Wednesday, November 26, 2008

Mashtaka KamiliMashtaka yalisomwa na Wakili wa Serikali, Stanslaus Boniface:

1. Matumizi mabaya ya ofisi kwa kuiruhusu kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers ya Uingereza kuingia mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria.
Kwa pamoja waliruhusu kampuni hiyo na mshirika wake, M/S Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation kusaini mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria ya Manunuzi ya Umma na ya madini.


2. Mei 28, 2005 watuhumiwa hao walitumia vibaya madaraka yao kuingia mkataba wa nyongeza wa miaka miwili kwa kampuni hiyo kuanzia Juni 14, 2005 hadi 23 Juni 2007 kinyume cha sheria ya Manunuzi ya Umma na ya Madini.

3. Kati ya Machi 28 ,2005 na Mei 28,2005 watuhumiwa wakiwa watumishi wa umma walitumia vibaya madaraka yao kwa kumwalika Dk Enrique Segura wa kampuni hiyo kurasimisha mkataba huo wa nyongeza ya muda kabla ya mazungumzo na timu ya serikali kushughulikia suala hilo.

4. Kati ya Machi 2005 na Mei 28, 2005 watuhumiwa waliachia suala la udhibiti wa madini lifanywe kienyeji bila kumshirikisha mwanasheria wa serikali kama ilivyopendekezwa na timu ya mazungumzo ya serikali, jambo lililosababisha ongezeko la muda wa mkataba huo wa miaka miwili.

5. Mramba alitumia vibaya mamlaka yake kwa kudharau ushauri wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wa kutotoa msahama wa kodi kwa kampuni ya M/S Alex Stewar (Assayers) Government Busines Corpotion.

6. Mramba peke yake kati ya Desemba 18 na 19, 2003 akiwa Waziri wa Fedha alitumia vibaya mamlaka yake kwa kutoa Tangazo la Serikali (GN) la mwaka 2003 lilitoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo katika shughuli zake za usambazaji wa bidha na utoaji huduma kinyume cha mapekezo yaliyotolewa na TRA.

7-11 Mramba akiwa waziri wa fedha anadaiwa kutoa misahama ya kodi ya mapato kwa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka yake kutoa hati za misamaha GN namba 424 /2003 na 497/2004 kati ya Desemba 19, 2003 na Oktoba 15, 2004 kinyume cha mapendekezo ya TRA.

12. Watuhumiwa hao wakiwa mawaziri kwa makusudi na kwa kutokuwa makini waliruhusu makataba ambao uliipa upendeleo kampuni hiyo na kuisababishia serikali hasara ya Sh 11,752,350,148.00.

133 Mramba akiwa waziri wa fedha kati ya 2003 na 2007, alishindwa kuchukua tahadhari katika, kutoa matangazo ya serikali namba GN 23/2003, 424/2003, 497/2004, 498/2004 , 377/2005 na 378/2005 yaliyolenga kusaidia kampuni hiyo kutolipa kodi na hivyo kuisababishia serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.

Hakimu Hezron Mwankenja aliruhusu dhamana kwa masharti kwamba:

Mosi, watoe pesa taslimu Sh3.9 bilioni kila mmoja.

Pili, wawasilishe hati zao za kusafiria

Tatu, wasitoke nje ya Dar es Salaam

Nne, wawe na wadhamini wawili waliothibitishwa na mahakama.

Walishindwa kutimiza masharti hayo kwa jana, na sasa wananyea ndoo Keko

No comments:

Post a Comment