Wednesday, March 18, 2009

Dk Mwakyembe Kumwaga Mboga


VYANZO vya karibu vya Dk Harrison Mwakyembe vimesema leo atatoa maelezo yake na vinasema kuwa leo"mstari uliokuwa hauvukwi, utavukwa". Mmoja wa watu wa karibu na Mwakyembe alisema jana, "Dokta atawatolea uvivu kesho". Alipobanwa kuelezea ni kwa jinsi gani uvivu huo utatolewa jamaa huyo alikataa na kusema "subirini kesho". Hadi tunakwenda mitamboni jioni hii haijawekwa sawa mkutano huo utafanyika wapi lakini muda uliopangwa hadi hivi sasa ni saa nne za asubuhi. Chanzo

No comments:

Post a Comment