the bishop of Musoma [to initiate Nyerere's cause] arose from the requests of many people who admired the devout Christian life of the Father of the Nation. They asked the bishop to start investigations that could lead to his beatification." Wewe mwana blogu unasemaje juu ya suala hilo? (Picha kwa Hisani ya Michuzi)

2 comments:

John Mwaipopo said...

Nyerere alikuwa kiongozi shupavu, sawa. Alikuwa hapendi kujilimbikizia mali, sawa. Alipenda wanyonge, Sawa. Aliheshimika hata nje ya nchi pia, sawa.Watanzania woooote tunamheshimu, kumpenda na kumkumbuka kwa busara zake nyiiingi. Hili la utakatifu nini kigugumizi nalo kidogo. Sijui ndio ule unafiki wa kanisa katoliki?

Mija Shija Sayi said...

Kwani ni vigezo gani hasa hutumika kumfanya mtu kuwa Mtakatifu?...kwa anayejua hili anisaidie halafu ndio nitatoa maoni yangu.

Post a Comment