Dk Slaa amkabidhi Lwakatare kadi ya Chadema
Frederick Katulanda, Bukoba
ALIYEKUWA naibu katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilfred Lwakatare jana amehama rasmi chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa jana alimkabidhi rasmi kadi Lwakatare katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Uhuru mjini Bukoba.
Akizungumza na wananchi kabla ya kukabidhiwa kadi ya Chadema, Lwakatare alisema uamuzi wake wa kukihama CUF umetokana na ushauri wananchi wa jimbo hilo Lwakatare aliyevalia mavazi rasmi ya Chadema, alisema baadhi ya watu wanadhani uamuzi wake huo unatokana na fedha lakini mawazo hayo ni potofu kwani yeye ni adui wa rushwa na kamwe hatohamia chama chochote kwa kupewa fedha.
“Nimejiunga Chadema siyo kwa sababu ya fedha, maana kuna watu wanasema nimelipwa milioni 80. Jamani sijalipwa hata shilingi moja, ninahama CUF kwa sababu ya kutaka maendeleo ya watu, siingii katika chama kwa sababu ya kutaka ukuu wa mkoa au udiwani bali kwa sababu nataka kuwatumikia wananchi” alieleza.
No comments:
Post a Comment