Saturday, March 07, 2009

Wito: Dk Rashid Ajiuzulu

Baada ya kauli yake ya kususa na kuiachana na ununuzi wa mitambo ya Dowans, lakini bila kutoa wazo mbadala la upatikanaji wa umeme na kuishia 'kuwatisha' Watanzania kuwa yeye Dk Idrisa Rashid na Tanesco, 'wasilaumiwe nchi ikiwa gizani, hospitali kukosa umeme na uchumi kuporomoka Habari Kamili, watu wengi wamesema 'hana jipya' hivyo ajiuzulu, awapishe wengine watakaokuja na mawazo mapya ya kufua umeme tofauti na haya ya kifisadi.
Mmoja aliandika hivi:
"Wananchi wasiadhibiwe kwa kukataa mafisadi kuwatumia kuwaibia. Kama Idris Rashid anatutisha ilhali akiwa mkuu wa shirika letu, awajibishwe mara moja kama umeme utakatika. Kwanini mitambo chakavu ambayo haijawahi kuzalisha umeme iwe tegemeo letu?Hii ni hujuma na ufisadi vinavyonuka. Na ni changamoto kwa nia ya kuleta maisha bora kwa wote kwa rais Jakaya Kikwete. Je watanzania watakubali kuchezewa mahepe mchana kweupe? Rashid jibu tuhuma za ufisadi katika deal la rada na uwajibike mara moja.Pia hujuma ya kutaka kununua mitambo chakavu ya IPTL ipingwe kwa nguvu zote kama ilivyofanyika kwa Dowans.

No comments:

Post a Comment