Thursday, September 30, 2010

Nimeipanda Hii

Hii ni picha iliyochorwa na msanii kuonyesha mandhari ya Hotel ya Mount Meru itakavyokuwa pindi ujenzi utakapokamilika na kufungua milango yake kwa wageni. Hoteli hii iliyopata kuvuma miaka ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini inatarajia kufunguliwa rasmi mnamo mwezi Novemba mwaka huu. Itarudi tena ikiwa ktk hadhi ya nyota 5 na kuahidi ushindani mkubwa ktk sekta ya huduma za malazi ktk miji ya Arusha na Moshi. Picha hii nimeichukua T-E-M-B-E-A Tanzania. Nimeipenda Sana hii blog kwa kuitangaza nchi yetu na vivutio vyake.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli umefanya vizuri kuitangaza nchi yetu kwa ni jukumu letu ili nasi nzhi yetu ijulikane. Kwani inavivutio vingi sana lakini utakuta vinasemwa vile vibaya tu na vile vizuri vinafichwa kapuni.

Post a Comment