Friday, March 06, 2009

Uporaji kweupe Dar

Leo asubuhi, nikiwa kwenye foleni maeneo ya jangwani, saa 1.20 asubuhi, gari la tatu kutoka gari langu kwa nyuma lilivamiwa na vibaka, wakafungua milango, ndani ya kama dakika 3 wakapora kila walichoweza kupora.
Ilikuwa ni kwenye foleni, jamaa wana visu, na kila mtu akawa anaangalia kama sinema hivi. HAKUNA MSAADA!
Watu kwenye daladala la karibu, wakawa wametulia kimyaaaaa. Na walio kwenye saloon cars wakawa wanafunga vizuri vioo ili wasiwe next target.
Siku zote hizi WARNING nilikuwa sizipi uzito unaostahili, leo nimekubali. Naomba munielewe, Sizungumzii mtu kupora cheni au simu dirishani.
Jamaa wamefungua milango, na kunyang’anya kila walichokifikia. Tafadhali sio tu ufunge vioo, lakini hakikisha milango imefungwa ( LOCKED) BONGO TAMBARAREEE!
Mdau OCTAVIAN ‘OC’

No comments:

Post a Comment