Wednesday, April 27, 2011

Kisa cha Mapacha Watatu

Mchezo wa kujivua gamba ndani ya CCM umefikia mahali patamu. Ninapoufikiria, ninapata tu maswali. Makosa majibu, kwani mambo mengi ambayo baadhi ya watu walioko wa upande wa mapacha hao wanadai ndiyo majibu, si majibu wala si hoja. Ni kauli tu za kujitetea. Mwalimu wangu wa Logic alinieleza kuwa ni Fallacies.

Mfano,
Mosi, wapo wanaosema: "Si wao tu, wapo wengi hawa wametolewa kafara. Maneno haya hayaelezi kama wao hawasiki, kama yangeleeza hivyo ningesema kuna hoja.

Pili, wapo wanaosema hata Mukulu wao ni miongoni mwao, hii yaweza kuwa sahihi, lakini haileti majibu kwamba, kama Mukulu naye yumo hastahili kuchukua hatua dhidi yao.

Tatu, wapo wanaosema kinachofanyika ni vita ya urais 2015, na hii masikioni ni sahihi, lakini haisema kama kilichofanyika dhidi yao ilikuwa stahili yao au wanaonewa.

Nne, wapo wanaosema mmoja wao atageuka kuwa 'kama' Jacob Zuma wa Afrika Kusini, lakini hawana majibu kama 'madhambi' ya Zuma na mazingira yake yanafanana na madhambi ya huyo pacha, wala kama madhambi ya Zuma yalikuwa na impact ya moja kwa moja kwa maisha ya wananchi wa Afrika Kusini, kama ilivyo madhambi haya.

Tano, wapo wanaosema wanachafuliwa kwa sababu mbalimbali, lakini hasemi kama bila kuchafuliwa mapacha hawa ni wasafi. Yapo na maswali mengine mengi, ukitaka ongezea.

No comments:

Post a Comment