Friday, March 27, 2009

Chenge asababisha vifo viwili

Bima ya gari lake ilimalizika Juni 06, 2007


Waziri wa zamani wa Miundombinu, Andrew Chenge yuko matatani tena; safari hii gari alilokuwa akiendesha limegonga "bajaji" na kuua wanawake wawili.
Lakini Jeshi la Polisi limeamua kupumzisha taratibu zake za kawaida za kulipeleka suala hilo mahakamani kushughulikiwa kama kosa la usalama barabarani na kuunda tume ya kuchunguza ajali hiyo.

2 comments:

davidmusika said...

ajali ngapi zilizowahi kutokea bila kuundiwa tume ya uchunguzi kwani hii ina nini? tena watu walikufa ni wawili tu! kule arusha,Tanga watu wangapi walikufa katika ajali na hatukusikia tume? kuna nini kinataka kufichwa hapa? kwanza kabisa inabidi chenge awe jela kwa kuendesha gari bila leseni! ebu fikiria ungekuwa wewe unaedesha bila leseni wacha kupata ajali?

davidmusika said...

wewe mwanasheria unaendesha gari bila bima unamaana gani inabidi awe rupango na sijui kwanini wamemuachia huru? au ameanza kutumia vijisenti vyake kufisadi?

Post a Comment