Thursday, January 17, 2008

Fununu: Wataka Kumuua Ballali?

Mtandao wa Jambo Forum umechapisha taarifa hii yenye fununu ikielezea jinsi mwandishi wake alivyoongea na Daud Ballali nchini Marekani. Fuatana naye...


WanaJF,

Nianze kwanza kwa kuwakumbusha jinsi ambavyo JF ilifanikiwa sana kwa kuwekwa barua ya Balali ya kujiuzulu hapa JF na story hiyo ikaenea kwenye vyombo vya habari Tanzania kiasi cha kufikia kina Saliva na wenzake kuchanganyikiwa na kuanza kukana hizo taarifa, habari nyingine zinazofikia vyanzo vya habari vya JF ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Balali akafanya interview na kipindi maarufu cha uchunguzi marekani cha 60 minutes.

Ikumbukwe pia kuwa mimi binafsi nimekuwa anti-Balali mkuu katika jamvi hili na mara kwa mara nimekuwa namuombea hadharani aende hell maana ndiko wezi na mafisadi wanastahili. Pamoja na haya yote, ujio wa afisa usalama mkuu wa serikali ya Kikwete RO hapa marekani kumjulia hali Balali na yale aliyosema baada ya kuonana naye vilinifanya nibadili uamuzi wangu kwa muda na kucheza the same game inayochezwa Tanzania.

Nilijiuliza sana maswali kuwa kwa nini RO asifurahie kuendelea vyema kwa Balali na aonekane kushangaa kumuona akipata nafuu kwa haraka? Kwa nini serikali ya Kikwete ilikataa kujiuzulu kwa Balali na baada ya muda mfupi Kikwete akatangaza kwa misifa mingi kuwa amemfuta kazi Balali? Haya yote yalipelekea nimtafute Balali ili nijue kulikoni.

Kwa vile kwa sasa hairuhusiwi kusema kama Balali anaendeleaje kiafya na yuko wapi hapa US, naomba usiniulize maswali kuwa nilikutana naye wapi maana sitakujibu. Yafuatayo ni maneno ya Balali mwenyewe kuhusu ugonjwa wake na kwa nini alikimbilia hapa Marekani:

1. Balali anadai kuwa aliitwa Dodoma bila sababu maalumu
2. Anashangaa kuwa aliyoulizwa Dodoma angeulizwa hata Dar
3. Anashangaa kwa nini alisindikizwa na mkubwa toka Dodoma
4. Alishangaa sana usiri uliondelea alipokuwa Dodoma
5. Anakumbuka kuwa alikunywa na kula Dodoma na kwenye ndege
6. Anadai kuwa matatizo yake yalianza haraka baada ya Dodoma
7. Mengine ni mambo ya kitabibu......

Binafsi simuonei huruma sana Balali lakini ningefurahi kuona akitoa story yake kwenye 60 minutes. Alichokifanya Balali ni kibaya na kinastahili adhabu kubwa lakini sio ya kujaribu kutoa maisha yake ili asitoe siri ya wizi mkubwa uliofanywa wakati wa uchaguzi wa ccm na baadaye taifa mwaka 2005.

Balali anastory kubwa sana ya kutoa na ninafanya juhudi zote kwa ushirikiano na baadhi ya watu ili story yake isikiwe na watanzania woooote.

Swali kubwa ni kuwa, kwa nini kuna watu wangependa sana kumuona Balali akiwa kwenye jeneza? Nani anafaidika sana na kifo cha mtu huyu (nitamwita fisadi akipona vizuri) ?

No comments:

Post a Comment