Tuesday, March 03, 2009

Taarifa ya Ikulu

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makubaliano makuu yaliyofikiwa katika mkutano wa tathmini ya utendaji wa Serikali uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumanne, Machi 3, 2009 kati ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake:

(a) Kwamba sekta ya madini isimamiwe kikamilifu kwa kuhakikisha kuwa wenye leseni za kutafuta na kuchimba madini wanazitumia kwa masharti yaliyoombewa, na kuwa wasiozitumia leseni hizo kwa kuzingatia masharti ya leseni hizo wanyang’nywe leseni hizo badala ya kuzitumia kuendesha ulanguzi tu.

(b) Kwamba zichukuliwe hatua za haraka kukomesha kabisa wizi wa mafuta ya transfoma ambao unasababisha hasara kubwa kwa taifa na kuruvuga mtandao wa kusambaza umeme kwa wananchi.

(c) Kwamba Kamishna wa Madini Nchini, kwa kutumia madaraka na mamlaka yake kisheria, achukue hatua mara moja kukomesha uchimbaji wa kokoto katika maeneo yasiyostahili, na hasa katika eneo la Kunduchi/Tegeta, Dar es Salaam ambako tayari Serikali ilikwishakupiga marufuku uchimbaji wa kokoto, lakini baadhi ya wachimbaji wamerudi katika eneo hilo kuendesha uchimbaji.

(d) Kwamba ziongezwe juhudi katika uzalishaji wa umeme nchini kwa sababu programu ya taifa ya uzalishaji umeme bado iko nyuma na bado liko pengo kubwa kati ya mahitaji halisi ya umeme nchini na umeme unaozalishwa kwa sasa.

(e) Kwamba dhana ya tenda na Sheria ya Manunuzi isiruhusiwe kuwa kikwazo katika miradi mikubwa mikubwa ya miundombinu ya nishati, hasa ile ambako wawekezaji wanajitokeza wenyewe kuwekeza katika maeneo ambako taifa linahitaji uwekezaji mkubwa na wa haraka na ambako nchi inaonekana ilichelewa kuwekeza. (hii imekaaje kuhusu Dowans?)

(f) Kwamba kasi iongezwe katika kuhakikisha kuwa maeneo yaliyoahidiwa umeme yanapatiwa umeme bila ucheleweshaji usiokuwa na sababu.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

03 Machi, 2009

No comments:

Post a Comment