Waandishi Wetu
HALI bado si shwari baina ya Jeshi la Polisi na Chadema baada ya chombo hicho cha dola kukizuia chama hicho kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima "hadi hapo hali itakapotengemaa".
Lakini hakuna ofisa wa jeshi hilo aliyekuwa tayari kutoa maelezo bayana kuhusu amri ya kuzuia maandamano ya Chadema kwa kisingizio hicho, huku kila mmoja akirumshia mpira mwenzake na mwishoni kutaka aulizwe Waziri Mkuu au mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ambaye hata hivyo hakupatikana. Isome Mwananchi. Chama hicho kimelalamika na kulaani kitendi hicho namna hii;
CHADEMA yalaani kuzuia mikutano
*Yatoa sharti kushirikiana na CUF katika bunge
Na Tumaini Makene
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi, kuzuia mikutano ya wabunge wake na mingine ya hadhara ya chama hicho, kikidai kuwa ni
dalili za wazi za 'kuminya haki za raia, kuvunja sheria ya haki, kinga na mamlaka ya bunge na kukaribisha dola ya kipolisi' nchini.
Kimesema kuwa vitendo vya Jeshi la Polisi, vinashiria hatari kwa demokrasia nchini, haki za kikatiba na za kisheria za wananchi, huku kikitoa mifano ya dhana hiyo ya dola ya kipolisi (police state) ni kama vile ilivyokuwa katika nchi za Zimbabwe, Afrika Kusini wakati wa utawala wa makaburu; na Kenya wakati wa utawala wa Rais wa Pili, Daniel Arap Moi. Hii iko Majira
1 comment:
Hivi hawaoni kuwa kwa ukifanyia chama hicho mizengwe ndio kinapanda chati...mimi sioni ubaya wa mikutano, waache wafanye kama watazungumza baya, sheria ipo!
Post a Comment