Sunday, June 21, 2009

Hii ya 'Je, Tutafika' Imekaaje?

Source: Bidii Forum

Mimi ni mmojawapo wa wapenzi wa kipindi kinachorushwa na Channel 10 kila Jumanne: Je, tutafika? Kipindi hiki huwa kina mada nzuri ingawa mara nyingi ‘animator’ anakiharibu, hasa anapozungumza zaidi kuliko wachangia mada. Anakera sana kwa hili na nadhani halijui hilo!

Pamoja na hoja nzuri zinazojadiliwa na kipindi hiki, linapokuwa ni swala linalohusu dini, ‘animator’ wenyewe anakuwa na ‘bias’ fulani, ambayo nimeona ni vizuri niiweke wazi. Kati ya mijadala inayohusu mambo ya dini nilishasikiliza miwili.

Wa kwanza ulihusu MAHAKAMA YA KADHI na wa pili kijitabu kilichoandaliwa na Chirstian Professionals of Tanzania (CPT) na kupitishwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kuhusu
MPANGO WA KICHUNGAJI KUELEKEA UCHAGUZI UJAO.

Katika mijadala yote miwili niliona kuwa ingawa ‘animator’ anaonekana akipinga udini lakini yeye mwenyewe ndiye aliyejaa huo udini. Katika mada ya kwanza yeye mwenyewe alionyesha upande aliokuwa akiuunga mkono na hivyo alijaribu kuweka ‘leading questions’ kwa wachangiaji ili wachangie kile alichotaka kuhitimisha na kilichohusu: kwa nini maaskofu wanapinga Mahakama ya Kadhi ambayo ni haki ya Waislamu? Kwa uelewa wangu hakuna anayepinga Mahakama ya Kadhi kama itaanzishwa nje ya Katiba kwa vile "Nchi haina dini na mambo yanayohusu imani ni watu wenyewe".

Katika mada ya pili, alikuwa na ‘tactics’ zilizile na ilionekana wazi kuwa anachochea udini zaidi badala ya kuelemisha umma wa Watanzania kuhusu mada yenyewe.

Mfano, katika mada zote mbili ‘selection’ ya wachangiaji haikuonyesha kuwa na uwiano mzuri. Aliwachagua watu wa dini fulani wengi zaidi na wenye uelewa wa dini yao kuliko wale aliowachagua wa dini ya pili na pengine alichagua wale alioona wanamwelekeo anaoutaka.

Kwa mada ya pili pia alifanya hivyohivyo. Dini moja aliwachagua watu 3 wenye uelewa mzuri wa dini yao na nyingine wawili (mmoja mchungaji Lusekelo) na kati ya hao wawili, mmoja hata hakujua kitu gani cha kuchangia. Na hivyo, baada ya mada yenyewe, hitimisho lilielekea upande mmoja aliotaka huyo ‘animator’ umma wa Watanzania ujue ndiyo Maaskofu wa Kanisa Katoliki wana udini na wanahatarisha amani ya nchi yetu kwa kujiingiza kwenye siasa.

Yaani waraka wao unaowataka watu watumie vizuri haki ya kuchagua viongozi waadilifu na wenye uchungu na nchi yao bila kujali dini, itikadi ya chama au kabila la mtu, yeye anaona hiyo siyo kazi ya madhehebu ya dini. Wachangiaji wote siku hiyo (Jumanne, June 16, 2009) walikuwa na mtazamo huo na ndivyo ‘animator’ wa kipindi alivyotaka Watanzania waelewe.

Lakini mimi huwa najiuliza kama huyu ‘animator’ ana nia ya kuelemisha jamii na hana udini, kwa nini huwa hawaaliki, mfano, padri au askofu fulani wa dhehebu husika ili nao waeleze upande wao na kuacha wasikilizaji waamue kulingana na jinsi walivyosikia maelezo yenyewe kuliko yeye kujifanya ndiye anayewaalimua?

Yeye kama ‘seasoned journalist’ nilitegemea awe mtu ‘open’ na asiye na udini lakini kwa mada hizo mbili na pia baada ya kusoma ‘articles’ zake alizoandika kuhusu hizo mada, niligundua kuwa ana ajenda ya siri na ni mtu aliyejaa udini kuliko anavyonekana anaupinga.

Katika mada ya pili alisisitiza zaidi kwa nini Kanisa linajiingiza kwenye siasa na kusema kufanya hivyo ni kuhatarisha amani ya nchi. Wachangiaji wengine nao pia walikuwa na maoni hayohayo.

Of course, inategemea yeye anafahamu nini katika ‘kuchanganya dini na siasa’. Binafsi naamini kuwa mwumini mzuri wa dini atakuwa mwanasiasa mzuri pia na mwanasiasa mzuri akiingia kwenye dini atakuwa mwumini mzuri vilevile. Dini au siasa havimuharibu mtu bali mtu ndiye anayeharibu dini au siasa.

Mtu mwenye imani nzuri ya dini au mtu mwadilifu lazima atafanya pia siasa yenye uadilifu. Madhehebu ya dini, mfano, yanachangia katika maendeleo ya nchi – ikiwa ni pamoja na siasa (kuhamasisha waumini wao wachague viongozi/wanasiasa waadilifu), huduma za jamii – elimu, afya,
etc.

Ukisema madhehebu ya dini yajiondowe kwenye siasa – yaani yajiondoe kwenye maendeleo ambayo ni siasa, elimu, afya, etc una maana kuwa unataka kuwafuga baadhi ya watu/Watanzania kutokuwa Watanzania halisi. Siasa ya Tanzania ni ya watu wote – wawe wachungaji, mashehe, mapadri au maaskofu au watu wa dini nyingine. Kwa maana hii, siasa na dini zinapaswa zifanye kazi moja ya kukamilishana. Ni kama anayekwea ngazi anashika pande zote mbili kwa wakati mmoja – yaani imani yake inaleta changamoto mwenye siasa na siasa inasaidia imani yake kukua vizuri kwa kuinjengea mazingira ya uhuru wa kutosha wa kuamini na kuabudu. Kufanya hivyo siyo sawa na kuchanganya dini na siasa bali ni
kuwajibika kwa imani/mwumini au kiongozi wa dini.

Kitu kinachokatazwa kufanyika katika madhehebu ya dini ni kuwa na viongozi wa kiroho wanaoshabikia chama kimoja dhidi ya kingine kwa sababu kufanya hivyo kutaleta msukosuko kati ya waumini na wananchi kwa ujumla kwa vile katika dini fulani kuna waumini wa vyama mbalimbali.

Na dini au dhehebu likishabikia chama kimoja, hapo inakuwa si sahihi. Kwa vyovyote vile kutakuwa na mwingiliano wa kimasilahi na vurugu. Lakini kusema usichanganye dini na siasa – kwa maana ya kusema usichangie kuboresha sisasa ya nchi – yaani maendeleo ya nchi, hapo naona ni kitu kisichoeleweka kabisa.

Dini zinapaswa kukamilisha sehemu ambazo serikali inashindwa au inafanya kwa kulegalega. Kwa sababu huwezi kusema mchungaji, padri, shehe au askofu achangie maendeleo ya nchi na kumkataza asichangie kuboresha siasa ya nchi yake. Kufanya hivyo ni kumfuga. Sijui ‘huyu seasoned journalist’ anaelewa nini kuhusu siasa na wanasiasa.

Kwa vile kila anayezaliwa ni mwanasiasa, inawezekanaje tuwe na baadhi ya watu wasioruhusiwa kuchangia kuboresha siasa/maendeleo ya nchi yetu au hoja ni kwa vile Kanisa linahamasisha waumini na wananchi kwa ujumla kuhusu kutumia haki yao ya kikatiba ya kushiriki katika mambo yote yanayohusu maendeleo ya nchi na maendeleo yao wenyewe?

‘Civic education’ katika Kanisa katoliki haikuanza leo au jana. Ni kitu cha miaka na miaka na ‘animator’ wa “Je tutafika?” anaona ‘civic education’ haipaswi kufanyika kanisani. Kanisa Katoliki linaamini kuwa imani lazima inonekane katika matendo. Na kuwa na mchakato wa kuwapa waumini uelewa mzuri kuhusu haki zao za msingi sidhani kama ni kazi ya serikali tu. Hii ni kazi ya kila mtu, kila dhehebu la dini na taasisi mbalimbali.

3 comments:

Anonymous said...

Acha uhanisi wewee, nyie wakristo udini umewakaa sana, mnaupiga vita sana uislam badala ya kushughulikia mambo yenu...! Msione tumenyamaza mkadhani sisi mambumbumbu siku tukiamuwa mtajuwa kwamba sisi kufa kwa ajili ya Allah ni bora kuliko kuishi kwa kuwafurahisha nyinyi makafiri. Kikwete akimpa cheo muislam mmoja tu, mnapiga kelelee ooh udini, mbuzi wakubwa nyie, lakini akimpa nafasi mgalatia mwenzio mnakaa kimyaa, hamsemi ni mdini! Na hii mada ya kadhi ni mambo ya waislam nyie wagalatia kinawauma nini? Kuma nina zenu...dawa yenu iko jikoni!
Enough is enough!

Anonymous said...

Ni kweli kabisa alichosema mtoa mada, huyo mtangazaji wa hicho kipindi ana udini na ni kwa muda mrefu sana. achana na mifano hiyo miwili, kuna mifano mingi sana tunayoweza kuisema hapa na tusiimalize.hata wakati wa kujadili mambo ya palestina na israel, yeye atawatafuta watu fulani ambao daima mawazo yao yanaongozwa na dini na wala sio utashi wa hari ilivyo.

Hata katika maswali yake kwa wajadili mada atahakikisha yanalenga kule yeye anakoamini kuliko hari harisi.naungana na mtoa mada kuwa yeye anahusika sana kubomoa watanzania katika udini kuliko kujenga udugu na mshikamano wetu.hivyo nalazimika kuamini kuwa yeye ni mtu mwenye itikadi kali kwa dini yake.

Anonymous said...

Wewe mtoa maoni wa kwanza hapo juu kwa nini unawatukana wenzio bila sababu? kwenye mada ya mlengwa hakuzungumzia dini fulani kwa ujumla. bali ni mtu mmoja na tabia yake ya udini! iweje wewe utukane watu wote wa dini fulani? jalibu kuwa mstaarabu na muungwana, japo hatuonani kwa macho, lakini siyo sababu ya kutoa maoni na matusi kwa watu wengine.

Post a Comment