Monday, November 22, 2010

Zitto alivyotofautiana na wenzake

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe amesema uamuzi wa kutoka nje ya bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akihutubia ulikuwa wa chama uliofikiwa kwa kura lakini yeye hakukubaliana nao, ndio maana aliamua kutokwenda bungeni siku hiyo.

Akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha TBC1, Bw. Kabwe alisema yeye asingeweza kuingia bungeni na kutoka wakati Rais Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, na ambaye amefanya mambo mengine mkoani Kigoma kuliko marais wengine.

"Kuliko kuingia na kubaki ndani wakati wenzangu wanaondoka, kitu ambacho kingekuwa kibaya zaidi, niliona ni bora kutoingia kabisa kwa kuwa rais ndiye alama ya bunge na amiri jeshi mkuu," alisema.

Bw. Kabwe ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, alisema ni kweli waliafikiana kwa kura na walio wengi wakaafiki kutoka lakini yeye alitofautiana, pamoja na kutambua kuwa chama kinaweza kuchuykua hatua, kwani hiyo ndiyoi gharama ya demokrasia.

Hata hivyo, alisema uamuzi huo usifikiriwe kuwa ni mgawanyiko amekanusha kuwa jambo hilo lisifikiliwe ni mgawanyiko bali mtazamo tofauti wa mawazo. Source: Majira

2 comments:

Anonymous said...

ndio demokrasia hiyo

Anonymous said...

Huyo ni Mrema mwingine yuko jikoni. Ni kijana anayefikiri ana akili kuliko viongozi wengine wa chama chake. Wenzake walioamua ku walk-out ni mashujaa - tutawakumbuka milele. Ndio wanaofanya leo hii jamii iendelee kujadili suala hilo na hiyo ndio petroli ya mjadala wa kuleta maendeleo. Enzi za 'ndiyo mzee; zilikufa pale tulipoamua kurejesha siasa za vyama vingi.

Post a Comment