Monday, March 23, 2009

Wabaguzi wa vyama vya siasa

Swali la Wiki:

Hili linaweza kuwa la kibaguzi: Hivi kwanini Watanzania wenye asili ya Kiasia wanavibagua vyama vingine vya siasa, yaani huwezi kuwaona kwenye chama zaidi ya hiki kinachotawala--CCM?

8 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mimi nadhani jibu ni rahisi tu - kwenye vyama vya upinzani kuna ulaji gani? CCM kuna Dowans, kuna Radar, kuna.....Siku chama cha upinzani kitakapoingia madarakani basi utawaona huko. Ulaji, ulaji, maakuli....

Anonymous said...

Jimu muhimu ni kwamba hawa jamaa wa kiasia wanaangalia nani anatawala. Kama itatokea wakati wowote chama kingine kishinde utawaona huko kibao. Na hao ndio chanzo kikubwa cha ufisadi kwani wanatumia sana pesa kuwarubuni viongozi wetu ili mradi tu wafanikishe biashara zao haramu.

Anonymous said...

swali lako kama si la kipuuzi ni la kibaguzi,ama la kijinga,wakati wakupigania uhuru,wahindi na baadhi ya wazungu walituunga mkono na sio waarabu,baada ya uhuru baraza lakwanza la mawaziri kulikuwa na mawaziri wazunu na waasia,iyo ni kuonyesha chama tawala akina unbaguzi ukiendelea na maswali yako kuna siku utauliza cuf ina viongozi wangapi au wanachama wakristu,swali lako halina hoja ni la kijinga bure kabisa.

Anonymous said...

kwa sababu ccm ni chama tawala hivyo wanategemea upendeleo fulani. Siku ikichukua tlp watahamia huko.

Anonymous said...

wewe anony 4:39 hasira za nini, unamshambulia bure muuliza swali badala ya kutoa jibu; mbona hao watanzania wenzetu hawaingii chadema, au Cuf sio kuibua masuala yako ya udini na matusi

Anonymous said...

Kweli Miruko, mimi sijawahi kuwaona wahindi au maarabu kwenye vyama vya upinzani, nadhani wanaona hakuna cha kufaidi na hawataweza kuwa karibu na watawala. Ni swali zuri

Anonymous said...

Jamani hata upinzani wapo mbona CUF kuna wapemba, waarabu na wahindi kibao ama mnaogopa kusema kwa kuhofia kukihusisha chama hicho na Hizbu? Kuna mbunge wa Mpanda mwarabu na ni Chadema? Acheni kusingizia CCM, mbona vyama vya wapinzani havina wazee?

Anonymous said...

hakuna wazee vyama vya upinzani! kwani Mzee Shababni Mloo wa CUF aliyefariki majuzi hakuwa mzee? James Mapalala mdogo? Dk Fortunatus masha, baba yake waziri masha mdogo?, Emmanuel Makaidi je? maalim seif? John Cheyo?... hao wanatosha

Post a Comment