Tuesday, January 29, 2008

Kusanya ushahidi

Umeanzishwa mtandao maalum kwa ajili ya kupata ushahidi wa matukio ya kutisha yanayotokea Kenya. Fungua ushahidi.com.
Maelezo yake haya hapa: A new website, http://www.ushahidi.com/ has been recently set up for witnesses in Kenya to post their stories and upload photos of what is happening where they are. No press interviews, no tapes, no notepads - just what the mwananchi has witnessed. Things that will us and not the press. There's a phone mumber set up as well to allow for text messaging - +44 762 480 2635. A local number will be added soon. Please visit ushahidi for more details and be sure to tell your friends and family in Kenya about it.Edited to add: Local Kenyan number - +254 711 862 149
(Picha Raila Odinga akimbembeleza mke wa Mbunge wa ODM, Melitus Were aliyeuawa na wakora usiku wa kuamkia leo).

Sunday, January 27, 2008

Ulevi Mbaya


Ukilewa pombe ukiwa Ilala Dar itabidi ukubali lolote kama jamaa huyu aliyefungwa kamba na mambo mengine...(Picha na Edwin Mjwahuzi

Mhariri Apata Nondo

Mhariri wa Mtanzania, Deodatus Balile, akiwa ameshika cheti chake cha Shahada ya Uzamili baada ya kula nondozz za Uongozi wa Biashara (MSc Business Management) nje ya Ukumbi wa Middleton katika Chuo Kikuu cha Hull nchini Uingereza. Sherehe za kuhitimu zilifanyika Alhamisi ya Januari 24, 2008. Picha na Ansbert Ngurumo

Mkuki Kwa Nguruwe...

Huko Kenya mambo yamefikia hatua mbaya kama hii. Kijana akiwa amechomwa mkuki katika mapigano yaliyoibuka baada ya uchaguzi, akisubiri huduma ya kuutoa hospitalini. Mungu msaidie

Thursday, January 24, 2008

Raila, Kibaki Wakutana

Unaweza kuita Nuru ya Matumaini. Ni habari iliyoleta mvuto kimataifa. Associated Press waliandika hivi. Magazeti ya Kenya hayakubaki nyuma, katika article yake ya awali Gazeti la Daily Nation liliweka hivi. Na hapa utalisoma Standard

Wednesday, January 23, 2008

Mafisadi Duniani

Mdau mmoja katoa mchango wake kuhusu 'Mafisadi BoT na CCM'. Nimeamua kuuweka hadharani (na mfano wa Freetown-Kushoto kisiwani kwa mafisadi na kulia uwanja wa fisi kwa kapuku) ili uone mwenyewe anachomaanisha.

Kumbuka kaka wataalamu wa dunia hii ni hatari. Utadhani kuwa ubadhilifu na ufisadi wote uko hapo tza tu, lakini ukweli ni kwamba umeenea kote. Waenezao haya ni wachache tu duniani. Na haya yalianza zamani.
Ingia website hizi uone.

http://judicial-inc.biz/slave_traders_.htm,
http://judicial-inc.biz/b.lood_diamonds.htm,
http://judicial-inc.biz/J_oran_va_der_sloot_supplement.htm,
http://judicial-inc.biz/thersea_heinz_kerry_bio.htm,
http://judicial-inc.biz/1.osephardim_of_curacao.htm,
http://judicial-inc.biz/j_history_caribbean_jews.htm,
http://www.blacksandjews.com/Jews.of.Black.Holocaust.ag.html,
http://sunray22b.net/slavery.htm,
www.jewwatch.com, www.erichufschmid.net, www.iamthewitness.com, www.prothink.org.

KIGOMA: Usafiri Noma

Usiombe kufika Kigoma ukakuta hali iko hivi. Unaweza kumaliza hata wiki njiani. Mungu wanusuru watani zangu. Ndekaaaayeeee! Wabishi hao!

CCM Matatani!

Raia Mwema toleo la leo lina mambo mazito kuhusu CCM, kile chama kikongwe, na jinsi kilivyoshiriki katika ufisadi wa BoT. Sina la Kuongeza Soma Mwenyewe Raia Mwema

Tuesday, January 22, 2008

Kichwa kimechoka? Pata picha za namna hii

Paka akiwa usingizini

si lazima kitanda kiwe na chaga

Huyu anacheka nini? mbona mwenzake haoni cha kumchekesha?


Mtoto huyu kiboko, anazomea dude baya hivi!


Hata sina maelezo ya kutosha







Saturday, January 19, 2008

Uwanja wa Fisi

imepata kipande hiki cha ardhi ya Manzese na jinsi kinavyoonyesha namna majumbe yalivyoshonana. Mliombali na Dar bila shaka mnayakumbuka maeneo haya, likiwemo eneo maarufu la Uwanja wa Fisi

Thursday, January 17, 2008

Fununu: Wataka Kumuua Ballali?

Mtandao wa Jambo Forum umechapisha taarifa hii yenye fununu ikielezea jinsi mwandishi wake alivyoongea na Daud Ballali nchini Marekani. Fuatana naye...


WanaJF,

Nianze kwanza kwa kuwakumbusha jinsi ambavyo JF ilifanikiwa sana kwa kuwekwa barua ya Balali ya kujiuzulu hapa JF na story hiyo ikaenea kwenye vyombo vya habari Tanzania kiasi cha kufikia kina Saliva na wenzake kuchanganyikiwa na kuanza kukana hizo taarifa, habari nyingine zinazofikia vyanzo vya habari vya JF ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Balali akafanya interview na kipindi maarufu cha uchunguzi marekani cha 60 minutes.

Ikumbukwe pia kuwa mimi binafsi nimekuwa anti-Balali mkuu katika jamvi hili na mara kwa mara nimekuwa namuombea hadharani aende hell maana ndiko wezi na mafisadi wanastahili. Pamoja na haya yote, ujio wa afisa usalama mkuu wa serikali ya Kikwete RO hapa marekani kumjulia hali Balali na yale aliyosema baada ya kuonana naye vilinifanya nibadili uamuzi wangu kwa muda na kucheza the same game inayochezwa Tanzania.

Nilijiuliza sana maswali kuwa kwa nini RO asifurahie kuendelea vyema kwa Balali na aonekane kushangaa kumuona akipata nafuu kwa haraka? Kwa nini serikali ya Kikwete ilikataa kujiuzulu kwa Balali na baada ya muda mfupi Kikwete akatangaza kwa misifa mingi kuwa amemfuta kazi Balali? Haya yote yalipelekea nimtafute Balali ili nijue kulikoni.

Kwa vile kwa sasa hairuhusiwi kusema kama Balali anaendeleaje kiafya na yuko wapi hapa US, naomba usiniulize maswali kuwa nilikutana naye wapi maana sitakujibu. Yafuatayo ni maneno ya Balali mwenyewe kuhusu ugonjwa wake na kwa nini alikimbilia hapa Marekani:

1. Balali anadai kuwa aliitwa Dodoma bila sababu maalumu
2. Anashangaa kuwa aliyoulizwa Dodoma angeulizwa hata Dar
3. Anashangaa kwa nini alisindikizwa na mkubwa toka Dodoma
4. Alishangaa sana usiri uliondelea alipokuwa Dodoma
5. Anakumbuka kuwa alikunywa na kula Dodoma na kwenye ndege
6. Anadai kuwa matatizo yake yalianza haraka baada ya Dodoma
7. Mengine ni mambo ya kitabibu......

Binafsi simuonei huruma sana Balali lakini ningefurahi kuona akitoa story yake kwenye 60 minutes. Alichokifanya Balali ni kibaya na kinastahili adhabu kubwa lakini sio ya kujaribu kutoa maisha yake ili asitoe siri ya wizi mkubwa uliofanywa wakati wa uchaguzi wa ccm na baadaye taifa mwaka 2005.

Balali anastory kubwa sana ya kutoa na ninafanya juhudi zote kwa ushirikiano na baadhi ya watu ili story yake isikiwe na watanzania woooote.

Swali kubwa ni kuwa, kwa nini kuna watu wangependa sana kumuona Balali akiwa kwenye jeneza? Nani anafaidika sana na kifo cha mtu huyu (nitamwita fisadi akipona vizuri) ?

Huyu Naye Mmhh!

Msanifu wa maarufu wa kurasa na masuala mengine ya graphics, Barnabas Mkwayu ameamua kutangaza kazi zake kupitia mtandao. Kweli anatisha na kazi si za mchezo kama unavyoziona hapa chini. Pitia kwake HAPA uone mengi zaidi.



Ballali Kakimbilia Malta?

Hivi ndivyo visiwa vya Malta anaposemekana kukimbilia Daud Ballali, ikiwa ni muda mfupi kabla ya kutimuliwa Marekani.

Sumu Yaondolewa Korogwe


Hatimaye sumu aina ya DDT iliyokuwa imetelekezwa wilayani Korogwe kwa miaka zaidi ya 30 imeondolewa na kwenda kutupwa 'mahali' ambapo itaharibiwa bila athali za kimazingira

Wednesday, January 16, 2008

Kubenea Atoka India


Mapokezi ya Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti dogo lenye mdomo mpana 'Mwanahalisi', Saed Kubenea aliporejea leo kutoka India alipoenda kwa matibabu zaidi baada ya kumwagiwa kimiminika yaweza kuwa 'tindikali', alikali, gongo, alicohol au kemikali nyingine. Akiongea na Waandishi wa habari, baadhi wakishangaa uso (macho) wake

Hapa akiwapungia waliokwenda kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere


Hata Hii Hujaona!

Mitindo ipo mingi ukitaka. Hata huu unatisha lakini ni mtindo murua kabisa.

Maandamano Tena!


Police have broken demonstrations in Mombasa, Kisumu and Migori as various other towns across the country remained tense following protest rallies called by the Orange Democratic Movement.

Wazanzibari na Vespa


Ukiingia mitaani Unguja, huwezi kumaliza dakika moja bila kuona pikipiki maarufu kama 'Vespa' kama walizopanda jamaa hawa wakati wa sherehe za 'Mapinduzi Halali' ya mwaka 1964

Tuesday, January 15, 2008

ODM Kidedea, KIbaki Mhh!

Uchaguzi wa Spika Bunge la Kenya umemalizika na Kenneth Marende, mgombe wa Chama cha ODM cha Raila Odinga ameibuka kidedea dhidi ya Francis Ole Kaparo wa PNU. Kaparo ndiye alikuwa Spika wa muda mrefu kabla ya uchaguzi Mkuu uliozaa vurugu Kenya. Marende alipata kura 105 wakati Kaparo aliibuka na kura 101. Uchaguzi huo ulirudiwa mara tatu, baada ya mara mbili kukosekana mshindi wa kuibuka na theluthi mbili kama sheria inavyotaka, hivyo kulazimika kutumia mtindo wa mwenye nyingi achukue (simple majority) (Pichani wabunge wa ODM wakisubiri matokeo hayo kwa hamu na bashasha)

Kenya: Uchaguzi wa Spika


Speaker election: Round one counting on
By NATION ReporterLast updated: 25 minutes ago
Kenya’s new MPs are at Parliament Buildings all set to elect of new Speaker in the first major test of strength between the Government and the Opposition since the elections two weeks ago.
A total of 207 MPs-elect are in Parliament ready to elect the speaker of the National Assembly.
- Soon after the MPs-elect are called to order and prayers are said, Ugenya MP-elect James Orengo seeks clarification from the Clerk Samuel Ndindiri on the basis of voting through secret ballot as that was not provided for in the standing orders. Mr Ndindiri answers that the orders talk of ‘a ballot’.
- Voting begins and ODM MPs-elect mark their ballots and show them to their colleagues. This draws several interventions from the Government side who argue that it is against the procedures. The opposition side answers that it is their choice and that there is no provision in law against them showing each other marked ballots.
- Attorney General Amos Wako says that while it may not be explicit in the rules that voting be by secret ballot, they can borrow from the House of Commons where the practice is on.
- The Clerk asks that the ballots already in the box be removed and the voting to start all over again. The ballot box is moved to the dispatch area.

Thursday, January 10, 2008

Happy New Year 1429

Leo ni Mwaka Mpya wa Kiislamu 1429. Ninawatakieni wasomaji wangu Heri ya Mwaka Mpya.

Taarifa Rasmi Iliyombana Balali

IKULU, DAR ES SALAAM
09 Januari 2008



TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI WA HESABU KATIKA AKAUNTI YA MALIPO YA MADENI YA NJE (EXTERNAL PAYMENT ARREARS ACCOUNT – EPA) ILIYOKO BENKI KUU YA TANZANIA

Nafurahi kuwaarifu kuwa, kazi ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka wa fedha 2005/06 za Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje yaani External Payment Arrears (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania imekamilika. Kazi hiyo ilifanywa na Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...Endelea

Wednesday, January 09, 2008

Breaking Newssssssss

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Daud Balali ametemeshwa kibarua leo baada ya kubainika ubadhirifu wa Shilingi Bilioni 123 katika akaunti ya madeni ya nje. Bravo Chadema. Bravo Dk Slaa. Bravo JK

Tuesday, January 08, 2008

Makubwa: KIbaki atangaza Baraza la Mawaziri

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amewashangaza wengi jioni hii kwa kutangaza sehemu ya Baraza la Mawaziri wakati juhudi za kimataifa za kuwapatanisha na wapinzani wake zikiendelea. Hata hivyo, tayari mpinzani wake mkuu, Raila Odonga ameshakataa kushiriki katika serikali yake ya umoja wa kitaifa.

Endelea:

President-Mwai Kibaki
Vice President-Kalonzo Musyoka
1. Internal Security – Prof George Saitoti
2. Defence – Yusuf Hajji
3. Special Programmes – Naomi Shaban
4. Public Service - Asman Kamama
5. Finance – Amos Kimunya
6. Education – Prof Sam Ongeri
7. Foreign Affairs – Moses Wetangula
8. Local Government – Uhuru Kenyatta
9. Information and Communications – Samuel Poghisio
10. Water and Irrigation – John Munyes
11. Energy – Kiraitu Murungi
12. Roads and Public Works – John Michuki
13. Science and Technology – Noah Wekesa
14. Justice and Constitutional Affairs – Martha Karua
15. East Africa Cooperation – Dr Wilfred Machage
16. Transport – Chirau Ali Mwakwere

Unaweza kusoma mwenyewe

Kegera zaidi

Fundi wa kuchoga ngoma akiwa kazini mjini
Bukoba
Hapa muuzaji wa ngoma akiwa katika biashara zake.

Sunday, January 06, 2008

Kagera iko vile vile



Mdau Susuma Susuma hivi karibuni alitembelea Mkoa wa Kagera. Kwa raha zake karudi na mafoto kibao. Nimeona si vibaya kukuwekea hapa.

Ngoma Bado Nzito Kenya

Mambo bado mazito Kenya. Hakuna makubaliano yoyote yaliyoafikiwa hadi sasa KIBAKI ameshikilia lake na RAILA hatakai kugeuka jiwe la chumvi. Wasiwasi mkubwa sasa ni kama Rais Mwai Kibaki atatangaza BARAZA LA MAWAZIRI kabla moto haujazimika. Viongozi wa dini waendelea kulilia AMANI ya Kenya. Hapa Tanzania Juhudi za Wampinzani kuandamana kumpinga Kibaki zimegonga mwamba abaada ya POLISI wenye 'ngoma' zao kumwaga mitaani Dar kwa idadi kubwa iliyozidi ile ya waandamanaji.

Saturday, January 05, 2008

Kama Noma iwe Noma. Hapa Wakenya walioathirika na vurugu wakijipanga kupatiwa chakula kilichotolewa msaada na Red Cross. Red Cross imeomba Sh1 bilioni za kenya kunusuru watu 500,000 walioathirika.

Wapinzani Dar Waitamani Kenya

Mambo kama haya tuliyaona Rwanda mwaka 1994. Sasa yako Kenya. Eeee Mungu Tusaidia

Mabomu. mabomu. mabomu. Hadi lini? Hali kama hii inaweza kujitokeza Dar leo kufuatia maandamano ya wapinzani kupinga serikali ya Kibaki, wakati polisi wamezuia maandamano hao. Taarifa za saa hizi zinasema kwa polisi walioko tayari kwa mapambano wamejikusanya wakisubiri wapinzani wakaidi. Soma zaidi hapa

Friday, January 04, 2008

Mambo Zaidi Kenya

Ngoja tusali, Allah atatusaidia
Chukua kitu hicho!

Kenya Kama Kawa

Watoto wa Kenya wamekata tamaa, matumaini ya amani yametoweka


Kujisalimisha chini ya ulinzi


' Bora niondoke na bati' huo ndio uamuzi wa mkazi wa Kibera, Nairobi baada ya vibanda vyote kuteketezwa kwa moto


"Mizigo hii tutaipeleka wapi? Ngoja tusikilize redio tujue wapi hakuna vurugu ndio tuelekee'

Chatu Mla Mayai Apatikana


Baada ya Vurugu kemkem za Kenya, si vibaya kupata akiburudisho hiki cha Chatu mla mayai kumeza mipira ya Golf. Soma mwenyewe, utanisaidia kutafsiri.


Big Mis-Snake! Python Swallows Golf Balls
A snake hoping to feast on four chicken eggs bit off more than it could chew after it swallowed four golf balls instead. Mis-snaken identity over ballsAn Australian couple had placed the golf balls in their chicken coop at Nobbys Creek in New South Wales to encourage their hen to nest.
When they checked the chicken coop they found the balls had gone missing - and discovered a lumpy carpet python nearby. They took the 80cm (32") snake, which is non-venomous, to the nearby Currumbin Wildlife Sanctuary.
A python in Australia which ate four golf balls, thinking they were chicken eggs, has had its life saved by surgery. The balls had been placed in the coop to enourage the hens to nest.

Tutu Aanza Mpango wa Amani


Askofu Desmond Tutu akizungumza Na Kiongozi wa ODM, Raila Odinga wakati wa mazungumzo yao ya kutatua mgogoro wa kisiasa Kenya.

Wednesday, January 02, 2008

Na Huu Pia Mwaka wa Shetani?

Miaka kadhaa iliuyopita, Kibwetere aliwachoma waumini wake huko Uganda na yeye hajawahi kuonekana. Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari mamia ya waumini waliuawa kanisani. Jana huko Eldoret, Kenya zaidi ya watu 30 walichomwa moto na kuuawa kanisani katika vurugu zinazofuatia kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi.IKO HAPA na HAPA


Elizabeth Wangoi wails near the Kenya Assemblies of God church in Kiambaa, Eldoret, where more than 35 women and children were burnt beyond recognition. The women and children sought refuge there after their homes were burnt in violence over disputed presidential poll results. Photo/JARED NYATAYA