Wednesday, March 30, 2011

Nimeoteshwa dawa MUHIMU sh 5,000

Ni kama vile tumerogwa. Tunaamini kila kitu. Tumegeuka taifa la kuamini utabiri, ndoto na sasa imani ya mizimu.

1. Alianza Mchungaji (Babu) Mwasapila wa kule Samunge, Loliondo yeye akasema ameoteshwa na Mungu (labda). Yeye anatoa kikombea kimoja tu cha Mugariga au Mtandamboo unavyoitwa Kenya. Makumi, mamia, maelfu, malaki ya watu wanamiminika kwake na hakuna dalili na kuacha. Wengi wanasema wamepona. Serikali imeingia kichwakichwa, imetamka dawa haina madhara, naona inaelekea kuitambua rasmi<<Soma Hapa>>

2. Akaibuka kijana Jafar kule Mbeya (pichani). Yeye ameoteshwa na Mizimu ya marehemu mama yake. Tofauti na Babu huyu anatoa vikombe viwili vya dawa. Watu pia wanamiminika. Serikali ikajifaragua na kutangaza kumfungia. Wateja wake wakakasirika na kuandamana, hadi ikasalimu amri<<Iko Hapa>>.

3. Ikawa asubuhi ikawa jioni, akaibuka Bibi mwingine kule Tabora. Huyu bado natafiti taarifa zake, lakini kwa ufupi <<ziko hapa>> Pia Nasikia serikali imeahidi kumboreshea mazingira Bibi huyu ili atibu kwa raha mustarehe.

4. Nasikia pia mwingibne alijitokeza Rombo, sina taarifa zaidi alipotelea wapi.

Kwa hiyo, Kwa kuwa Watanzania kuamini jambo lolote ni kitu rahisi, nami natangaza kuwa nimeota dawa ya KUONGEZA PESA mfukoni. Malipo yake ni sh 5,000 kwa kikombe. Tuwasiliane.

No comments:

Post a Comment