Saturday, July 16, 2005

Natabiri 'Story' ya Sumaye Itakuwa Hivi


Sumaye auza tani 100,000 za mahindi Kibaigwa

Dodoma Julai 18, 2006

Na Mwandishi Wetu
MKULIMA maarufu katika maeneo ya Kibaigwa mkoani Dodoma na Mvomero mkoani Morogoro, Frederick Sumaye, ameuza tani 100,014 za mahindi katika soko la Kimataifa la Kibaigwa.

Sumaye aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa miaka 10 mfululizo na mbunge wa Hanang, aliuza mahindi hayo aliyolima kwenya mashamba yake makubwa yaliyopo Kibaigwa na Mvomero, ikiwa ni karibu mwaka mmoja baaa ya kuacha madaraka.

Jana, Sumaye aliwaeleza waandishi wa habari kuwa mahindi hayo ni ya kwanza na anatarajia mavuno makubwa zaidi hapo baadaye.

"Kwangu kilimo kimo damuni, nimesomea kilimo na ninajua ninachofanya. Nitalima na kuendeleza kuwashangaza wengi. Hata hili soko la Kimataifa ninaweza kulijaza mwenyewe," alisema.

Sumaye (56), mwaka jana alijitosha kwenye kinyang'anyiro cha kuwania Urais wa Tanzania, lakini akatolewa na Halmashauri Kuu wa CCM na baada ya hapo akatangaza kutogombea ubunge.

Alipotangaza kuwa hatawania tena ubunge, ilidhihirika wazi kuwa hataendelea kuwa Waziri Mkuu kwa kipindi cha tatu, kwani Katiba ya nchi inaeleza kuwa Waziri Mkuu lazima atokane na wabunge wa majimbo.

Alianza kujihusisha moja kwa moja na kilimo cha mahindi baada ya muda wake wa uongozi kumalizika na anaamini kuwa kilimo chake kitakuwa na tija kwani hapo baadaye anatarajia kuanzisha teknolojia ya kupata mbegu za mahabara (GMO) zinazoweza kuzaa sana na kumpatia faida kubwa kuliko alivyokuwa kwenye siasa.

Mashamba anayotumia kuzalisha mahindi hayo yaliwah kulalamikiwa na watu wa kada mbalimbali wakiwemo

Hata hivyo yeye mwenyewe na Rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa walisema huo ni wivu tu, kwani kiongozi anastahili kuwa na shamba la mfano.

3 comments:

Rama Msangi said...

Mkulima mashuhuri aliyejipatia mashamba kwa njia zakutia mashaka enzi zake akiwa..... Haya bwana mie sina la tusubiri tuone utabiri wako, ila usije ukahamia kutabiri soka hata siku moja hata kama utabiri huu utafanikiwa kwa asilimia 100

Indya Nkya said...

Aisee hapo naona umegonga penyewe. Ataonyesha mfano toka rais mtarajiwa hadi mkulima.

Martha Mtangoo said...

Ni kweli bwana umejuaje? itakuwa hivyo kama ulivyoandika halafu mbaya zaidi hiyo Story itaandikwa na Regnald Saimon, Kibaigwa. wakati Bw. Rama Msangi atakuwa Mheshimiwa Mbunge wa kujitegemea.

Post a Comment