Wednesday, May 18, 2011

Gamba limekwamia shingoni?

TAFAKARI YA LEO
Sekretarieti ya CCM chini ya Wilson Mukama hivi karibuni ilianza kampeni mikoani kuelezea maazimio ya NEC kuhusu KUJIVUA GAMBA. hadi sasa wametembelea mikoa kadhaa, ikiwamo Dodoma, Morogoro, Iringa, Singida na sasa Mara.

Walianza na moto mkali kwa kusema wangetoa barua za kuwataka mafisadi wajivue gamba ndani ya siku 90, baadaye wakasema hakuna aliyetamka idadi ya siku, bali ni hadi mkutano mwingine wa NEC. Wengine wakadai hayo yahakuwa maamuzi ya NEC, wanabishana wenyewe kwa wenyewe.

Msemaji wao, Nape Nnauye ndiye anayesikika zaidi hadi watani zao wamemwita 'vuvuzela', anasisitiza kuwa uamuzi huo uko pale pale, kwamba mafisadi ama watajitoa au wataondolewa na barua zitatoka. Yeye anasema walitajwa kwenye vikao, wengine wanasema hawakutajwa. Yetu macho, tunasubiri atakayejitoa mwenyewe ili tujue kuwa ndiye fisadi.

Ghafla wimbo ukaanza kubadilika, chorus ya 'mafisadi ndani ya CCM' ikabadilika, akaanza wimbo mpya mpya kuwa yeye anapambana na mafisadi wote, hata 'mafisadi wa CHADEMA' wanaopimwa kwa kulipwa mshahara mkubwa. Wimbo huu mpya ukazua malumbano makali na watani zao, misheni ya Sekretarieti ikabadilika, wakaanza mapambano ya maneno. Lengo la watani zao la kuwang'oa kwenye reli ili washindwe kuwaondoa mafisadi
likatimia.

Hivi sasa watuhumiwa wa ufisadi roho kwatuuuu! Wanafuarahia mlio wa mavuvuzela, wanamtazama Nape, Mukama, Mwigulu (Chiligati mjanja, hasikiki) wakipambana na CHADEMA, muda unakwenda, mwisho wa siku watapimwa kwa yafuatayo:

1. Kutoa barua za mafisadi ndani ya muda katika ngazi zote
2. Kuwaondoa kwenye chama (kujivua gamba) ndani ya muda
3. Kurudisha imani ya wanachama kwa chama chao cha wakulima na wafanyakazi
4. Kurudisha wanachama waliohama/ kupata wapya baada ya kupata gamba jipya, na mwisho itakuwa ni:
5. Kuwashughulikia 'mavuvuzela, endapo watashindwa kujivua gamba na kuliacha mabegani kama picha inavyooneshwa hapo juu.

No comments:

Post a Comment