Wednesday, June 24, 2009

Zitto Atikisa Tena Bunge

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto mchana huu ametingisha kiberiti cha bunge baada ya kukataa 'kufuta' matamshi yake, kuwa majibu aliyotoa Waziri Sumari kwa Mh. Slaa ni ya HOVYOHOVYO..." pamoja na pressure ya wazi toka kwa wabunge wa wakiomba mwongozo wa Mwenyekiti, Zitto aligoma katakata kufuta kauli yake na kudai kwamba wabunge kadhaa wameshaongea kauli za kutatanisha katika bunge hili lakini hakuna hatua zilizochukuliwa..alimalizia kwa kusema "NIPO TAYARI KWA LOLOTE" kabla hajendelea kuchangia mjadala wa bajeti. Bunge linaendelea kuwaka moto baada ya jana kuwa namna hii. Mjadala juu ya suala lake unaendelea kukomaa kwenye forum ya Bidii na wengine wako hapa kwenye Jamii Forum

No comments:

Post a Comment