Sunday, April 09, 2006

Kiduka cha Luka Chabomoka

Jeff Msangi alivumbua kiduka hiki cha Luka, akauliza ni cha nani?. Luka mwenyewe alijitokeza. Baadaye Mimi, Miruko, nikapata picha yake (IONE HAPA). Wengi walikisifia sasa kiduka, lakini sasa Luka ameamua kukibomoa (labda kilijengwa pasiporuhusiwa). Amekiita www.bongo5.com

10 comments:

Anonymous said...

Bwana Miruko kwa kweli kiduka unaweza kusema ilijengwa mahala pasiporuhusiwa. Bongo5.com inavitu vytoe zilizokwepo katika kiduka na mengi zaidi. Karibuni sana bongo5.com

Sababu kubwa ni kwamba watu wengi wamelalamika kuwa jina la kiduka haikueleza lengo ya tovuti yangu. Natumaini bongo5.com inaeleweka zaidi.

Ningependa kupata maoni yenu kuhusu mabadiliko nilizofanya. Kiduka.com itarudi baada ya muda, lakini kazi yake itaendana zaidi na jina lake.

Luca

mwandani said...

Bwana Miruko saa nyingine nikifungua blogi yako inatokea kidirisha kinachosema nimeshinda maelfu ya fedha na tiketi kwenda kustarehe Bahamas. Kwa kuwa mimi ni mtu wa 10000 kugonga tovuti yako.
Hivi uliweka utaratibu huu au ni matapeli fulani tu wanataka kuniingiza mjini?

Habari Hub said...

Reginald

Sipendi kusema uwongo kiduka kilikuwa baab kubwa, tatizo la hii Bongo5 mambo yake yamejificha hayako hadharani kama kiduka ambacho ulikuwa mtembezi ukishafika dukani unafungua 'shelf' unalotaka lakini hii hapana.

Mshauri mshkaji wako arudishe kiduka kilikuwa supa sana.

Reggy's said...

Bwana Mwandani, mie sijaweka kitu kama hicho, labda matapeli wanatumia jina blogu yangu kukutapeli. Bila shaka wamebaini blogu zinazofunguliwa sana.

Kuhusu hoja ya Charahani, huyu mwenye kiduka kaniletea ujumbe kuwa sasa bongo5 iko kamili gado na kuwa Bongo Flava inapatikana kama kawa, nadhani kama unavyoshauri basi aziweke kama zilivyokuwa zimepangwa katika kiduka. bye

MK said...

muheshimiwa J. Nambiza Tungaraza naomba usi-respond ktk vitu kama hivyo maana hao ni wezi wanataka tarehe yako ya kuzaliwa, jina kamili na baada ya kupata hivyo tu wanatumia ktk kufanyia wizi kama kuombea mikopo, mortgages, credits cards na wizi mwinginine mkubwa.

Siku zote ogopa offer zozote za internet hasa hasa zingine zinasema tuma kiasi fulani cha pesa kupokea zawadi au wanasema piga simu kupokea zawadi na ukipiga simu line ina cost £1.50 kwa dakika na wanakuweka nusu saa hewani ukisubiri.

Kwa ufupi kuwa mwangalifu na popups, nenda ktk blog yangu na usome nakala moja kuhusu internet security kwa habari zaidi.

Nashukuru,
©2006 MK

MK said...

Rs Miruko nimeshamaliza hile kazi.nadhani utakuwa umeiona upande wa kulia ktk hii blog.


Nashukuru,
©2006 MK

John Mwaipopo said...

Miruko hivyo vikolombwezo ulivyoviweka bloguni kwako umevitoa wapi weye. Kizuri ni sharti ule na nduguyo.

Reggy's said...

Bwana Mwaipopo, mie si mchoyo. haya mambo yamewezekana kwa msaada mkubwa wa MK (www.vijimamboz.blogspot.com) na mengine, hasa Kijiwe cha Ghahawa, nimeigiza kutoka kwa Baba Said (www.msangimdogo.blogspot.com) katika huduma za Tag Board (http://www.tag-board.com)

Christian Bwaya said...

Miruko naomba nijue pa kuanzia kama nataka kuweka vile vidude vya kutafutia gazeti tando ulivyoweka kulia juu ya blogu yako. Nimevutiwa na jinsi vilivyokaa. Naomba maelekezo kwa kifupi. Tule wote mtaalamu au sio?

promoter 1 said...

mtoto akizaliwa hukaa kutambaa kisha kutembea ata angalia bongo inakua kila siku hongera san

Post a Comment