Sunday, March 01, 2009

Profesa Safari Akerwa Kushindwa

Prefesa Abdallah Safari, aliyekuwa mgombea Uenyekiti, CUF na kuambulia kura sita (6), anakusudias kutunga kitabu kuelezea kukerwa kwake, bila shaka haya yatakuwamo:

"Sikufurahishwa na uchaguzi ule kwa ujumla. Wamenidhalilisha sana
kwa kuniuliza maswali ya kipuuzi na kusahau mchango wangu katika chama.

“Mimi nilijitolea kama wakili kukitetea chama mpaka nikafukuzwa kazi katika chuo cha Diplomasia. Sikujali nikaendelea kukitetea chama changu. Ilifika mahali nikampoteza baba yangu mzazi nikiwa nakihangaikia chama, halafu leo nakuja kuulizwa maswali ya kipuuzi vile?” alihoji na kuongeza:

”Siku ile nilikuwa na familia yangu, mke na watoto wangu, nao walihuzunika kuliko hata mimi.

”Kwa hiyo sasa natunga kitabu changu ambacho kitaitwa ‘Haja ya kuwa na Tume huru ya Uchaguzi’. Humo nitaeleza kila kitu ikiwamo hatima ya uanachama wangu ndani ya CUF,” alisema Profesa Safari.


PATA HABARI KAMILI

No comments:

Post a Comment