Thursday, March 26, 2009

Chadema Yatimua 15

Chadema ambacho jana kiliripotiwa Mwananchi jana kuandamwa na bundi, kimewavua uanachama watu 15 kwa makosa mbalimbali yakiwamo usaliti na kutoa siri za chama. Waliovuliwa ni Abdul Mateleta, Nasir Chimko, Hamisi Msasa, Abdallah Kaoneka, Mkwanji Maulid, Bimkubwa Uwesu na Peter Katunka, anayedaiwa kuwa mtumishi wa Mbunge wa Ubungo, Charles Keenja.

Wengine ni Zuberi Haji, Kimaro T, Bakari Shingo, Shaaban Salum, Adam Yasin, Said Mareja, Mwanahamisi Sadiki na Martin Mng’ongo, aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Kinondoni, ambaye inadaiwa alikuwa mpangaji na mshauri mkuu wa mpango wa uasi ndani ya chama na anayepeleka nyaraka zote.
Kamati Kuu pia ilitengua nafasi ya mjumbe wa Kamati Kuu ya Mecky Mzirai na kumpa onyo kutokana na kudaiwa kuvujisha siri za chama na kupanga mikakati ya kuleta vurugu ndani ya chama hicho. Hata hivyo rufaa yake ipo wazi kwa siku 14. Zaidi Soma Hapa

No comments:

Post a Comment