Rais Jakaya Kikwete
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
WIZARA NA MAWAZIRI WAKE:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
1.Utawala bora, Mathias Chikawe
2.Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira
3.Menejiment ya Utumisi wa Umma – Hawa Ghasia
Ofisi ya Makamu wa Rais
4-Muungano-Samia Suluhu Hassan
5-Mazingira - Dk. Terezya Luoga Hovisa
Ofisi ya Waziri Mkuu
6.Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi
7.Uwezeshaji na Uwekezaji, Dk. Mary Nagu
8) Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Mkuchika
Manaibu: Aggrey Mwanri na Kassim Majaliwa
9) Wizara ya Fedha, Mustapha Mkullo
Manaibu: Gregory Teu na Pereira Ame Silima
10) Wizara ya Mambo ya Ndani-Shamsi Vuai Nahodha,
Naibu: Balozi Hamis Kagasheki
11) Wizara ya Sheria na Katiba: Celina Kombani
12) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa: Bernard Membe
Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi
13) Wizara ya Ulinzi na JKT: Dk. Hussein Mwinyi
14) Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi: Dk. Mathayo David Mathayo
Naibu: Benedict Ole Nagoro
15) Wizara ya Mawasiliano Sayansina Tenknolojia: (Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Naibu: Charles Kitwanga (mawe matatu)
16) Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka
Naibu: Goodluck Ole Madeye
17) Wizara ya Maliasili na Utalii: Ezekiel Maige
18) Wizara ya Nishati na Madini, William Ngeleja,
Naibu: Adam Malima
19) Wizara ya Ujenzi: John Magufuli
Naibu: Prof. Harrison Mwakyembe
20) Wizara ya Uchukuzi: Omary Nundu
Naibu: Athuman Mfutakamba
21) Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Cyril Chami
Naibu: Lazaro Nyalandu
22) Wizara ya Elimu: Dk Shukuru Kawambwa
Naibu: Philipo Mulugo
23) Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii: Dk. Hadji Hussein Mpanda
Naibu: Dk. Lucy Nkya
24) Wizara ya Kazi na Ajira: Gaudencia Kabaka
Naibu: Dkt. Makongoro Mahanga
25) Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto: Sophia Simba
Naibu: Umi Ali Mwalimu
26) Wizara ya Elimu Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo: Dk. Emmanuel Nchimbi
Naibu: Dk. Fenella Mukangara
27) Wizara ya Ushirikiano EAC, Samuel Sitta
Naibu: Dk. Abdallah Juma Abdallah
28) Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Prof Jumanne Magheme, Naibu: Christopher Chiiza
29) Wizara ya Maji, Prof Mark Mwandosya
Naibu: Eng. gerson Lwinga
Kabla ya kutangaza, Rais Kikwete alisema haya:
Katika Muundo wa Serikali hakuna mabadiliko makubwa isipokuwa yafuatayo:
1.Idara ya Umwagiliaji tumeiunganisha na Kilimo ambako ndipo ilipokuwa zamani.
a.Imeonekana upangaji wa maendeleo ya kilimo unakuwa hauna hakika bila ya umwagiliaji kuwa sehemu ya kilimo. Tuliihamishia maji kurahisisha pia upangaji na hasa kwa vile maji ndiyo wanaotoa haki ya matumizi ya maji.
b.Kwa kuwa tatizo la uhaba wa maji ya binadamu ni kubwa sana na tunataka tuongeze kasi ya kukabiliana na tatizo hilo tumeona tuiondolee wizara hii mzigo wa umwagiliaji ili ibaki na kazi moja tu ya kuhakikisha kuwa watu wanapata maji safi na salama mita 400 kutoka wanapoishi.
2.Idara ya Vijana tumeihamisha kutoka Wizara ya Kazi na kuihamishia Wizara ya Habari kwa sababu kuu 2.
a.Kwanza inashabihiana na michezo na utamaduni.
b.Tunataka Wizara ya Kazi ipate muda wa kutosha wa kushughulikia masuala ya ajira na wafanyakazi ambayo sasa yamepanuka.
3.Shughuli za Uwezeshaji wa Wananchi zilizokuwa Wizara ya Fedha na Wizara ya Kazi zitahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu.
4.Marekebisho mengine ni madogo:
a.Katika Ofisi ya Rais tunairudisha shughuli ya mahusiano na jamii hivyo tunaongeza Waziri wa Nchi ambaye pia atashughulikia shughuli zilizopanuka za Tume ya Mipango, MKURABITA na TASAF.
b.Katika Ofisi ya Waziri Mkuu tutakuwa na Waziri wa Nchi wa kushughulikia Uwekezaji na Uwezeshaji wa Wananchi.
c.Katika Ofisi ya Waziri Mkuu Wizara ya TAMISEMI tumeongeza Naibu Waziri wa kushughulikia masuala ya Elimu.
Baada ya kusema hayo nitangaze orodha yetu:
Nitawaapisha Jumamosi tarehe 27 Novemba, 2010 saa 05:00 asubuhi
1 comment:
Tunashukuru kwa Baraza lako hilo japo kuna wengine hatujaona kama wamefanya kitu chochote kile katika awamu iliyopita, kama Makongoro mahanga, Sophia Simba angebaki tu na UWT yake, na Lukuvi je ataweza hiyo shughuli. Hofu na mashaka pia ipo kwa huyu mama Celina Kombani je naye ataweza kuleta usawa wa na katika kipindi hiki tunataka kuundwa kwa katiba mpya. aache mambo yake ya Bagamoyo. please.
Post a Comment