Friday, January 13, 2006

Poleni, lakini shetani apigwe kwa tahadhari

Taarifa kwamba mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu waliokwenda Mji Mtakatifu wa Mecca, Saudia wamekufa wakati wa kumpiga mawe shetani zinasikitisha. Angalia jamani, watu 345 wamekufa wakiwemo watanzania wawili, na kila mwaka wanakufa wengi vile vile, hivi serikali ya Saudia, na Waislamu wote ulimwenguni, hawaoni kuwa hilo ni tatizo? Kwa nini hawaweki utaratibu mzuri, wa kudumu wa kumpiga mawe shetani? Hivi shetani yupo Mecca pake yake? Kwanini wasiandae utaratibu wa kumpiga shetani huko katika nchi zao badala ya kusongamana pale Mecca? Au na shetani naye amejiandaa kukabiliana nao? TAFAKARI!

10 comments:

Ndesanjo Macha said...

Shetani tunaye ndani na nafsi zetu. Aliyesema kuwa unahitaji kutafuta fedha za kununua tiketi kisha usafiri maili maelfu kumpiga jiwe shetani wakati yuko nafsini mwako. Hili ndio tatizo la dini. Kwenye dini hutakiwa kuhoji. Kama kitu kimeandikwa, fuata!

kimanzichana said...

Tatizo ni kutokuwepo kwa usalama. Hata kwetu hapa Kimanzichana haturuhusu msongamano wa watu.

Jeff Msangi said...

Miruko,
Ulilopendekeza hapa ni suala la maana sana na nadhani linahitaji nguvu na muitikio wa kimataifa.Shetani hayuko Mecca peke yake.

Martha Mtangoo said...

Kwa upande wangu mimi ningesema kuwa kama mahali ambapo kulitakiwa shetani apigwe mawe ni Jamaica na Marekani kati mji mmoja hapo ingedaiwa anapigwa mawe ningekubali, kwa maana kuwa shetani maeneo hayo nahisi ndiko anakoishi na nafkiri katika nchi zingine huwa anaenda likizo kupumzika tu, sasa nawashangaa hawa ndugu zangu ambao wanampiga shetani Maka mji mtakatifu unajua wananichanganya sana, mji mtakatifu halafu anapigwa shetani inakuwaje hapa!!!!!!!!!!!!! labda ndugu yangu Baba saidi angetusaidia kwa hili.

Jeff Msangi said...

Martha kwanini umechagua Jamaica?Ningependa kujua.Nahisi naelewa kwanini umeitaja Marekani.Nisaidie tafdhali.

Ndesanjo Macha said...

Hata mimi nina hamu ya kujua kwanini Jamaika imechaguliwa.

Martha Mtangoo said...

Ni hivi nimeichagua Jamaica kwa vigezo hivi, mara nyingi sana huwa napenda kuangalia katika tv miziki inaitwa Danc hall ambayo inapigwa na akina Sean Paul na akina Wyne Wonder kwa jinsi wale akina dada ambao huwa wanacheza shoo katika miziki ya aina hiyo, mavazi yao yanathibitishakuwa shetani anaishi huko, kwa maana huwa wamevaa vichupi tu na visidiria inaonyesha ni jinsi gani shetani alivyo na makazi ya kudumu huko maana nchi kama tanzania mambo kama hayo ni mashikolo mageni na wala hatujayazoea, ndio maana nimeitaja kwa maana inashabihiana na Marekani, huku kwetu shetani huwa anakuja likizo tu lakini haishi huko.

Mija Shija Sayi said...

Kuna wakati hata kuvaa suruali kwa wakina dada walokole ilikuwa ni kumkubali shetani.

msangimdogo said...

Dada yangu Martha, ameniomba nimpe ufafanuzi kuhusu Kupiogwa mawe kwa Shetani katika Mji Mtakatifu. Na kwa hakika nadhani ana hoja ya msingi kabisa hapo, kwa maana ni jambo la kushangaza kidogo na ambalo hata hivyo, kwa bahati mbaya sana kwangu mimi limekuwa katika ile ile hali aliyoizungumzia Bw. Macha hapo juu, kuwa tatizo la kwenye dini ni kuwa hakuna kuhoji....kilichoandikwa ni lazima kitekelezwe basi.Ila nitasema jambo moja hapa:

Siku moja nikiwa mjini Kondoa, nilikutana na mzee mmoja ambaye nadhani huyo alistahili sana kuwa daraja jingine kuliko alilonalo sasa....mzee ni mbishi huyo sikuwahi kupata kumwona mwingine kabla yake, maana yule anaweza kujikana hata yeye mwenyewe na akakuelewesha ukamkubalia.

Katika moja ya maongezi yake, mzee yule alinitupia swali akiniuliza kwanini niamini maandiko matakatifu, wakati enzi yanaposemekana kuanza kushushwa hakukuwa na teknolojia ya kuandika?, Alihoji kuwa kuna mlolongo wa watu wangapi hapo kati kati toka yaliposhuka siku ya kwanza hadi kufikia katika hali hii tunayoyaona hivi sasa?, alihoji pia kuwa, Je, nilikuwa na uhakika gani kuwa hapo katikati hakukuwa na kuchezewa kwa namna fulani kwa maandiko hayo (EDITING), ili yaendane na wakati, na kwamba katika mchakato huo tuna uhakika gani kuwa haya yalitoka kwa Mungu na haya yakatoka kwa waliokuwa wahariri :wa maneno ya Mungu"?

Nilikaa nikajiuliza sana, lakini pamoja na kuwa nilikuwa na imani yangu inayoniongoza, bado mzee huyo alikuwa na hoja. Hivi Haiwezekani kuwa watu wa sehemu zinazoitwa za kwenda Kuhiji, kuwa walifanya hivyo ili pia kunufaisha mataifa yao kupitia mafuriko ya watalii wa kipindi hicho?

Hivi kungekuwa na ubaya gani ikiwa, kungalikuwa na mgawanyo wa sehemu za kuhiji kwa mzunguko?, Hivi waisilamu walioko Marekani, ingekuwaje kama siku moja wangeambiwa tu kuwa Hijja inafanyika katika bara hilo?

Bado nitaendelea kulichambua suala hiuli kwa utuo, hasa maana dadangu Martha kaibua changamoto kubwa kichwani mwangu.....nitawasaka masheikh na mapadri au maaskofu kujua kwanini Macca....kwanini Vatican tu...Kwani Tanzania haiwezi kuwa ardhi takatifu....Tunatafakari

ndesanjo said...

Sehemu za kuhiji ziko nyingi sana Afrika na duniani kote. Mwarabu akienda kuhiji kwao sina ubaya. Mhindi akienda mto Ganges kuhiji au milima ya Himalaya sina tatizo. Tatizo ni pale sisi Waafrika tunapokuwa na tabia ya kwenda kuhiji kwa wengine tu. Kwetu hatuhiji na wao kwetu hawaji kuhiji. Tunaondoka hao kwenye Yerusalem, hao kwenda Roma, hao kwenda Maka. Yaani huko ndio mungu amebariki? Tusipofika hatua ya kutambua mambo mepesi mepesi kama haya, kuna mengine magumu yatatupa tabu sana.
Tazama kwenye uislamu hata kusali wanaelekea huko uarabuni. Mmasai akisali kwanini asielekee uliko mlima wa mungu (oldonyo lengai)?? Kwanini aelekee alikotoka Muhammad na sio nabii Lenana?

Post a Comment