Thursday, March 31, 2011

Babu hadi New York Times

Crowds Come Over Roads and by Helicopters for Tanzanian’s Cure-All Potion

By JEFFREY GETTLEMAN

Published: March 28, 2011

NAIROBI, Kenya — He’s a sensation in two countries. He’s snarled traffic for miles. He’s so popular that people have literally died waiting in line to see him. More

Ajali nyingine Mhhh! Yetu macho!

MTOTO wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Bw. Bernard Lowassa (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Oysterbay, Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma>>>Endelea.

Wednesday, March 30, 2011

Haba na Hana Ujaza Kibaba


Na Mwandishi Maalumu, Arusha

KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati limetangaza kiwango cha fedha ambazo zimekusanywa kutoka kwa wagonjwa wanaokunywa kikombe cha dawa ya Mchungaji Ambilikile Masapila kuwa ni sh milioni 50.>>>Endelea

Huu ndio Murgariga wa Babu

Waziri Lukuvi akikagua mti wa tiba Loliondo hivi karibuni


The ‘magic herb’ that has made thousands of people flock to remote Loliondo village in Tanzania was identified by Kenyan scientists four years ago as a cure for a drug-resistant strain of a sexually transmitted disease.

An expert on herbal medicine also said yesterday the herb is one of the most common traditional cures for many diseases. It is known as mtandamboo in Kiswahili and it has been used for the treatment of gonorrhoea among the Maasai, Samburu and Kikuyu. Endelea nayo>>>‘Magic herb’ is well known to Kenyan scientists

Nimeoteshwa dawa MUHIMU sh 5,000

Ni kama vile tumerogwa. Tunaamini kila kitu. Tumegeuka taifa la kuamini utabiri, ndoto na sasa imani ya mizimu.

1. Alianza Mchungaji (Babu) Mwasapila wa kule Samunge, Loliondo yeye akasema ameoteshwa na Mungu (labda). Yeye anatoa kikombea kimoja tu cha Mugariga au Mtandamboo unavyoitwa Kenya. Makumi, mamia, maelfu, malaki ya watu wanamiminika kwake na hakuna dalili na kuacha. Wengi wanasema wamepona. Serikali imeingia kichwakichwa, imetamka dawa haina madhara, naona inaelekea kuitambua rasmi<<Soma Hapa>>

2. Akaibuka kijana Jafar kule Mbeya (pichani). Yeye ameoteshwa na Mizimu ya marehemu mama yake. Tofauti na Babu huyu anatoa vikombe viwili vya dawa. Watu pia wanamiminika. Serikali ikajifaragua na kutangaza kumfungia. Wateja wake wakakasirika na kuandamana, hadi ikasalimu amri<<Iko Hapa>>.

3. Ikawa asubuhi ikawa jioni, akaibuka Bibi mwingine kule Tabora. Huyu bado natafiti taarifa zake, lakini kwa ufupi <<ziko hapa>> Pia Nasikia serikali imeahidi kumboreshea mazingira Bibi huyu ili atibu kwa raha mustarehe.

4. Nasikia pia mwingibne alijitokeza Rombo, sina taarifa zaidi alipotelea wapi.

Kwa hiyo, Kwa kuwa Watanzania kuamini jambo lolote ni kitu rahisi, nami natangaza kuwa nimeota dawa ya KUONGEZA PESA mfukoni. Malipo yake ni sh 5,000 kwa kikombe. Tuwasiliane.

Tuesday, March 29, 2011

Pia tujifunze kufikiria kinyume


Baada ya taarifa ya serikali hapo jana kueleza kuwa dawa ya Babu wa kule Samunge haina madhara, wengi wamefurahi, hasa wale waliopata kikombe.

Fikra kinyume inahoji, je, ingekuwaje kama ingebainika kuwa dawa hiyo inayotokana na mti wa Mugariga ina madhara kwa binadamu ambayo labda yangejitokeza baada ya muda mrefu?

Fikiria kwamba kila siku anatibu watu 2,000 (kama alivyodai) zidisha mara siku 180 (tangu Oktoba alipoanza) utapata= watu 360,000 (waliokunywa). Hivi hao, ndugu zao, marafiki zao wangekuwa katika hali gani?


Na tushukuru dawa hiyo iwe kweli imetoka kwa Mungu, kama sivyo hali itakuwaje hapo baadaye, baada ya 'NGUVU' iliyoitoa kubainika?

Kwa upande wa serikali iliyoamua 'kutibiwa' na kuivaa dawa hiyo kichwa kichwa, kana kwamba serikali inaongozwa kwa ndoto na utabiri, itakuwa na kauli gani?

Tafakari. Chukua hatua!

Monday, March 28, 2011

Dawa ya Babu haina madhara-Serikali

TAARIFA YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
KUPITIA TAASISI ZAKE ZA UTAFITI KUHUSU DAWA YA
MCHUNGAJI MSTAAFU AMBILIKILE MASAPILA WA SAMUNGE - LOLIONDO

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA), TAASISI YA UTAFITI WA DAWA ASILI YA CHUO KIKUU CHA AFYA YA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI, (MUHAS) MKEMI MKUU WA SERIKALI (CGC), TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU (NIMR)

Taarifa ziliifikia Serikali kuwa, Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, anatibu magonjwa sugu kwa kutumia dawa aliyooteshwa na Mwenyezi Mungu. Inasemekana kuwa, mchungaji alianza tiba hii tangu mwezi Agosti 2010, lakini watu wengi walianza kumiminika kwenda huko Samunge, kuanzia mwishoni mwa mwezi wa pili, mwaka huu wa 2011.

Kufuatia taarifa hii, serikali iliielekeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa, ufanyike haraka uchunguzi kuhusu dawa hii na itoe ushauri Serikalini ipasavyo. Baada ya kupokea maagizo hayo, wizara iliteua wataalamu kutoka taasisi zake tukiwemo sisi, TFDA, NIMR, Muhimbili kwa maana ya MUHAS, Mkemia Mkuu na tulijumuisha wataalamu wa hapa wizarani, ili kuifanya kazi hiyo muhimu, akiwemo Msajili wa Tiba Asili na Mbadala.

Hapo Machi 7 mwaka huu, sisi TFDA na wenzetu wanasayansi tulifanya safari kwenda Samunge kuonana na kufanya mazungumzo na Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila. Sisi TFDA na wataalam wenzangu wote, tunamshukuru sana mchungaji mstaafu, kwa ushirikiano na msaada mkubwa aliotupa sisi watafiti wote. kwa kuwa, tulifanya mazungumzo kwa masaa kadhaa kuhusu dawa hiyo jinsi alivyoanza, pia, alituonyesha mti unaotumika na alitupa sehemu mbali mbali za mti huo, kwa uchunguzi zaidi. Kadhalika, alituonyesha jinsi anavyotayarisha dawa hiyo na kutupatia sampuli yake iliyokwishategenezwa, tayari kwa matumizi. Sisi TFDA na wataalamu wenzetu tuliondoka nayo, kwa ajili ya uchunguzi zaidi, kwenye maabara zetu.

Baada ya kurejea kituoni Dar es Salaam, kazi ya utafiti wa dawa hiyo ilianza:

Jambo la kwanza kama watafiti, ilikuwa ni kuangalia na kuhakikisha usalama wa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila kwa watu. Uchunguzi uliofanyika, umetoa matokeo ambayo tumeridhika kuwa, dawa kwa kipimo anachotumia Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila, haina madhara yoyote yanayotambulika kwa sasa, kwa matumizi ya binaadamu.

Kazi inayofuata kwetu sisi watafiti baada ya matokeo haya, ni kuchunguza na kubaini, kama kweli dawa hii inatibu magonjwa hayo matano (5), kama anavyoeielezea yeye Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila. Uchunguzi huu utakapo kamilika, matokeo yake yatatolewa mara moja kwa wananchi wote!.

Hata hivyo, ninaomba kuwatahadharisha kuwa, hatua hii ya uchunguzi, si ya muda mfupi. Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kisayansi duniani, tafiti za namna hii zina mchakato unaohitaji muda wa kutosha kukamilisha hatua zake mbali mbali, na pia, kufikia viwango na vigezo vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa. Tunafanya hivyo kwa kuzingatia kuwa, dawa hii ni kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na inafuatiliwa na wananchi wetu na mataifa mbalimbali.

Sambamba na utafiti katika hatua hii, pia tunafanya uchambuzi wa kisayansi, katika maabara zetu, kwa sampuli tuliyoichukua kwa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa kuangalia mambo mengine mawili muhimu kama ifuatavyo:


1. Kwa hatua tuliyofikia na taarifa tulizo nazo za dawa hii mpaka sasa, tumeandaa na tunakamilisha taratibu, ili tuweze kufuatilia maendeleo ya kiafya ya wagonjwa 200, ambao wamekubali kwa ridhaa yao wenyewe, kushiriki katika utafiti huu, ili kuona maendeleo yao kiafya, baada ya kunywa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa maradhi walionayo. Hatua hii, inafuata vigezo vyote vya Kitaifa na Kimataifa.

2. Pia tumeweka utaratibu madhubuti, wa kufuatilia matumizi ya mti huu, kama “mmea tiba”, katika sehemu nyingine za nchi yetu, kwani tuna taarifa kuwa, makabila mbali mbali yamekuwa yakitumia mti huu kama tiba. Makabila hayo ni pamoja na; Wagogo, Wamasai, Wabarbaig na Wasonjo kule Samunge.

Kwa niaba ya watafiti na wataalam wenzangu, ninaomba nimalize kwa kusema kwa muhtasari kuwa:

1. Sisi sote tumeridhishwa kuwa, dawa anayotoa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, haina madhara yeyote yanayotambulika kwa sasa kwa matumizi ya binadamu. jambo hili mwazoni lilitia wasiwasi Serikali, Wataalam mbalimbali na wananchi kwa ujumla.

2. Kazi hiyo ya utafiti inaendelea ili kubaini magonjwa inayotibu,

3. Katika hatua hii, ninapenda kuwashukuru wataalamu wenzangu wote wa kikosi kazi cha wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya mkuu wa wilaya, Ngorongoro na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha na wananchi wote kwa kufanikisha zoezi hili mpaka sasa.

4. Pia sisi tunamshukuru sana Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa ushirikiano alioutoa, kwa timu ya watafiti waliofika kumuona, kuanzia siku ya kwanza mpaka leo hii..

Mwisho ninachukua fursa hii, kuwaomba wananchi wawe na subira katika kipindi hiki ili watupe nafasi tuweze kufanya kazi hii ya utafiti na uchambuzi zaidi, kwa utulivu na umakini wa juu kwani duniani kote, tafiti za aina hii, hazina njia ya mkato, nasi tunaahidi kwamba, tutatoa taarifa ya kina mara utafiti utakapo kamilika.

Asanteni na Ninawashukuru kwa kunisikiliza.

Serikali inapokunywa dawa

Kwa kawaida, mawaziri wetu wa Wakuu wa Mikoa wakitoa kauli kuhusu mambo fulani tunasema Serikali imesema au imeagiza. Sasa hivi 'Wakulu wetu' wanamiminika Loliondo kwa Babu kutibiwa, kwa nini tunashindwa kusema "Serikali inaumwa? Kumbuka: Babu alishasema kwake hakuna Kinga, kila anayekwenda anataka Tiba!

Askari Polisi akinywa dawa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi akiwa na Rose Nyerere, binti wa Baba wa Taifa, Mwalimu nyerere wakipata Kikombe cha Babu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Ezekiel Maige akipata kikombe cha Mchungaji Ambilikile Mwasapila juzi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Teresya Huvisa akipata kikombe.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk Yohana Balelel wakipata tiba ya mchungaji Ambilikile Mwasapile wa kijiji cha Samunge, Loliondo juzi.

Sunday, March 27, 2011

Babu Azuia wagonjwa wapya

Babu akitoa tamko la kuzuia wagonjwa wapya hadi Aprili Mosi. Isome hapa

Foleni yazidi kipimo, inadaiwa kufikia km 50 kutoka kwa Babu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na mwenzake wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Terezya Uvisa wakiwasili kwa Babu Loliondo kuzungumza naye kuhusu uwezekanao wa kuzuia maafa zaidi, kisha nao walipata kikombe chao: Kumbuka: Kwa Babu hakuna Kinga kuna Tiba.

Monday, March 21, 2011

Mambo yawa mambo kwa Gaddafi

Rais Muammar Gaddafi wa Libya mambo yanazidi kumwendea kombo baada ya majeshi ya Marekani na washirika wake kushambulia makazi yake. Haijulikani alipo. Soma zaidi>>>>

Haya ni baadhi ya madude yanayofanya kazi kule Libya. Inasemekana mtoto wa Gaddafi, Khamis, amekufa kwenye ajali ya ndege iko hapa. Hata hivyo, washambuliaji hao wa magharibi wanasema lengo lao si kumuua Gaddafi>>>Habari Kamili

Moja ya amashambulizi. Ni ya kushutukiza na nchi za magharibi zinasema hayatachukua muda

Haya ndiyo madege yao. Je, mwisho wa Gaddafi ni kama Saddam Hussein? Tusubiri tu muda.

Sunday, March 20, 2011

Askofu Mpya wa Dodoma


Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Mhashamu Gervas Nyaisonga katika Kanisa Kuu la Paulo wa Msalaba mjini Dodoma jana. Kama vile anamuuliza: "Na wewe utakuwa unanilima kama Pengo aliyekusimika?"

Wednesday, March 16, 2011

Kikao hiki kitaleta maisha bora?


President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete chairs a cabinet meeting at Dar es Salaam State House this morning (photos by Freddy Maro)

Tuesday, March 15, 2011

Loliondo sasa kumekucha

'Tiba Liliondo inaimarisha ndoa'

*Walioitumia wafurahia matokeo, wasimulia
*Mgonjwa atoka Afrika Kusini akiwa na drip
*Mzee apotea baada ya kunywa dawa ya babu

Na Gladness Mboma

DAWA inayotolewa na Mchunngaji Mstaafu wa KKKT (Babu), Bw. Ambilikile Mwasapile katika
Soma zaidi>>>>


Daktari: Mgonjwa Loliondo amepona Ukimwi

Mussa Juma, Loliondo na Deusdedit Moshi, Dodoma

DAKTARI Joachiam Mbosha wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Ngorongoro ya Wasso, amethibitisha kuwa mmoja wa wagonjwa wa Ukimwi aliyekwenda kutibiwa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile, maarufu kwa jina la
Soma zaidi >>>

Sunday, March 13, 2011

Dawa ipo ya kutosha Loliondo


Babu wa tiba amewaondolea wasiwasi wateja wake, akisema dawa bado ipo ya kutosha. Walioionja wanasema si chungu wala yenye ukakasi.

Waliokwishatibiwa, waelezwa ni kama tone la watakaotibiwa. Mashuhuda wanazidi kueleza inawatibu.

Kila mtu na maamuzi yake, kasheshe itabaki namna ya kufika huko. Msongamano, vumbi, ajali, nauli juu na mengine mengine. Lakini yote kwa yote bora uzima.

Tuesday, March 08, 2011

Dawa Loliondo kwa kila kiumbe!

Mgonjwa akiwahishwa

Kila mwenye kuamini anapata anachostahili

Maelefu wako kwenye msafara wakiwa na matumaini ya kwenda kwa Babu kupata dozi

Du! Simba hadi Mbagala!

Simba akiwa ndani ya gari la polisi lenye namba PT 2068 Landrover Diffender mara baada ya kuuawa na polisi eneo la Mbagala Kimbangulile Jumapili.

Askari Ismael Abdul mwenye bunduki aina ya G3 iliyotumika kummaliza simba aliyevamia eneo la Mbagala Kimbangulile Dar es Salaam Jumapili alfajiri.

Wednesday, March 02, 2011