Thursday, November 22, 2007

Haijapata Kutokea...Mabao 17-0!

Hii Kali.
Timu ya Taifa ya wanawake, Tanzania bara imewageuza urojo wenzao wa Zanzibar baada ya kuwachapa bila huruma mabao 17-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam. Katika mpambano huo, Asha Rashid alifunga mabao 8 peke yake, Ester Chaburuma mabao 6 na Fatma Mustapha mawili. Mechi hiyo ilikuwa ya kirafiki ya kumuwezesha kocha wa Timu ya taifa ya wanawake, Charles Mkwasa kuchagua timu moja ya Taifa ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake mwishoni mwa mwaka huu. Sambamba na ushindi huo, Timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars (wanaume) imeitandika ile ya Zambia, Chipolopolo, 1-0

3 comments:

KreativeMix said...

cool

Anonymous said...

Shenzi we unatishia mambo mapya mbona hana cha ajabu ama kwakuwa sasa blog inakwenda mbele?

Mzee wa Sumo said...

Sasa hivi blog yako inatisha Murangira!

Post a Comment