Friday, March 06, 2009

Huyu Binti Apewe Msaada

Watu mbalimbali waliozungumzia suala la huyu binti, Miss Tanzania (2006) na vituko alivyotoa katika Mahakamaya Wilaya Kinondoni na kuanza kukwaruzana na wazazi wake waliomwekea dhamana katika kesi yake ya kuharibu gari la Msanii Stephen Kanumba wanapendekeza atafutiwe wataalamu wa Saikolojia ili apewe msaada utakaobadili akili zake. Wengi wamesikitishwa na kitendo chake cha kutaka kukimbilia kwa mpenzi wake, Jumbe Yusuf na kumuacha solemba mama yake mzazi aliyemwekea dhamana ya Sh 500,000. Habari Leo limepata taarifa zake kamili na za kina.

No comments:

Post a Comment