Monday, May 02, 2011

Nani kulamba kitita cha Osama?

Mwili wake umeshazikwa
Dunia nzima sasa inazungumzia kifo cha Osama Bin Laden, yule anayeaminika kuwa ndiye gaidi nambari one. Kwa kujikumbusha tu ni kwamba marekani iliahidi $1,000,000 kwa yeyote atakayempata ama akiwa hai au amekufa. Sasa nani atalamba kitita hicho? Wengi bado wanajiuliza kweli kafa au 'imetengenezwa' na Marekani?
Jinsi alivyouawa imeandikwa kwa kina CNN. Tunasubiri kuona mwili wake. Kwenye mtandao nimepata picha hii, ya kweli au imepikwa? Maiti yake huenda isionekane kwani itahudumiwa kwa taratibu za Kiislamu. Lakini taarifa za karibuni kabisa kutoka Reuters, The New Yolk Times zinasema Osama ameshazikwa. Tuendelea kujadili huku ukweli ukijidhihiri.

No comments:

Post a Comment