Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Prof Haroub Othman (pichani) amefariki dunia alfajiri ya leo katika Kisiwa cha Unguja mjini Zanzibar. Habari zilizoifikia blog hii zinasema Prof Othman alifariki akiwa usingizini na usiku alikuwa katika tamasha la Majahazi lililoanza jana visiwani humo.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala Pema Amina.
Haroub tutamkumbuka kwa makala zake nyingi na uchambuzi kadhaa juu ya mambo yanayoendelea nchini na Duniani, mfano makala yake hii.
Source: Kidevu
No comments:
Post a Comment