Friday, June 26, 2009

Zombe Atafutiwa Kifungu Chake

Mawakili wa serikali katika kesi ya akina Zombe wamependekeza adhabu mbadala kwa watuhumiwa wawili, akiwamo mshtakiwa wa kwanza, Abdallah Zombe, bila shaka baada ya kuhisi kuwa wanaweza kuchomoka katika Hatia ya Mauaji ya Kukusudia (Murder)
Kiongozi wa Jopo la mawakili hao, Revocatus Mtaki katika kuhakikisha kuwa washitakiwa wote hawaponi katika ghadhabu ya mkono wa sheria, aliiomba mahakama iwatie hatiani kwa kosa mbadala Zombe na mshtakiwa wa 13, Koplo Festus Gwabisaba, ikiwa mahakama itaridhika kuwa hawahusiki kwa kuwa kwa ushahidi ulioko mahakamani wao hawakwenda katika eneo la mauaji katika Msitu wa Pande.
“Kama mahakama itaona kuwa mshtakiwa wa kwanza (Zombe) na wa 13 (Gwabisabi) hawakushiriki katika mauaji kwa kuwa kwa ushahidi ulioko mahakamani hawakwenda Pande, basi iwatie hatiani kwa kosa Accessory after the facts (mshiriki baada ya kosa) chini ya kifungu cha 213,387(i) na 388 cha Penal Code,” alidai Mtaki. Habari Kamili

No comments:

Post a Comment