Tuesday, January 15, 2008

ODM Kidedea, KIbaki Mhh!

Uchaguzi wa Spika Bunge la Kenya umemalizika na Kenneth Marende, mgombe wa Chama cha ODM cha Raila Odinga ameibuka kidedea dhidi ya Francis Ole Kaparo wa PNU. Kaparo ndiye alikuwa Spika wa muda mrefu kabla ya uchaguzi Mkuu uliozaa vurugu Kenya. Marende alipata kura 105 wakati Kaparo aliibuka na kura 101. Uchaguzi huo ulirudiwa mara tatu, baada ya mara mbili kukosekana mshindi wa kuibuka na theluthi mbili kama sheria inavyotaka, hivyo kulazimika kutumia mtindo wa mwenye nyingi achukue (simple majority) (Pichani wabunge wa ODM wakisubiri matokeo hayo kwa hamu na bashasha)

No comments:

Post a Comment