Tuesday, March 03, 2009

Dowans: Maswali Kuliko Majibu


Mjadala katika vyombo vya habari wiki hii ni kuhusu mitambo ya Dowans, iliyokuwa ya Richmond. Kinachohojiwa ni ama inunuliwe na serikali au la. Kama kawaida, magazeti ndiyo yanaongoza mjadala, Mwananchi linazungumzia jinsi serikali inavyotia hofu na hapa Nipashe linaeleza jinsi suala hilo lilivyopofusha macho ya Tanesco.

Maswali: Hivi ni lazima mitambo inayotakiwa kununuliwa iwe ni ya Dowans pekee?

Kwa nini sheria ya manunuzi ivunjwe na kununua mitambo 'chakavu' kwa maslahi ya watu wachache?

Kuna ulazima wa kubadili sheria ya manunuzi kama wanavyopendekeza Zitto na Tanesco?

Hawa watu wa serikai hawakuelewa mafunzo ya sakata zima la Richmond?

Kuna kweli wowote kuwa Tanesco wameupinga chenga uamuzi wa bodi na ule wa kamati ya Shellukindo?

Hivi Watanzania wanamuelewaje Zitto Kabwe?


Bado saa chache kupiga kura hapo juu, kulia

No comments:

Post a Comment