Tuesday, March 03, 2009

Bongo Tambarare

Wazo Bonzo

Bongo yetu haina usumbufu. Pengine ni nchi pekee ambayo vituo vya redio tangu alfajiri vinachukua magazeti vinasomea wasikilizaji neno kwa neno, sentensi kwa sentensi, aya kwa aya hadi matangazo ya biashara...

Vipo piav ituo vya redio, vinapekuwa kurasa kwa kurasa na kuwaonyesha watazamaji habari zote za gazeti husika.

Pengine vituo hivyo havina mambo yao ya kutangaza muda wote, au vinawasaidia wasikilizaji wasiokuwa na hamu ya kujisomea wala pesa za kununua magazeti.

Hivi bado tutasema Bongo hakuna wasomaji wa magazeti? ...Hakuna anayelalamika, mambo mwendo mdundo.

No comments:

Post a Comment