Monday, June 29, 2009

Enzi Mpya ya Chiluba


Kila enzi na kitabu chake. Hii ndiyo enzi mpya ya Frederick Chiluba wa Zambia. Viongozi wetu hasa Afrika 'wana-enjoy' sana wanapokuwa madarakani. Sina wivu nao kama walacho ni halali yao, lakini kama wanakula halali ya wananchi wao, sina huruma yanapowakumba haya ya Chiluba . Soma zaidi hapa.

Sunday, June 28, 2009

Buriani Profesa Haroub Othman

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Prof Haroub Othman (pichani) amefariki dunia alfajiri ya leo katika Kisiwa cha Unguja mjini Zanzibar. Habari zilizoifikia blog hii zinasema Prof Othman alifariki akiwa usingizini na usiku alikuwa katika tamasha la Majahazi lililoanza jana visiwani humo.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala Pema Amina.
Haroub tutamkumbuka kwa makala zake nyingi na uchambuzi kadhaa juu ya mambo yanayoendelea nchini na Duniani, mfano makala yake hii.

Source: Kidevu

Saturday, June 27, 2009

Sheikh Gorogosi Afa Ajalini

Breaking News
Taarifa mbazo bado ni moto ni kwamba Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheik Suleiman Gorogosi amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea kwenye Kijiji cha Mnolela Wilaya ya Lindi Vijijini baada ya tairi ya mbele ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Mtwara kupasuka na kupinduka.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Sifuel Shirima zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea jana saa 8:09 katika barabara ya Mtwara-Lindi wakati akitokea Uwanja wa Ndege Mtwara baada ya kushuka kwenye ndege akitoa jijini Dar es Salaam.

Kamanda Shirima alisema katika gari hilo kulikuwa na watu watatu, akiwamo Bakari Maguo, mfanyabiashara wa Lindi ambaye ni mmiliki wa gari hilo na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Lindi mjini, Bakari Fundi ambao wamejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Ligula mkoani Mtwara.

Gorogosi alikuwa amekwenda Lindi kufungisha ndoa ya mtoto wa Maguo ambaye ni mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Taifa la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambayo ilikuwa ifungwe leo.

Ndugu wa marehemu Abilahi Mohammed aliiambia Mwananchi Jumapili jana kuwa mazishi wa Gorogosi ambaye alikuwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Lindi yatafanyika saa 10:00 jioni leo jioni mjini humo.

Pia Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata), lilitoa taarifa jana jioni likieleza kuwa Gorogosi lilithibitisha kifo cha Gologosi na kueleza kuwa atazikwa leo.
Marehemu ameacha wake wawili. Kabla ya kifo chake alikuwa pia mjumbe wa baraza la Ulamaa la Bakwata.

Lwakatare Rasmi Chadema

Dk Slaa amkabidhi Lwakatare kadi ya Chadema

Frederick Katulanda, Bukoba

ALIYEKUWA naibu katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilfred Lwakatare jana amehama rasmi chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa jana alimkabidhi rasmi kadi Lwakatare katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Uhuru mjini Bukoba.

Akizungumza na wananchi kabla ya kukabidhiwa kadi ya Chadema, Lwakatare alisema uamuzi wake wa kukihama CUF umetokana na ushauri wananchi wa jimbo hilo Lwakatare aliyevalia mavazi rasmi ya Chadema, alisema baadhi ya watu wanadhani uamuzi wake huo unatokana na fedha lakini mawazo hayo ni potofu kwani yeye ni adui wa rushwa na kamwe hatohamia chama chochote kwa kupewa fedha.

“Nimejiunga Chadema siyo kwa sababu ya fedha, maana kuna watu wanasema nimelipwa milioni 80. Jamani sijalipwa hata shilingi moja, ninahama CUF kwa sababu ya kutaka maendeleo ya watu, siingii katika chama kwa sababu ya kutaka ukuu wa mkoa au udiwani bali kwa sababu nataka kuwatumikia wananchi” alieleza.

Zombe OUT?

Wazee wa Baraza wamemwona ACP Abdallah Zombe hana hatia. Wanasema ushahidi uliotolewa haukumhusisha na mauaji na zaidi ya yote hakwenda kwenye msitu wa Pande, mauaji ya wafanyabiashara wa magenge yalikofanyika. Anasubiriwa jaji tu... Full Report

Friday, June 26, 2009

Zombe Atafutiwa Kifungu Chake

Mawakili wa serikali katika kesi ya akina Zombe wamependekeza adhabu mbadala kwa watuhumiwa wawili, akiwamo mshtakiwa wa kwanza, Abdallah Zombe, bila shaka baada ya kuhisi kuwa wanaweza kuchomoka katika Hatia ya Mauaji ya Kukusudia (Murder)
Kiongozi wa Jopo la mawakili hao, Revocatus Mtaki katika kuhakikisha kuwa washitakiwa wote hawaponi katika ghadhabu ya mkono wa sheria, aliiomba mahakama iwatie hatiani kwa kosa mbadala Zombe na mshtakiwa wa 13, Koplo Festus Gwabisaba, ikiwa mahakama itaridhika kuwa hawahusiki kwa kuwa kwa ushahidi ulioko mahakamani wao hawakwenda katika eneo la mauaji katika Msitu wa Pande.
“Kama mahakama itaona kuwa mshtakiwa wa kwanza (Zombe) na wa 13 (Gwabisabi) hawakushiriki katika mauaji kwa kuwa kwa ushahidi ulioko mahakamani hawakwenda Pande, basi iwatie hatiani kwa kosa Accessory after the facts (mshiriki baada ya kosa) chini ya kifungu cha 213,387(i) na 388 cha Penal Code,” alidai Mtaki. Habari Kamili

Millingo Asimika Askofu Aliyeoa

Askofu Mkuu aliyetimuliwa katika Kanisa Katoliki, Emmanuel Millingo (kushoto) akiwa na mkewe, Maria Sung kwenye picha ya pamoja na mmoja wa maaskofu wake wapya, aliowasimika nchini Kenya, Daniel Kasomo na mkewe, MaryAnne Kasomo. Mapadri kadhaa nchini Kenya wamejitenga na Kanisa Katoliki na kuanzisha dhehebu lao, Married Priests Now. Full Report

Tangulia Michael Jackson


Msanii nguli wa Muziki wa Pop, Michael Jackson amefariki dunia leo usiku wa saa 7 majira ya Tanzania, kutokana na ugonjwa wa moyo. Mdogo wake amenukuliwa na vyombo vya habari kuwa Jackson alicollapse akiwa nyumbani, akatangulia kwa muumba wake. Atakumbukwa mambo mengi, muziki mzuri, kubadili sura, na vitendo vingine...

Thursday, June 25, 2009

Update Kuhusu Zitto

Spika wa Bunge, Samuel Sitta amesema anachunguza kauli ya Zitto Kabwe na kitendo chake cha kukataa uamuzi wa meza, uliomtaka afute kauli yake kuwa Waziri amesema mambo ya hovyo hovyo.
Tayari Zitto kashasema yuko tayari kwa lolote. Duru za karibu na Zitto zinasema, kama angetimuliwa bungeni, angwenda moja kwa moja Biharamulo kwenye kampeni za uchaguzi, nyingine zinasema ana safari ya Nairobi.
Hata hivyo, Spika amesema atatoa uamuzi huo wiki moja baadaye, kipoindi ambacho siku za kumaliza kampeni zitakuwa zimekaribia, kwa kuwa uchaguzi mdogo ni Julai 5.

Wednesday, June 24, 2009

Zitto Atikisa Tena Bunge

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto mchana huu ametingisha kiberiti cha bunge baada ya kukataa 'kufuta' matamshi yake, kuwa majibu aliyotoa Waziri Sumari kwa Mh. Slaa ni ya HOVYOHOVYO..." pamoja na pressure ya wazi toka kwa wabunge wa wakiomba mwongozo wa Mwenyekiti, Zitto aligoma katakata kufuta kauli yake na kudai kwamba wabunge kadhaa wameshaongea kauli za kutatanisha katika bunge hili lakini hakuna hatua zilizochukuliwa..alimalizia kwa kusema "NIPO TAYARI KWA LOLOTE" kabla hajendelea kuchangia mjadala wa bajeti. Bunge linaendelea kuwaka moto baada ya jana kuwa namna hii. Mjadala juu ya suala lake unaendelea kukomaa kwenye forum ya Bidii na wengine wako hapa kwenye Jamii Forum

Monday, June 22, 2009

Wabunge 'Bubu' Bungeni Hawa


"...Kwa mujibu wa mtandao huo, Bunge, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ndiye pekee ameonyeshwa kuwa hajawahi kuuliza swali lolote wala kuchangia jambo lolote tangu Bunge limeanza. Habari za kina hapa.

Sunday, June 21, 2009

Hii ya 'Je, Tutafika' Imekaaje?

Source: Bidii Forum

Mimi ni mmojawapo wa wapenzi wa kipindi kinachorushwa na Channel 10 kila Jumanne: Je, tutafika? Kipindi hiki huwa kina mada nzuri ingawa mara nyingi ‘animator’ anakiharibu, hasa anapozungumza zaidi kuliko wachangia mada. Anakera sana kwa hili na nadhani halijui hilo!

Pamoja na hoja nzuri zinazojadiliwa na kipindi hiki, linapokuwa ni swala linalohusu dini, ‘animator’ wenyewe anakuwa na ‘bias’ fulani, ambayo nimeona ni vizuri niiweke wazi. Kati ya mijadala inayohusu mambo ya dini nilishasikiliza miwili.

Wa kwanza ulihusu MAHAKAMA YA KADHI na wa pili kijitabu kilichoandaliwa na Chirstian Professionals of Tanzania (CPT) na kupitishwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kuhusu
MPANGO WA KICHUNGAJI KUELEKEA UCHAGUZI UJAO.

Katika mijadala yote miwili niliona kuwa ingawa ‘animator’ anaonekana akipinga udini lakini yeye mwenyewe ndiye aliyejaa huo udini. Katika mada ya kwanza yeye mwenyewe alionyesha upande aliokuwa akiuunga mkono na hivyo alijaribu kuweka ‘leading questions’ kwa wachangiaji ili wachangie kile alichotaka kuhitimisha na kilichohusu: kwa nini maaskofu wanapinga Mahakama ya Kadhi ambayo ni haki ya Waislamu? Kwa uelewa wangu hakuna anayepinga Mahakama ya Kadhi kama itaanzishwa nje ya Katiba kwa vile "Nchi haina dini na mambo yanayohusu imani ni watu wenyewe".

Katika mada ya pili, alikuwa na ‘tactics’ zilizile na ilionekana wazi kuwa anachochea udini zaidi badala ya kuelemisha umma wa Watanzania kuhusu mada yenyewe.

Mfano, katika mada zote mbili ‘selection’ ya wachangiaji haikuonyesha kuwa na uwiano mzuri. Aliwachagua watu wa dini fulani wengi zaidi na wenye uelewa wa dini yao kuliko wale aliowachagua wa dini ya pili na pengine alichagua wale alioona wanamwelekeo anaoutaka.

Kwa mada ya pili pia alifanya hivyohivyo. Dini moja aliwachagua watu 3 wenye uelewa mzuri wa dini yao na nyingine wawili (mmoja mchungaji Lusekelo) na kati ya hao wawili, mmoja hata hakujua kitu gani cha kuchangia. Na hivyo, baada ya mada yenyewe, hitimisho lilielekea upande mmoja aliotaka huyo ‘animator’ umma wa Watanzania ujue ndiyo Maaskofu wa Kanisa Katoliki wana udini na wanahatarisha amani ya nchi yetu kwa kujiingiza kwenye siasa.

Yaani waraka wao unaowataka watu watumie vizuri haki ya kuchagua viongozi waadilifu na wenye uchungu na nchi yao bila kujali dini, itikadi ya chama au kabila la mtu, yeye anaona hiyo siyo kazi ya madhehebu ya dini. Wachangiaji wote siku hiyo (Jumanne, June 16, 2009) walikuwa na mtazamo huo na ndivyo ‘animator’ wa kipindi alivyotaka Watanzania waelewe.

Lakini mimi huwa najiuliza kama huyu ‘animator’ ana nia ya kuelemisha jamii na hana udini, kwa nini huwa hawaaliki, mfano, padri au askofu fulani wa dhehebu husika ili nao waeleze upande wao na kuacha wasikilizaji waamue kulingana na jinsi walivyosikia maelezo yenyewe kuliko yeye kujifanya ndiye anayewaalimua?

Yeye kama ‘seasoned journalist’ nilitegemea awe mtu ‘open’ na asiye na udini lakini kwa mada hizo mbili na pia baada ya kusoma ‘articles’ zake alizoandika kuhusu hizo mada, niligundua kuwa ana ajenda ya siri na ni mtu aliyejaa udini kuliko anavyonekana anaupinga.

Katika mada ya pili alisisitiza zaidi kwa nini Kanisa linajiingiza kwenye siasa na kusema kufanya hivyo ni kuhatarisha amani ya nchi. Wachangiaji wengine nao pia walikuwa na maoni hayohayo.

Of course, inategemea yeye anafahamu nini katika ‘kuchanganya dini na siasa’. Binafsi naamini kuwa mwumini mzuri wa dini atakuwa mwanasiasa mzuri pia na mwanasiasa mzuri akiingia kwenye dini atakuwa mwumini mzuri vilevile. Dini au siasa havimuharibu mtu bali mtu ndiye anayeharibu dini au siasa.

Mtu mwenye imani nzuri ya dini au mtu mwadilifu lazima atafanya pia siasa yenye uadilifu. Madhehebu ya dini, mfano, yanachangia katika maendeleo ya nchi – ikiwa ni pamoja na siasa (kuhamasisha waumini wao wachague viongozi/wanasiasa waadilifu), huduma za jamii – elimu, afya,
etc.

Ukisema madhehebu ya dini yajiondowe kwenye siasa – yaani yajiondoe kwenye maendeleo ambayo ni siasa, elimu, afya, etc una maana kuwa unataka kuwafuga baadhi ya watu/Watanzania kutokuwa Watanzania halisi. Siasa ya Tanzania ni ya watu wote – wawe wachungaji, mashehe, mapadri au maaskofu au watu wa dini nyingine. Kwa maana hii, siasa na dini zinapaswa zifanye kazi moja ya kukamilishana. Ni kama anayekwea ngazi anashika pande zote mbili kwa wakati mmoja – yaani imani yake inaleta changamoto mwenye siasa na siasa inasaidia imani yake kukua vizuri kwa kuinjengea mazingira ya uhuru wa kutosha wa kuamini na kuabudu. Kufanya hivyo siyo sawa na kuchanganya dini na siasa bali ni
kuwajibika kwa imani/mwumini au kiongozi wa dini.

Kitu kinachokatazwa kufanyika katika madhehebu ya dini ni kuwa na viongozi wa kiroho wanaoshabikia chama kimoja dhidi ya kingine kwa sababu kufanya hivyo kutaleta msukosuko kati ya waumini na wananchi kwa ujumla kwa vile katika dini fulani kuna waumini wa vyama mbalimbali.

Na dini au dhehebu likishabikia chama kimoja, hapo inakuwa si sahihi. Kwa vyovyote vile kutakuwa na mwingiliano wa kimasilahi na vurugu. Lakini kusema usichanganye dini na siasa – kwa maana ya kusema usichangie kuboresha sisasa ya nchi – yaani maendeleo ya nchi, hapo naona ni kitu kisichoeleweka kabisa.

Dini zinapaswa kukamilisha sehemu ambazo serikali inashindwa au inafanya kwa kulegalega. Kwa sababu huwezi kusema mchungaji, padri, shehe au askofu achangie maendeleo ya nchi na kumkataza asichangie kuboresha siasa ya nchi yake. Kufanya hivyo ni kumfuga. Sijui ‘huyu seasoned journalist’ anaelewa nini kuhusu siasa na wanasiasa.

Kwa vile kila anayezaliwa ni mwanasiasa, inawezekanaje tuwe na baadhi ya watu wasioruhusiwa kuchangia kuboresha siasa/maendeleo ya nchi yetu au hoja ni kwa vile Kanisa linahamasisha waumini na wananchi kwa ujumla kuhusu kutumia haki yao ya kikatiba ya kushiriki katika mambo yote yanayohusu maendeleo ya nchi na maendeleo yao wenyewe?

‘Civic education’ katika Kanisa katoliki haikuanza leo au jana. Ni kitu cha miaka na miaka na ‘animator’ wa “Je tutafika?” anaona ‘civic education’ haipaswi kufanyika kanisani. Kanisa Katoliki linaamini kuwa imani lazima inonekane katika matendo. Na kuwa na mchakato wa kuwapa waumini uelewa mzuri kuhusu haki zao za msingi sidhani kama ni kazi ya serikali tu. Hii ni kazi ya kila mtu, kila dhehebu la dini na taasisi mbalimbali.

Friday, June 19, 2009

Maendeleo kuhusu the Utamu.

Source ya habari habari ya theutamu, Swahili Time imelazimika kuiondoa mtandaoni baada ya kuwepo taarifa za kutatanisha, kuhusu ukweli wake. tutaendelea kufahamishana yanayojiri. Taarifa zaidi zinazosambaa sasa zinaeleza kuwa huyo bwana hajakamatwa. Mmoja aliandika hivi kwenye Bidii:

So far ni uzushi.dogo ni mtoto wa mweshimiwa Lusinde,ukoo wa malechela.todate yupo Uk yeye na familia yake wakila kuku raha mustarehe.so all of this news about him ni huzushi.nimeonana na kuongea na wana familia yake wamenithibitishia hilo.Tanzania wanaitaji sana kuinvest kwenye CYBE CRIME TECHNOLOGIES kuliko chochote kile wamaitafuta utamu baada ya Mweshuimiwa Rais kutolewa how about walala hoi waliojiua kutokana na UTAMU?.how about wizi wa mabenki kupitia internet ambao sofar umesababisha zaidi ya 25 million USD kuibiwa katika kipindi cha miezi 7 iliyopita?serikali yetu inakumbatia siasa kuliko technology.wao todate wanaamini watanzania ni mamuma but sio kweli CCM wanatakiwa kujua kuwa Karne ya kupigiwa kura kwa sababu eti wamegawa fulana au pilau zimeisha.kikwete inabidi astafishe vikongwe atoe ajira kwa vijana aone vinginevyo tumeumiaSIKU NJEMA

Wednesday, June 17, 2009

Nukuu ya Leo

"Na nikanukuu usemi wa kiingereza “wrong diagnosis wrong Treatment” na nikatoa ushauri wa kukutaka Mhe. Mwenyekiti uunde Kamati ya wataalam na wazoefu wa shughuli za kiuchaguzi walio ndani ya chama na hata nje mkae na kutengeneza mfumo, mbinu na utaratibu utakaokiwezesha chama kurejesha ari ya kupendeka na wagombea wetu kuchaguliwa na kushinda chaguzi. Ushauri ulioonekana si muhimu kwa sasa na nikapuuzwa.

Mh Mwenyekiti; naomba sasa nimkabidhi barua yangu ya kujiuzulu Mhe. Katibu Mkuu ambapo uamuzi huu unaanza mara baada ya kumkabidhi barua hii. Najua kujiuzulu kwangu kutapelekea kutolewa tafsiri mbali mbali zilizo za kweli na zisizo za kweli.

Najua kujiuzulu kwangu kutawasononesha na kuwakwaza wengi,
Najua kujiuzulu kwangu kutawafaidisha baadhi ya watu ambao sasa watapumua na kujisemea kama wahaya wasemavyo “TWAMWIYUKAO” AU KWA TAFSIRI “BORA
AONDOKE ALIKUWA AMETUKALIA PABAYA”

Mimi kwangu yote ni mazuri tu; tunapaswa tumuachie Mwenyezi Mungu; “Ni Kheri
Nusu shari kuliko shari kamili”

Nilipokutana na Mhe. Katibu Mkuu kwa maongezi wiki mbili baada ya kupumzishwa Unaibu Katibu Mkuu na kuteuliwa Bw. Joran Bashange; nilimwambia Katibu Mkuu kuwa siku ya Jumapili baada ya Uteuzi nilikwenda kanisani na baada ya Ibada niliamua nimuone mchungaji wangu wa kanisa nimweleze yaliyokuwa yamenielemea moyoni mwangu. Mchungaji baada ya kunisikiliza hakuwa na maneno marefu bali alisema;

“Sikiliza Wilfred; Maandiko matakatifu katika Biblia yanasema, kila jambo linalotokea Duniani na kila linapotokea Mungu ana makusudi katika jambo hilo” Na akazidi kuniambia; “SHUKURUNI MUNGU KWA KILA JAMBO”
Maneno hayo ndiyo yanayonipa nguvu na faraja hadi leo na kesho.

Mhe. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mhe.Katibu Mkuu na Waheshimiwa wajumbe wa Baraza Kuu.

NAWASHUKURUNI SANA KWA KUNISIKILIZA"
Wilfred Lwakatare

MCHANGO NA MAONI NILIYOYATOA NDANI YA KIKAO CHA BARAZA KUU LA TAIFA,
CHA TAREHE 09/06/2009
KATIKA AGENDA YA KUTOKANISHA
MUHTASARI WA KIKAO CHA BARAZA KUU CHA TAREHE 28/2/2009.

Saturday, June 13, 2009

CUF Yaja ya 'Operesheni Zinduka'

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)


maazimio ya KIKAO CHA baraza kuu la uongozi la taifa kILICHOFANYIKA OFISI KUU, BUGURUNI, MJINI DAR ES SALAAM TAREHE 8 – 9 Juni, 2009
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lilipokea, kuzijadili na kuzifanyia maamuzi agenda 11 ambazo ni pamoja na Tathmini ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa Nne wa CUF uliofanyika Februari 2009; Tathmini ya Uchaguzi Mdogo katika Jimbo la Busanda, Tanzania Bara na Magogoni, Zanzibar; Programu ya Kuimarisha Chama kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji wa 2009 na Uchaguzi Mkuu wa 2010; Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Chama kwa mwaka 2009; Mapendekezo ya Mchakato wa kupatikana Wagombea nafasi za Uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu; Mapendekezo ya Ratiba ya Uteuzi wa Wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani, Kupitisha Rasimu za Kanuni za Jumuiya ya Vijana wa CUF na Jumuiya ya Wazee wa CUF; na Taarifa ya Hali ya Kisiasa Nchini.

Baada ya mjadala wa kina kuhusiana na agenda hizo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo kuhusiana na masuala hayo:
...14 LIMEAMUA viongozi wa kitaifa wa CUF kuongoza Programu Maalum ya kuuandaa umma wa Watanzania kuleta mabadiliko makubwa ya kisiasa kwa kukiangusha CCM na kuchagua CUF, Chama Mbadala, kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji mwaka 2009 na uchaguzi mkuu wa 2010. Programu hiyo itakayohusisha kazi maalum ya kuwazindua Watanzania juu ya wajibu wao wa kihistoria itakuwa katika operesheni maalum itakayojulikana kama ‘Operesheni Zinduka’. Operesheni hiyo kabambe itakayowafikisha viongozi wa kitaifa wakishirikiana na wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kutoka kila kanda kati ya Kanda tano za Tanzania Bara na Kanda mbili za Zanzibar pamoja na mtandao wa Chama cha CUF wa Viongozi wa Wilaya, Kata na Matawi itaambatana na uzunduzi wa ‘Dira ya Mabadiliko’ (Vision for Change) ambayo ndiyo itakayotumiwa na CUF kama mwongozo wa sera zake kuelekea 2010.

15 Limeagiza Kamati ya Utendaji ya Taifa kusimamia taratibu zote za maandalizi ya CUF kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka huu wa 2009 na taratibu za kuwapata wagombea wa CUF wa nafasi za Ubunge na Udiwani mapema iwezekanavyo ili waanze kazi ya kutekeleza ‘Operesheni Zinduka’ na kuitangaza ‘Dira ya Mabadiliko’ (Vision for Change) katika maeneo yao na hivyo kukiweka CUF katika nafasi nzuri ya ushindi kwa kuongoza mapambano ya kuing’oa CCM madarakani.

Thursday, June 11, 2009

Bajeti ya Serikali 2009/2010

Ni Bajeti ya Kujihami na Msukosuko wa uchumi, ndivyo Gazeti la Mwananchi limeitafsiri bajeti ya serikali mwaka 2009/10.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo amemaliza kusoma bajeti ya serikali ya Sh9.5 trilioni. Kwa kiwango kikubwa bajeti iliyosomwa leo jana ilichambuliwa na Rais Jakaya Kikwete, hasa katika eneo la kujihami na msukosuko wa uchumi. Kipya alichoeleza ni jinsi ya kupata ongezeko la bajeti kutoka 7.2 trilioni za mwaka 2008/09. Bajeti Kamili Pia Waziri Mkulo aliwasilisha mwelekeo wa Hali ya Uchumi.

Wednesday, June 10, 2009

Timu ya Vijana yatolewa Nusu Fainal

For Immediate Release

Dar es Salaam, Wednesday 10th June 2009...
COPA Coca-Cola defending champions, Tanzania, failed to go through to the finals after it lost its game today to Nigerian 2-1 at the ongoing COPA Coca-Cola Inter-Africa Tournament in Pretoria, South Africa.
Tanzania will now play Malawi for the third position in the tournament. SOMA ZAIDI

POOL A

Team Pld W D L GF GA GD Pts
1 Tanzania 5 4 1 0 14 4 10 13
2 Malawi 5 3 1 1 12 5 7 10
3 Kenya 5 2 2 1 13 3 10 8
4 Africa Invite 5 2 0 3 7 13 -6 6
5 Ethiopia 5 2 0 3 7 16 -9 6
6 Namibia 5 0 0 5 4 12 -8 0


POOL B

Team Pld W D L GF GA GD Pts
1 South Africa 5 4 1 0 10 4 6 13
2 Nigeria 5 3 1 1 15 2 13 10
3 Zambia 5 2 3 0 11 4 7 9
4 Zimbabwe 5 2 1 2 12 8 4 7
5 Uganda 5 1 0 4 5 12 -7 3
6 Botswana 5 0 0 5 2 22 -20 0

JK ahami Uchumi Kama Obama

Rais Jakaya Kikwete amehutubia taifa kupitia kwa wazee wa Mkoa wa Dodoma na wabunge. Amezungumzia zaidi msukosuko wa uchumi duniani kwa mapana yake na hali ya uchumi kwa ujumla; na overview ya bajeti. Kwa namna fulani, ni kama ame-pri-empty hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha ya kesho cheki hapa. JK ameibua kitu kipya cha serikali kudhamini madeni ili kupunguza makali ya uchumi wa dunia. Mdau kanitumia SMS akihoji, je, hiyo si EPA nyingine? Reuters wameandika hivi na Hotuba Kamili Hii Hapa.

Wakati huo huo, Kurugenzi ya Mwasiliano Ikulu imesema yafuatayo: Mambo makuu katika Hotuba ya Rais, Dodoma, – jumatano, Juni 10, 2009.

1. Rais ameelezea hali ya mtikisiko wa uchumi duniani, chimbuko la mtikisiko huo na athari za hali hiyo kwa uchumi wa Tanzania. Athari hizo ni kama ziafuatazo:

(a) Bei na mahitaji ya bidhaa za Tanzania kwenye masoko ya kimataifa yamepungua.
(b) Mahitaji na bei za madini ya vito vimepungua kwenye masoko ya kimataifa
(c) Mahitaji ya mazao ya kilimo ya Tanzania kama vile maua na mboga yamepungua kwa asilimia 25
(d) Viwanda vya ngozi, nguo, nyuzi na mavazi pia vimeathirika na hivyo kuathiri pia upatikanaji wa ajira nchini
(e) Sekta ya utalii ambayo ndiyo kubwa kwa uingizaji wa fedha za kigeni pia imeathirika kwa watalii wanaokuja nchini kupungua
(f) Mapato ya Serikali pia yamepungua na hivyo kuathiri mapato ya ndani na mapato ya fedha za kigeni
(g) Uwekezaji kutoka nje umepungua pia na baadhi ya makampuni yaliyokuwa yanataka kuja kuwekeza Tanzania, ama yameahirisha ama yamefuta mipango yao ya uwekezaji. Mifano ni mradi wa uwekezaji katika nickel pale Kabanga, Ngara, Kagera na miradi ya umeme, saruji, mbolea na aluminium smelter mkoani Mtwara
(h) Hali ya ajira nchini imekuwa mbaya zaidi kwa sababu ya matatizo hayo ya uchumi na hadi Aprili, mwaka huu, kiasi cha watu 48,000 walikuwa wamepoteza ajira
(i) Vile vile kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania inakadiriwa kuwa itapungua kutoka kwenye asilimia 7.4 kama ilivyobashiriwa mwaka huu hadi kufikia asilimia 5 hadi 6.

2. Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete ametangaza mkakati wa kuhami na kunusuru uchumi wa Tanzania kwa malengo makuu manne yafuatayo:

(a) Kulinda ajira na vipato vya wananchi
(b) Kuhakikisha upatikanaji wa chakula
(c) Kulinda uwekezaji muhimu katika miradi ya maendeleo, hususan miundombinu
(d) Kulinda programu muhimu za kijamii

3. Kutokana na hali hiyo, Rais ametangaza hatua zifuatazo katika kutekeleza mkakati huo wa kuunusuru uchumi (rescue package):
(a) Serikali imeamua kufidia hasara waliyopata wanunuzi wa mazao kwa msimu uliopita wa 2008/2009. Hasara hiyo ni kiasi cha bilioni 21.9 na Serikali italipia hasara hiyo ambayo imetokana na kushuka ghafla kwa bei ya mazao ya Tanzania kwenye soko la kimataifa
(b) Serikali itatoa udhamini kwa kuahirisha mikopo ya walioathirika ambao ni pamoja na viwanda, utalii, kilimo na sekta nyingi za uchumi kwa muda wa miaka miwili. Serikali imeyataka mabenki kutokutoza riba kwenye mikopo hiyo katika miaka hiyo miwili
(c) Serikali itatoa mitaji ya uendeshaji (working capital) kwa riba nafuu na itayakopesha mabenki kwa riba ndogo ya asilimia mbili na mabenki hayo yatatakiwa kuwakopesha wahitaji kwa riba ndogo zaidi kuliko ilivyo sasa.
(d) Serikali imedhamiria kuboresha mifuko ya dhamana ikiwa ni pamoja na mifuko ya kukopesha biashara ndogo ndogo kwa kuiongezea fedha zinazoweza kukopwa na wananchi
(e) Serikali imeamua kuongeza kasi ya uzalishaji chakula kwa kutoa mikopo ya thamani ya bilioni 20 kupitia Benki ya TIB, na pia kutoka kiasi kingine cha sh bilioni 20 kwa ajili ya mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya ununuzi wa zana za kilimo kupitia taasisi za karadha, na kuongeza idadi ya wakulima watakaopata mbolea ya ruzuku na kiasi cha bilioni 90 kwa ajili ya mboleo hiyo. Vile vile, Serikali imeamua kuanza kuutumia Mfuko wa Hifadhi ya Chakula (SGR) kupunguza bei ya vyakula kwa wananchi na hifadhi hiyo itaongezewa fedha za kununulia chakula zaidi
(f) Serikali imeamua kukwamua mradi wa kusambaza umeme mkoani Mtwara na pia kuboresha Reli ya Kati kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 43.
(g) Serikali imeamua kuhakikisha kuwa programu zote za kijamii kama maji, elimu na afya kama vile ya kupambana na magonjwa ya ukimwi, kifua kikuu na malaria haziathiriki kwa sababu ya msukosuko wa sasa wa kiuchumi.
(h) MPANGO wote huu utaigharimu Serikali kiasi cha sh bilioni 1, 692.5 (karibu sh trilioni 1.7). Fedha hizo zimetengwa katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2009/2010 inayoanza Julai Mosi, 2009.
Sehemu kubwa ya fedha hizo ni za ndani ya nchi ingawa kutakuwapo na michango ya wabia wa maendeleo kama Benki ya Dunia, Shirika la Fedha Duniani (IMF), Serikali ya India na Umoja wa Ulaya (EU).

Tuesday, June 09, 2009

Ghailani Kizimbani Leo

WASHINGTON – U.S. authorities have brought the first Guantanamo Bay detainee to the United States, flying him into New York to face trial for bombing U.S. embassies in Tanzania and Kenya, the Justice Department said Tuesday.

The department said
Ahmed Ghailani arrived in the early morning hours Tuesday. U.S. Marshals took custody of Ghailani from his military jailers and brought him to the Metropolitan Correctional Center in Manhattan. Ghailani is scheduled to appear in Manhattan federal court later Tuesday.

"With his appearance in federal court today, Ahmed Ghailani is being held accountable for his alleged role in the bombing of U.S. Embassies in Tanzania and Kenya and the murder of 224 people," Attorney General Eric Holder said in a news release. "The Justice Department has a long history of securely detaining and successfully prosecuting terror suspects through the criminal justice system, and we will bring that experience to bear in seeking justice in this case
." Soma zaidi hapa.

Breaking News

Imetokea ajali ya basi la Hajjs mkoani Dodoma, lililokuwa linatoka Dar es Dalaam. Watu 6 wameripotiwa kufa papo hapo na majeruhi ni zaidi ya 15. Nitaendelea kuhabarishana.

Mambo Yaanza Bungeni


The legislators meet in Dodoma from 9th June 2009 for the Budget session. The 16th Session of Parliament is expected to continue up to the end of July.

The Finance Minister, Hon. Mustafa Mkullo,MP is expected to deliver a budget speech on the on Thursday 11th June 2009 and thereafter Members of Parliament will debate on the budget of the next fiscal year.

Each Ministry will in due course present their budget for 2009/10 to the legislators for discussions in House.

Hata hivyo, Taarifa hiyo ya Bunge, haikuweka bayana sababu za kipindi cha mkutano kupunguzwa kutoka miezi mitatu hadi mwezi mmoja na majuma matatu. Kwa Kina soma hapa.

Monday, June 08, 2009

Kiongozi Mpya Asimikwa Jimbo la Same

Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Joseph Chennoth (kushoto) akiwa na Msimamizi Mpya wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Same, Padri Rogath Kimaryo baada ya kusimikwa rasmi kuwa kiongozi wa jimbo hilo katika Misa Takatifu ya Jumapili iliyoongozwa na Balozi huyo katika Kanisa Kuu la Parokia ya Same mkoani Kilimanjaro. (Mzee Kidevu)

Na Waandishi Maalumu, Same

Wakati kiongozi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Same, Padri Rogath Kimaryo alisimikwa jana, jimbo hilo limeelezwa kuwa liko hatarini kuingia katika machafuko makubwa endapo makasisi, viongozi wa kidini na waumini wa kawaida wataendeleza mgawanyiko ambao hivi sasa uko dhahiri miongoni mwao za kina ziko hapa.

Mwakilishi wa Baba Mtakatifu hapa Tanzania, Joseph Chennoth jana alimsimika rasmi padre Rogathe Kimario kuongoza Dayosisi ya Same ya Kanisa Katoliki katika ibada iliyokuwa na ulinzi wa jeshi la polisi kila kona ya kanisa hilo Soma Hapa.



Sunday, June 07, 2009

Askofu Akana Kushiriki Freemason

Askofu Jacob Koda (pichani mwenye msalaba, akiwa na mapadri walio chini yake) ambaye amevuliwa mamlaka ya kuongoza jimbo Katoliki la Same 'amezushiwa' kuwa hatua hiyo imechukuliwa kwa sababau anashiriki ibada za mashetani maarufu kama Freemason, lakini yeye ameibuka na kukana tuhuma hizo, huku akiweka wazi kile anachodai ni sababu ya hatua hiyo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti la Mwananchi, alisema: “Sijashiriki na sitashiriki dini hiyo lakini wanaozusha hayo mambo wajue muosha naye huoshwa, hivyo walivyonisingizia siku sio nyingi vitawarudi”.

Askofu Koda ambaye hata hivyo alisisitiza kuwa yeye bado ni askofu hadi milele kwa kuwa aliochoondolewa ni mamlaka ya kuongoza jimbo, alifafanua kuwa hatua hiyo dhidi yake inatokana na uchu wa madaraka, chuki binafsi na wivu wa maendeleo aliyoleta katika jimbo hilo.

Saturday, June 06, 2009

Du! Scandnavia imefilisika!


KISARIKA, MALIMI & MLOLA (ADVOCATES)

SCANDINAVIAN EXPRESS SERVICES LIMITED
(UNDER RECEIVERSHIP)

NOTICE OF APPOINTMENT OF
JOINT RECEIVERS/MANAGERS

A: NOTICE is hereby given to the general public that we, SILVANUI BENEDICT MLOLA and SENI SONGWE MALIMI of KISARIKA, MALIMI & MLOLA (ADVOCATES) were on 26th May, 2009 appointed by NATIONAL BANK OF COMMERCE LIMITED to be Joint Receivers/Managers of all the assets o SCANDINAVIAN EXPRESS SERVICES LIMITED (hereinafter referred to as “the Company”), charged under the Debenture Instrument (hereinafter referred to as “Debenture”) dated l4 May, 2001. Consequent to that, ownership of the Company’s assets now vests in us. We are in the process of taking over physical possession on 3 June, 2009.

B: We further notify the general public and the employees of the Company as follows:-

(a) With effect from the publication of this Notice, no person is allowed to do transactions of whatever nature with the Company except through the Joint Receivers/Managers via the address shown below and through the Company’s address in Dar es Salaam.

(b) This Notice does not terminate any contract of employment between the Company and its employees and all employees of the Company should continue with their duties until notified otherwise.

(c) All creditors of the Company, both secured and unsecured, are required to submit to us particulars of their claims supported fully by documents, so that such claims are received by us not later than 12.00 noon on 3’Pt June, 2009. No further claims will be allowed beyond that date.

(d) All persons, corporate or natural, who hold any property of the Company, must notify us in writing to enable us take possession of such property.

C: This Notice is also a formal announcement that the Company’s assets and business are being offered for sale. An Information Memorandum is under preparation and will be made available in hard and soft form to all interested buyers, together with buying instructions.


SILVANUS BENEDICT MLOLA
AND
SENI SONGWE MALIMI
JOINT RECEIVERSIMANAGERS,
SCANDINAVIAN EXPRESS SERVICES LIMITED
C/O KISARIKA, MALIMI & MLOLA (ADVOCATES)
3RD FLOOR, ELITE CITY BUILDING,
CORNER OF SAMORA AVENUE/MOROGORO ROAD,
P.O. BOX 71394, DAR ES SALAAM.

TEL: +255 22 213361612133619; FAX: +255 22 2133615
Email: info@kmadvocates.com
smIolacäkmadvocates.com & malimlCkmadvocates.com

Shughuli bado pevu Z'bar

Winchi ‘Ndovu’ ya Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam, ikinyanyua meli ya Mv Fatih iliyozama katika bandari ya Zanzibar. Ilifanikiwa kuibinua chini juu, lakini kkazama tena. Inaelekea shughuli bado ni pevu. Picha na Bukuku

Friday, June 05, 2009

Nahodha Meli Iliyozama Alonga

Nahodha wa meli ya MV Fatih iliyozama katika Bandari ya Malindi mjini Zanzibar wiki iliyopita, ameonya kuwa jitihada za kuopoa meli hiyo zisipofanywa kwa umakini, zinawesababisha uharibifu utakaosabaisha uchunguzi wa ajali hiyo kutokwenda sawa.
Akizungumza ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kutokea kwa ajali hiyo, Nahodha Usi Ali Ussi, alisema taarifa kuwa meli hiyo inamomonyoka kutokana na kuchakaa wakati wa kuvutwa si za kweli.
Kwa kina soma hapa

Thursday, June 04, 2009

Obama Ataka Suluhu na Waislamu

President Obama pledged on Thursday to “seek a new beginning between the United States and Muslims around the world,” imploring each to drop their suspicions of one another.

WABUNGE WALIVYOJAA KWENYE BODI ZA MABENKI

Hivi karibuni Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilitangaza nia yake ya kuwaondoa wabunge kwenye bodi za mabenki. Hawa ni baadhi yao:

SANDUKU LA BARUA 9111
DAR ES SALAAM
TANZANIA
27 Februari, 2009

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete,
ameteua wenyeviti wa Bodi za Mashirika na Taasisi chini ya Wizara ya
Fedha na Uchumi kama ifuatavyo: -

1. Bodi ya TIB – Prof. William Lyakurwa
2. Bodi ya Chuo cha Uhasibu Arusha – Bibi Mwanaidi Mtanda
3. Bodi ya NBC Ltd – Dr. Mussa Assad
4. Bodi ya Twiga Bancorp Limited – Dr. Amon Y. Mbelle
5. Bodi ya Benki ya Posta – Dr. Lettice Rutashobya
6. Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania)– Prof.
Hassa M. Mlawa

Uteuzi huu wa wenyeviti ulianza rasmi tarehe 14 Novemba, 2008.
Aidha, Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkulo amewateua
wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi wa Mashirika/Taasisi hizo.

Bodi ya TIB
1. Bw. Haruna Masebu
2. Mhe. Mgana I. Msindai (Mb)
3. Bibi Edwina Lupembe
4. Bw. Bedason Shallanda
5. Bw. Adatus V. Magere

Bodi ya Chuo cha Uhasibu Arusha
1. Bw. Patric Mwangunga
2. Dr. Suleiman Mohamed
3. Bibi Elipina Mlaki
4. Bw. Leonard Mususa
5. Mhe. Estherina Kilasi (Mb
6. Prof. T. A. Satta
7. Dr. Clemence Tesha
8. Mhe. Felix Mrema (Mb)
9. Bw. Mugisha G. Kamugisha

Bodi ya NBC Ltd
1. Ponsiano Nyami (Mb)

Bodi ya Twiga Bancorp Limited
1. Mhe. Siraju Kaboyonga Juma (Mb)
2. Mhe. Abdallah Kigoda (Mb)
3. Mhe. Devota Likolola (Mb)
4. Mhe. Hulda S. Kibacha (Mb)
5. Bibi Mariam A. Nkumbi
6. Bw. Geofrey M. K. Msella

Bodi ya Benki ya Posta
1. Bibi Juliana Lema
2. Bw. Saidi M. Hussein
3. Bw. H. H. Mchangila
4. Bi. Bertha E. Mallogo

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania)
1. Bw. Dennis Muchunguzi
2. Bi. Suzan Mkapa
3. Bibi Maria Kejo
4. Mhe. Lucy Mayenga (Mb)
5. Mhe. Richard Ndassa ( Mb)

Monday, June 01, 2009

Air France yapotea na wabiria 228

PARIS (Reuters) – An Air France plane with 228 people on board went missing on its way from Brazil to Paris on Monday, after hitting strong turbulence, prompting military jets to take off from both sides of the Atlantic to search for it.
Air France said in a statement the plane sent an automatic message reporting an electrical short-circuit at 0214 GMT, roughly 15 minutes after flying into the turbulence.
Senior French minister Jean-Louis Borloo ruled out the possibility of a hijacking of the flight AF 447 from Rio de Janeiro to Paris.
"There was very, very strong turbulence. For now we can't understand what happened," Borloo, the second most senior in the government, said on France Info radio.
"Apparently the possibility of a hijacking has been excluded," Borloo said.
Flight AF 447 has 216 passengers and 12 crew on board. It left Rio de Janeiro on Sunday at 7 p.m. (2200 GMT) and was expected to land at Paris Charles de Gaulle airport on Monday at 11:15 a.m. (0915 GMT).
"It's an awful tragedy. It's dreadful ... Until 10.45 a.m. (0845 GMT) we could still have some hope, but at this stage the kerosene reserves have been more than used up," Borloo added.
The jet's last known location was unclear.
A government source in Brazil said the plane disappeared from Brazilian radars at around 0130 GMT, about three to 3 1/2 hours into its flight. That would mean controllers lost track of the plane while it was closer to Brazil than to France.
Henry Wilson, a Brazilian air force spokesman, said planes had taken off from the island of Fernando de Noronha off Brazil's northeast coast to look for the Air France jet.
Jean-Christophe Ruffin, France's ambassador in the west African country of Senegal, told French iTele that aircraft had also taken off from there to search for the missing Airbus.
The plane was an Airbus 330-200, according to the Paris airports authority website.
RADAR HOLE
Pilots stay in contact with traffic control across the Atlantic by radioing in their position every 20 to 30 minutes. There is no radar cover because radar can only 'see' along a direct line of sight.
"Anything that's the other side of the horizon cannot be seen by radar, so once you've gone 200 or 300 miles off the coast, radar cannot see you any longer," said David Learmount of Flight International.
Air France said relatives of people traveling on board flight AF 447 were being taken care of in a special area of Charles de Gaulle airport.
Part of the terminal was briefly evacuated because of a suspect package but that turned out to be a false alarm.
The last major incident involving an Air France plane came in July 2000 when one of its Concorde supersonic airliners crashes just after taking off from Charles de Gaulle Airport, Paris, bound for New York.
All 109 people on board are killed along with at least four on the ground.
Brazil had two major plane crashes in 2006 and 2007, raising concerns about the safety of air travel in Latin America's largest country.
In July 2007, all 187 people on board and 12 people on the ground died when a TAM airline Airbus A 320 overshot a runway at Sao Paulo's Congonhas airport.
In September 2006, a Gol airline passenger jet crashed in the Amazon jungle after it and a small private plane collided. All 154 people on board died.
(Reporting by Jean-Baptiste Vey, Gerard Bon, Astrid Wendlandt and Tim Hepher in Paris, Pedro Fonseca in Rio; editing by Crispian Balmer and Angus MacSwan)