Thursday, January 06, 2011

Watatu wathibitika kuuawa na polisi

Taarifa rasmi kutoka polisi Arusha zimethibitisha kuwa watu watatu wameuawa kwa kupigwa risasi. Muda huu polisi walikuwa wanajiandaa kuwapeleka watuhumiwa, akiwamo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa na wafuasi wengine wa chama hicho mahakamani, lakini shughuli imesitishwa.

Taarifa kutoka Arusha zinasema mamia ya wafuasi wa Chadema kutoka Kilimanjaro, Karatu wametinga mjini AR kwa mabasi, na FFU wameanza upya kurusha mabomu.

No comments:

Post a Comment