Monday, March 16, 2009

Kesi juu ya Kesi


Machi 16, 2009

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa niaba ya kamati inayoundwa na waandishi, wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari ambao jumla yao ni 13 , ninapenda kuwafahamisha kuwa kesho Machi 17, mwaka huu saa 4.00 asubuhi tunatarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari katika Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.


Dhumuni la kufanya mkutano huo ni kuelezea kusudio lao la kumfungulia mashtaka mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi pamoja na magazeti yake yakiwemo Kulikoni na Nipashe kwa kuwakashifu.

Kashfa hizo ni pamoja na kuwaita waandishi, wamiliki na wahariri hao kuwa ni mafisadi na magazeti yao aliyoyaita kuwa ni vipeperushi, yameanzishwa, kumilikiwa na kufadhiliwa na mafisadi nchini.

Aidha, katika kikao hicho na wanahabari, wajumbe wa kamati wananakusudia kueleza umma ili uelewe kuwa hawana ugomvi binafsi na mwenyekiti huyo bali wanatimiza wajibu kama vyombo vya habari katika kuelimisha, kupasha habari na kuburudisha na si vinginevyo, hii ni pamoja na kuzingatia maadili.

Tunatarajia ushirikiano katika hilo.

……………………
Prince Bagenda
Mwenyekiti wa kamati

No comments:

Post a Comment