Saturday, June 13, 2009

CUF Yaja ya 'Operesheni Zinduka'

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)


maazimio ya KIKAO CHA baraza kuu la uongozi la taifa kILICHOFANYIKA OFISI KUU, BUGURUNI, MJINI DAR ES SALAAM TAREHE 8 – 9 Juni, 2009
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lilipokea, kuzijadili na kuzifanyia maamuzi agenda 11 ambazo ni pamoja na Tathmini ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa Nne wa CUF uliofanyika Februari 2009; Tathmini ya Uchaguzi Mdogo katika Jimbo la Busanda, Tanzania Bara na Magogoni, Zanzibar; Programu ya Kuimarisha Chama kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji wa 2009 na Uchaguzi Mkuu wa 2010; Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Chama kwa mwaka 2009; Mapendekezo ya Mchakato wa kupatikana Wagombea nafasi za Uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu; Mapendekezo ya Ratiba ya Uteuzi wa Wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani, Kupitisha Rasimu za Kanuni za Jumuiya ya Vijana wa CUF na Jumuiya ya Wazee wa CUF; na Taarifa ya Hali ya Kisiasa Nchini.

Baada ya mjadala wa kina kuhusiana na agenda hizo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo kuhusiana na masuala hayo:
...14 LIMEAMUA viongozi wa kitaifa wa CUF kuongoza Programu Maalum ya kuuandaa umma wa Watanzania kuleta mabadiliko makubwa ya kisiasa kwa kukiangusha CCM na kuchagua CUF, Chama Mbadala, kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji mwaka 2009 na uchaguzi mkuu wa 2010. Programu hiyo itakayohusisha kazi maalum ya kuwazindua Watanzania juu ya wajibu wao wa kihistoria itakuwa katika operesheni maalum itakayojulikana kama ‘Operesheni Zinduka’. Operesheni hiyo kabambe itakayowafikisha viongozi wa kitaifa wakishirikiana na wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kutoka kila kanda kati ya Kanda tano za Tanzania Bara na Kanda mbili za Zanzibar pamoja na mtandao wa Chama cha CUF wa Viongozi wa Wilaya, Kata na Matawi itaambatana na uzunduzi wa ‘Dira ya Mabadiliko’ (Vision for Change) ambayo ndiyo itakayotumiwa na CUF kama mwongozo wa sera zake kuelekea 2010.

15 Limeagiza Kamati ya Utendaji ya Taifa kusimamia taratibu zote za maandalizi ya CUF kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka huu wa 2009 na taratibu za kuwapata wagombea wa CUF wa nafasi za Ubunge na Udiwani mapema iwezekanavyo ili waanze kazi ya kutekeleza ‘Operesheni Zinduka’ na kuitangaza ‘Dira ya Mabadiliko’ (Vision for Change) katika maeneo yao na hivyo kukiweka CUF katika nafasi nzuri ya ushindi kwa kuongoza mapambano ya kuing’oa CCM madarakani.

No comments:

Post a Comment