Thursday, January 06, 2011

BBC yaripoti 10 kuuawa Arusha

Watu wasiopungua kumi wameripotiwa kuuwawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Arusha Tanzania, kwenye makabiliano baina ya Polisi na wafuasi wa chama cha upinzani cha CHADEMA.

Ghasia zilianza baada ya Polisi kumkamata mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema, wakiwa wanaelekea kuhutubia mkutano wa kisiasa. >>>Endelea BBC

Mke wa Dk. Willibrod Slaa, Bi. Josephine Mushumbusi, baada ya kujeruhiwa, kisha kukamatwa na polisi jijini Arusha jana.

1 comment:

emuthree said...

Haya na hii ndio Afrika yetu, sijui lini tutaondokana na hili...nani wa kulaumiwa, kila mmoja ana lake kichwani, lakini mimi kinachoniuma ni kuwa wanaoumia ni wengine na mwisho wa siku wanafaidi wengine!

Post a Comment