Thursday, March 19, 2009

Yaliyojiri kwa Mwakyembe

Dk. Mwakyembe alionyesha kukerwa na baadhi ya wanahabari wanaotumiwa kuwachafua watu kwa maslahi ya wachache na si ya taifa na taaluma nzima ya habari.

Waandishi wa habari lazima mzingatie maadili ya taaluma yenu na msikubali kutumiwa na baadhi ya watu kuwachafua wengine kwa sababu kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya taaluma, ambayo kwa sasa imeingiliwa na ni jukumu lenu kuilinda,” alisema.

Alisema kuna wanasiasa waliochafuka kutokana na matendo yao machafu kwa jamii na kwamba, wanatumia wanahabari wasio waadilifu kuwasafisha na kuwafichia maovu, lakini kuna wengine hawawezi kusafishika.

Kutokana na kauli hiyo ya Dk. Mwakyembe, aliyeonyesha magazeti yaliomchafua, baadhi ya wanahabari waliingia kwenye mgawanyiko, jambo lililomfanya mwanasiasa huyo, ambaye kitaaluma ni mwanasheria kukatisha kujibu maswali na kuwasuluhisha.

Mmoja wa waandishi, alihamaki na kubishana huku akitetea habari iliyoandikwa katika gazeti lake, iliyoshutumiwa na Dk. Mwakyembe.

Kutokana na kutetea huko, mwandishi wa habari mwingine, ambaye gazeti lake halikushutumiwa, alimtaka kunyamaza kwa sababu yeye naye ni mwandishi kama walivyo wengine.

Mwandishi huyo aliyekuwa akilitetea gazeti lake, alijibu kwamba, hata kama yeye ni mwandishi wa habari kama walivyo wengine, lakini huyo asijifananishe na yeye.

Hivi karibuni kumezuka mjadala mkubwa kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuonyesha nia ya kutaka kununua mitambo ya Dowans, jambo lililopingwa na baadhi ya wabunge wakisema ni kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma. TANESCO baadaye ilitangaza kuachana na mpango huo. Chanzo:
Gazeti la Uhuru. Note: Gazeti halikutaja majina, bado yanatafutwa.

1 comment:

Anonymous said...

Majina hayakutajwa nini, sema unawaogopa Kubenea na Balile. Kubenea amtetea mwakyembe na balile alilala upande wa bosi wake rostam

Post a Comment