Monday, September 27, 2010

Wakataeni wagombea wanaowahonga-Pengo

Na Peter Mwenda

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo amewataka wakristo kufuata dhamira ya Mungu ya kuchagua viongozi ambao hawawarubuni kwa khanga, bia na fulana.

Akihutubia waumini katika ibada ya kuombea amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi mkuu iliyofanyika katika Kijiji cha Hija, Parokia ya Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema wakristo wakatoliki wajue kwamba kura zao zina thamani kubwa kwa jamii na mbele ya Mungu.

"Kama mngejua thamani ya kura yako kwa jamii na mbele ya Mungu huwezi kupokea zawadi za khanga na bia kwa ajili ya kumpigia mtu asiyefaa kupewa kazi ya kuongoza," alisema Kadinali Pengo.>>>Endelea

1 comment:

Adela Dally Kavishe said...

ila inakuwa vigumu sana watu kukataa hongo ndio maana

Post a Comment