Thursday, March 05, 2009

Salva akerwa na habari ya Dowans

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu jana aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutoa maneno 'makali' dhidi ya gazeti la Mwananchi kuwa limepotosha kauli ya Rais Jakaya Kikwete. Vyombo vingi vya habari leo vimekariri taarifa hiyo kama ilivyotolewa. Gazeti lenyewe la Mwananchi toleo la leo limelazimika kujibu. SOMA MAJIBU yake hapa.

1 comment:

Anonymous said...

Salva ni mwanahabari mahiri na ana uzoefu wa muda mrefu katika medani za habari. Nadhani msingi wa teuzi yake kuongoza Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, ilitokana na kazi 'nzuri' iliyofanywa na gazeti lake la Mtanzania wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM.

Kufuatia kazi hiyo, na ile ya PR ya Richmond, Mkulu akaamini jamaa ni bingwa wa PR hivyo akamleta jikoni. Nimetokea kuona akiitisha press conference ni kulalamikia magazeti ambayo hayamripoti vizuri Mkulu. Kwa wanaojua newsroom politics ni kuwa 'Kichaa Kapewa Rungu'.

Hata ile issue ya Mwanahalisi, ni Mkulu alikasirika, Salva akapiga Tarumbeta, Mkuchika aweweseka na kupiga jaramba. Ilikuwa ni issue ndogo tuu ya Salva kumweleza Mkulu kuwa kwa mujibu wa katiba ya nchi na ya chama chake inaeleza wazi mwisho wa utawala wake ni 2010. Kueleza Kikwete mwisho wake 2010 kuna kosa gani?. Katiba ya CCM pia inatamka wazi 2010 ni mwisho wake ila atalazimika kuomba tena na chama kimpitishe. Pamoja na utaratibu wa CCM, rais aliyemaliza kipindi kimoja atapewa upendeleo, huu ni utaratibu tuu na sio katiba, hivyo hakuna kosa mwanaCCM yoyote kumpinga. Kubenea kusema kuna mpango wa kumpinga, kuna kosa gani?. Kwenye hili Salva ameonyesha udhaifu na hili la mwananchi pia ni udhaifu mwingine.

Sisi tumetawaliwa na Wakoloni Waingereza mpaka waandishi wetu wanaandika kukloni mwingereza. Wakitakiwa kuripoti kile tuu kilichosemwa bila analysis wala opinion.

Wamarekani wameenda mbali zaidi kwa mwandishi zaidi ya kuzisema zile 5 Ws and H, za Who, What, When, Where, Why and How, Mmarekani anazama zaidi 'So what, what does that mean and with what effect'.

Hiyo kauli ya Rais 'tusifungwe na sheria ya manunuzi katika miradi mikubwa ya umeme na vipindi vya dharura ilitolewa wakati huu wa mjadala wa Dowans ili iweje?. mwananchi wameenda deep zaidi kwa kuelezea kauli hiyo what does it means and with what effects.

Alichotakiwa kufanya Salva sio tuu kuiblast Mwananchi, bali alitakiwa afafanue hiyo kauli ya rais iliyonukuliwa ilikuwa na maana gani.

Waandishi wetu wengi ni 'parrot journalist' ambao hawana uwezo wa kunyambua kauli za viongozi, wao ni kuripoti tuu kilichosemwa kama kasuku.

Hata hivyo sio kosa la Salva, ndio majournalist wetu wengi walivyo, tena Salva ana bahati, kuna kichwa Premi Kibanga kiko chini yake. Premi akiwa BBC, alikuwa moto wa kuotea mbali, kaingia Ikulu, kamwagiwa maji, amepoa na kuwa baridi.

Tuangalie na upande wa pili, tusije mlaumu bure Salva, kumbe anaamrishwa tuu na kutekeleza amri, kumbe hivyo ndivyo anavyotaka Mkulu mwenyewe.

Post a Comment