Sunday, January 06, 2008

Ngoma Bado Nzito Kenya

Mambo bado mazito Kenya. Hakuna makubaliano yoyote yaliyoafikiwa hadi sasa KIBAKI ameshikilia lake na RAILA hatakai kugeuka jiwe la chumvi. Wasiwasi mkubwa sasa ni kama Rais Mwai Kibaki atatangaza BARAZA LA MAWAZIRI kabla moto haujazimika. Viongozi wa dini waendelea kulilia AMANI ya Kenya. Hapa Tanzania Juhudi za Wampinzani kuandamana kumpinga Kibaki zimegonga mwamba abaada ya POLISI wenye 'ngoma' zao kumwaga mitaani Dar kwa idadi kubwa iliyozidi ile ya waandamanaji.

No comments:

Post a Comment