Wednesday, June 17, 2009

Nukuu ya Leo

"Na nikanukuu usemi wa kiingereza “wrong diagnosis wrong Treatment” na nikatoa ushauri wa kukutaka Mhe. Mwenyekiti uunde Kamati ya wataalam na wazoefu wa shughuli za kiuchaguzi walio ndani ya chama na hata nje mkae na kutengeneza mfumo, mbinu na utaratibu utakaokiwezesha chama kurejesha ari ya kupendeka na wagombea wetu kuchaguliwa na kushinda chaguzi. Ushauri ulioonekana si muhimu kwa sasa na nikapuuzwa.

Mh Mwenyekiti; naomba sasa nimkabidhi barua yangu ya kujiuzulu Mhe. Katibu Mkuu ambapo uamuzi huu unaanza mara baada ya kumkabidhi barua hii. Najua kujiuzulu kwangu kutapelekea kutolewa tafsiri mbali mbali zilizo za kweli na zisizo za kweli.

Najua kujiuzulu kwangu kutawasononesha na kuwakwaza wengi,
Najua kujiuzulu kwangu kutawafaidisha baadhi ya watu ambao sasa watapumua na kujisemea kama wahaya wasemavyo “TWAMWIYUKAO” AU KWA TAFSIRI “BORA
AONDOKE ALIKUWA AMETUKALIA PABAYA”

Mimi kwangu yote ni mazuri tu; tunapaswa tumuachie Mwenyezi Mungu; “Ni Kheri
Nusu shari kuliko shari kamili”

Nilipokutana na Mhe. Katibu Mkuu kwa maongezi wiki mbili baada ya kupumzishwa Unaibu Katibu Mkuu na kuteuliwa Bw. Joran Bashange; nilimwambia Katibu Mkuu kuwa siku ya Jumapili baada ya Uteuzi nilikwenda kanisani na baada ya Ibada niliamua nimuone mchungaji wangu wa kanisa nimweleze yaliyokuwa yamenielemea moyoni mwangu. Mchungaji baada ya kunisikiliza hakuwa na maneno marefu bali alisema;

“Sikiliza Wilfred; Maandiko matakatifu katika Biblia yanasema, kila jambo linalotokea Duniani na kila linapotokea Mungu ana makusudi katika jambo hilo” Na akazidi kuniambia; “SHUKURUNI MUNGU KWA KILA JAMBO”
Maneno hayo ndiyo yanayonipa nguvu na faraja hadi leo na kesho.

Mhe. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mhe.Katibu Mkuu na Waheshimiwa wajumbe wa Baraza Kuu.

NAWASHUKURUNI SANA KWA KUNISIKILIZA"
Wilfred Lwakatare

MCHANGO NA MAONI NILIYOYATOA NDANI YA KIKAO CHA BARAZA KUU LA TAIFA,
CHA TAREHE 09/06/2009
KATIKA AGENDA YA KUTOKANISHA
MUHTASARI WA KIKAO CHA BARAZA KUU CHA TAREHE 28/2/2009.

No comments:

Post a Comment