Spika wa Bunge, Samuel Sitta amesema anachunguza kauli ya Zitto Kabwe na kitendo chake cha kukataa uamuzi wa meza, uliomtaka afute kauli yake kuwa Waziri amesema mambo ya hovyo hovyo.
Tayari Zitto kashasema yuko tayari kwa lolote. Duru za karibu na Zitto zinasema, kama angetimuliwa bungeni, angwenda moja kwa moja Biharamulo kwenye kampeni za uchaguzi, nyingine zinasema ana safari ya Nairobi.
Hata hivyo, Spika amesema atatoa uamuzi huo wiki moja baadaye, kipoindi ambacho siku za kumaliza kampeni zitakuwa zimekaribia, kwa kuwa uchaguzi mdogo ni Julai 5.
1 comment:
Siku zote zitto kabwe ndiye kwa macho ya spika sita, mwenye kufanya makosa bungeni. inaonekana spika ameamua kula sahani moja na zitto, maana kama ni suala la lugha chafu mimi naona wabunge wa ccm ndio wametoa lugha nzito na chafu sana, lakini machoni mwa spika anaonekana kabwe tu.
Hivi mbunge kuwaita wenzake mbwa!!! ama mmoja kuomba mungu ili atoe laana kwa mawaziri na wakuu wa serikali ni sahihi? hivi wewe baba spika zitto kakukosea nini hasa? kuwa fair bwana.
Post a Comment